Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,713
Ni kweli kabisa ni risk ambayo inachukuliwa,kwasababu ukishaanzisha mahusiano unaweza gundua tabia kuhusu rafiki yako ambazo hukuwa unazijua awali,mfano wivu wa kupindukia hasa kwa ule upande ambao ulikuwa na hisia.Au ulikuwa unajua baadhi ya tabia za rafiki yako lkn mwanzo hukuona big deal,lkn mkishaanza kudate na kujicommitt unaona tabia hizo ni kero mfano unajua rafiki yako mahusiano yake ya awali hakuwork kwasababu anaplan mahusiano kama business?Je utambadilishaje mtu kama huyo ambae anataka kuwa in control all the time?kila kitu kina faida na hasara, unaweza kuwa usivyomdhania, utakuwa dissapointed, na waweza poteza rafiki.
je kama mahusiano hayatowork unafikiri wanaweza kuwa marafiki kama awali?Mahusiano huwa yana miiko na mipaka ambayo wahusika hupaswa kuweka bayana baina yao...
Binafsi naamini mahusiano yenye kujengwa katika misingi ya urafiki juwa imara zaidi...
Mapenzi ni kama mmea ambao huanza katika hali ya mbegu, baadaye mche na hatimaye mmea kamili...
je kama mahusiano hayatowork unafikiri wanaweza kuwa marafiki kama awali?
Inawezekana kabisa lakini ni jambo linalotegemea uelewa wa wahusika...
Kuna kitabu kimoja cha mahusiano nishawahi kukisoma, mwandishi anashauri usijaribu kuanzisha mahusiano ya kirafiki na mwanamke au mwanaume ambaye unadhani utakuja anguka kwa penzi lake...
je kama mahusiano hayatowork unafikiri wanaweza kuwa marafiki kama awali?
Hapa tunaongelea marafiki wa kawaida tu ambao hawajawahi kuivuka mipaka ya urafiki yaani hawajahusisha tamaa za kingono!Kwanza tuijue mipaka ya urafiki ni ipi?? Kuna mambo wanafanya watu walio kwenye mahusiano yakimapenzi, lakini mambo hayo hayo wanafanya pia watu marafiki tu na wala sio wapenzi...