mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 12,210
- 9,032
Kama Lowassa aliwajibika kwa kosa ambalo hakulifanya bali waliokuwa chini yake, PINDA anasubiri nini kuwajibika? Kwanini Bunge haikuunda kama teule kuchunguza kashfa hii ambayo ni kubwa kuliko ile ya Richmond? Kwanini Bunge linaogopa kujadiliwa kwa Taarifa ya PCCB?... Kwanini tusiamini kuwa the very persons waliohusika kwenye sakata la Richmond ndiyo hao hao waliokomba fedha zetu via ESCROW a/c? Kwanini tusiamini kuwa LOwassa alitolewa pale ili Ufisadi uweze kutamalaki! Maana ushahidi unaonyesha kuwa Baada ya Lowassa kutolewa ndipo mikataba Zaidi ya Madini na Gesi yaliposainiwa Zaidi; hii inathibitishwa na kauli ya Lowassa kuwa alimshauri Rais kuvunja Mktaba wa Richmond only Rais kumkatalia kwa maelezo kuwa hiyo ni upepo na utapita tu! Na hata baada ya kubainika kuwa Miraji alikuwa one of the beneficiary! Akina Sitta na Membe walienda mbali Zaidi kwa kumdanganya JK kuwa Edo alikuwa anaandaa mpango wa kumpindua!!! ... Sasa JK anajua Ukweli kuwa alifanya Makosa kumtosa Edo! Sasa anajua kuwa Mikakati ya mahasimu wake ni kumhujumu via familia yake mwenyewe!!! Hope this time Mr President atawachinjilia baharini wote na kumrejesha Lowassa kumalizia ngwe yake ....
Kama Lowasa hakulifanya basi asingewajibika kujiuzuru,Tanzania hatuna utamaduni wa kujiuzuru kwa jambo ambalo hujalifanya wewe moja kwa moja,na ndio maana Hussein Mwinyi hakujiuzuru kwenye tafrani ya mabomu ya Mbagala,ni baba yake tu Mzee Mwinyi ndie aliye wahi kujiuzuru kutokana na makosa yalifanyika chiniya wizara yake ,wakati wa Mwl Nyerere.