Fresh news: Ukweli kuhusu mgomo wa madaktari - part II

Hili litakuwa fundisho kwa serikali DHAIFU kama ya jakaya mrisho na viungo vyake vyote.

2015 Mi naona ni mbali sana!
 
Madai ya madaktari unalinganisha na posho za madiwani? na wameshaambiwa sawa, tuanze bajeti ijayo. Kwani hao madiwani na wao si zinaanza bajeti hiyohiyo ijayo.

Tuondoleeni ujinga nyie madaktari, kama hamjui maumivu ya mgonjwa yanakuwaje, sasa mtayajuwa.
 
Wiki iliyopita nilienda wadi ya "Sewahaji" bale Muhimbili kumuangalia mgonjwa kwa kweli jamani, tuweke unazi na unafiki pembeni, watu wa kada ya Afya wanafanya kazi katika mazingira magumu mmo, mazingira yale niliyoyaona pale kwa kweli ni hatarishi sana. Kama kweli Serikali ingekuwa "SIKIVU", ingewasikiliza hawa ndugu zetu madaktari. Pia, ukienda kwenye taasisi ya ocean road, kwa kweli kama una moyo mwepesi unaweza ukakimbia ukiwaona wagonjwa wa kansa wa pale au unaweza kutapika au kutokula kabisa, lakini madaktari wamekuwa wakiwahudumia kwa miaka yote, tena kwenye hali duni, kwa kweli sasa inawapasa mazingira yao ya kazi yaboreshwe. Naonga mkono mgomo wa madaktari...
 
Madk komaeni tena sana.Kwa nn ninasema hivyo;

soma hapa,

1.serikali yetu imeweka mbele udkiteta zaidi badala ya kutumia hekima kusuluhisha mambo.

2.Kusema hakuna fedha ni uongo 300 bil zilizopo nje /USWISI ni za akina nani...JE ZINGEKUWEPO NCHINI ZINGETEKELEZA MANGAPI?

3.Viongozi hawana uchungu ,wakiugua wanakwenda nje kutibiwa.HAWAJUI kuwa wtz ni wengi zaidi yao hivyo watoe vipao mbele kwa raia kwanza kupitia dks wetu.HII NI DHAMBI KUBWA INAYOSHAMIRISHWA NA DHANA YA WALIO NACHO NA WASIO NACHO....

4.wafanyakazi wa tz fanyeni kazi zenu kwa kujiamini/muwe na umoja katika kudai haki zenu.
Posho za kuwalipa viongozi wengine kama wakuu wa mikoa waliopo dom for nothing wanazipata wapi?...WATZ /WAPIGA KURA HAWANA UMUHIMU KWA HAWA VIONGOZI?

5.Nchi hii hakuna haki mpaka wabananishwe ,tena wanapoona wanafamilia zao/watoto wao ndo waathirika wakubwa,ndo wanasahtuka na kutoa matamko.mfano nenda vyuo vikuu......

6.Haki huinua taifa ,lakini dhambi ni aibu ya watu wote.....dhambi hii ya watz kufa ni ya viongozi wetu kwani siasa kwao ndo silaha yao bila kujua ukweli na hali halisi.Kwa mtini jifunzeni.

7.Ufisadi upo kila kona na kutowasikliza madks ni UFISADI PIA.

8.Haya ndo madhara ya walalahoi wetu bungeni wanaopitisha kila kitu 100% kwa 100%.......bila kujali wapiga kura wao.

9.Nchi hii imeuza siku nyingi.wenye say sasa hivi ni vigogo na watoto wao,kwani pes ndo kila kitu.

10.UDHAIFU wa viongozi wetu ndo umetufisha hapa.Mikataba bomu,kuna nini vichwani mwenu...mmeIWEKA WAPI miungu yenu wakati mnapofanya maamuzi?....

11.rasilimali tulizo nazo mfano madini yangemaliza tatizo la dks kama viongozi wetu wangekuwa na mfumo mzuri /strategic planning .......badala yake USWISI ndo kila kitu....HATUTAFIKA....

12.WAANDISHI WA HABARI WANGEANDIKA KILA KITU KAMA KILIVYO BILA KUPEWA MLUNGULA TANZANIA HII INGEKUWA KAMA JEHANAMU.....VIJIJINI PANATISHA .........

13.DHAMBI KUBWA INAYOLITAFUNA HILI TAIFA NI UDHALIMU,UZIZI NA UASHERATI,DHULUMA NA TAMAA.VIONGOZI TUBUNI TUKOMBOLEWE.

14.Mfalme sulemani aliomba hekima kuwaongoza waisraeli ...Je hekima za viongozi wetu zipo wapi...? kwa nn kila kitu ni malalamiko?,manung'uniko?


......................nina mengi wino umeisha.Nitarudi........
 

Jamani tungekuwa hatuna Rais DHAIFU si tungechukua zile 303Bilion za Uswis tuwape Madaktari na kuboresha mazingira ya hospital??? Anagalia sasa....Madiwani nao wameonezewa....aaaaagh!!
 
Kwa serikali hii ya ma V8, kugoma ni kama kwenda kazini. Ndio tutaumia, tutakufa, lakini lazima tueshimiane. Hamna maana yoyote ya kutoa mkoloni mwekundu na kuingiza mweusi. Kuna watu humu nchini wanadhani wao wana hati miliki ya hii nchi na kuponda maraha, kubembea na kusafiri, kujipangia mishahara. Halafu kuna wale wa wito. hakuna taaluma isio na wito. Ndio maana mwanasiasa asie na wito ni rahisi sana kuwa fisadi. acheni fujo walipeni madaktari, boresheni mazingira ya kutolea huduma za afya. Madaktari, kaza uzi kwelikweli.
 

Angalieni tu wasije wakawa-ulimboka mmoja mmoja mpaka muishe.
 

Wanakaa wote kwenye kapu moja, haponi mtu!. Wanyonge wanakufa sana kw uzembe wa raia wawili tu hapa tanzania!, natamani sana kutandika mtu viboko! #Nimeisoma hii pia asante!!!!
 

Tumekuelewa naona mmeanza kwa kumgonjesha Dr. Ulimboka ili naye aonje maumivu ya wagonjwa wengine.
 
Tume ya katiba ya Warioba wanalipwa Billion 10 kwa mwaka. Hiyo hela wameweza kuiweka kwenye bajeti. Leo hii hao akina warioba na wengineo ambao walishastaafu lakini wanakula billion 10? hizo hela si zingepelekwa kwenye hospital zetu zikaboresha huduma za afya...aisee mi ninawaunga mkono asilimia 100. Nitakua naenda kanisani kila siku nimuombe Mungu nisije nikaumwa maana itakua soo lakini ninawasupport endeleeni kudai haki zenu mpaka kieleweke...hao usalama wa taifa wanafanya nini huko hospitali? wamekuja kutibu wagonjwa au? they can destroy you physically but they cant destroy your spirit.
 
Mgomo=tukio la kugoma, goma=sita/kaidi kufanya jambo unalopaswa kufanya bila ya kulazimishwa au kushurutishwa.

Madhara/athari za mgomo wa madaktari ni dhahiri kwa taifa letu. Namshauri mh.spika na bunge lote, kusitisha mara moja shughuli zao za kawaida na kujadili hatua za haraka kumaliza mgogoro baina ya madaktari na serikali 'sikivu' ya CCM.
 
Tumekuelewa naona mmeanza kwa kumgonjesha Dr. Ulimboka ili naye aonje maumivu ya wagonjwa wengine.

Jana nilisema humuhumu JF hao dawa yao ni kula kichapo cha vibaka. Wananchi wana hasira ya kupoteza watoto zao mahospitali, wake zao wankwenda kujifunguwa wanaachwa wanahangaika na uchungu, wagonjwa wanakufa kwa kuwa tu madaktari wamegoma. Hao ilikuwa hukumu yao ni firing squad tu.
 


Hii serikali haina mbadala zaidin ya kugoma, mwongozo kautoa katika mada yenyewe kua kulikua na 2wiks za kujadili suala hili. Na baada ya kuona hakuna matumaini ndio mgomo ulipokuja jitokeza. Jiulize kwa nini serikali haikufanyia kazi mapungufu ilihali kulikua na mgomo kabla ya huu unaoendelea?

Kuhusu kusomea kada hii ya udaktari na si nyingine naomba nikujibu swali kwa mfano. Siku zote kila binadamu ana uwezo mkubwa wa kufanya kitu fulani zaidi ya kingine, madaktari ni THE MOST SELF TRUSTING PERSONS IN THIS WORD, kwa kua waliamini kufuata kile kilichoko mioyoni mwao (Udaktari). Fuatilia maisha yao utagundua kua hua wana tabia zinazofanana hasa katika ukuaji wao. Huyu ungemlazimisha kua Engineer leo jengo lingedondoka kwa upepo wa bahari tu.

Hata hivyo mkataba wa madaktari ni baina yao na Serikali na terms ni kuwatibu watanzania. Sisi wananchi tuna mkataba na Serikali sio madaktari hata kidogo. Nadhani watu wa LAW wanaweza chambua. We are not among two parties to the Contract, but Third parties. "Quid pro Quo" kwamba nothing goes for nothing, hapo ndipo swala la CONSIDERATION linapoingia na ndio madai ya madaktari. And this consideration should be equitable to make the CONTRACT viable.

Serikali inataka kutumia mabavu kuwanyamazisha madaktari (Intimidation) kama upande wa pili wa mkataba huu.

NATOA WITO KWA WATANZANIA WENZANGU KUUNGA MKONO MGOMO HUU ILI MADAKTARI WAJALIWE KAMA NCHI NYINGINE. Najua kuna maisha yatapotea ya wapendwa wetu, lakini mapinduzi ya amani kwa kutekeleza madai ya madaktari serikali HAISIKII............
 
Kuna tatizo moja kubwa kwenye hoja zinazojengwa na Ellyjr8. Kuongelea nyongeza ya posho ya madiwani hakusaidii sana katika kujenga hoja ya matatizo ya msingi ya madaktari yaliyosababisha mgomo. Sana sana kunawafanya muonekane kuwa wanasiasa ndani ya majoho ya madaktari. Mimi nashauri mngejielekeza zaidi kwenye hoja za msingi zinazowasababisha kugoma kama mazingira duni na hatarishi kwa afya zenu, ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi, malipo duni etc. Muhimu zaidi ni kujibu hoja za serikali kuwa fani yenu kisheria hairuhusiwi kugoma, wameshafanyia kazi zaidi ya nusu ya madai mliyoyatoa awali na kuwa mengine ama hayatekelezeki mara moja ama yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Vinginevyo mtapata wakati mgumu sana kuushawishi umma wa watanzania wenzenu kuwa mgomo wenu una manufaa kwa taifa hili.
 
"Kama hatuwezi kugawana utajiri wa nchi hii, basi tugawane umasikini" big up doktas.
 

DO NOT TALK ABOUT THE HELL JK he is worthless to us. Ukitazanma ramani ya AFRICA ni wazi Tanzania ndio yenye migodi inayofanya kazi, yenye maziwa mengi na Bandari, achilia mbali mbuga za wanyama na usisahau Mt. Kilimanjaro.....

The HELL says "Hatuwezi kuishi bila msaada" au sisi ndo tungekua Superpower in AFRICA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…