Fresh news: Ukweli kuhusu mgomo wa madaktari - part II | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fresh news: Ukweli kuhusu mgomo wa madaktari - part II

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ellyjr8, Jun 27, 2012.

 1. e

  ellyjr8 Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  FRESH NEWS: UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI -II.


  Leo ningependa turudi jamvini kujadili kidogo kuhusu huu mgomo wetu, awali katika sehemu ya kwanza ya mada hii, nilijaribu kuainisha madai yetu, makubaliano na kuacha kwako mwanya wa kufikiri utendaji wa serikali yetu “SIKIVU” ilivyo na inavyofanya hadi sasa (kama hukubahatika kusoma hebu itafute facebook na Jamii forum ili upitishe macho KIDOGO TU ikiwa na thread title UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI)..leo nilifikiri si vibaya tukijadili kuhusu madhara ya mgomo huu.


  HALI HALISI HOSPITALINI:


  Hospitali ya Taifa Muhimbili, Ocean Road Institute, Temeke, Mwananyamala, Amana, Bugando, Mbeya, KCMC, ST.Francis, Haydom, Dodoma n.k. huku kote hakuna kinachoendelea..madakatari kwa maana ya General practitioner na Specialist, sio Assistant Medical Officer,AMO( KWANI KUNA UTOFAUTI KATI YA NGAZI ZA UDAKTARI KUTOKANA NA KISOMO/ELIMU-nisingependa kwenda katika hili) .. Hii ni TOTAL TOOLS DOWN,(TTD), episode III..

  Kama tulivyosema awali hatudai posho, na ongezeko la mishahara tu(hii si priority hata katika madai), ila eti kulingana na majibu ya serikali, tutegemee madai hayo katika next next fiscal year(2013/2014) lakini hebu jiulize
  1. Madai ya madaktari yalianza lini?

  2. Madiwani waligoma ama kudai mshahara/posho lini??!
  3. Priority ya Taifa ni wananchi(kupitia madai ya madaktari) au viongozi(kupitia posho mpya za madiwani zilizotangazwa Bungeni)?
  4. Nyongeza ya posho ya madiwani imetokea wapi?? ilipangwa katika bajeti?
  5. Viongozi au wananchi hamuoni haya??

  SISEMI TUNAHITAJI MISHAHARA YETU ILINGANE NA WABUNGE, MAWAZIRI, WAFANYAKAZI WA TRA, BOT, n.k..LA HASHA!! ILA UNAPODAI MAZINGIRA BORA YA KAZI, NYONGEZA YA MSHAHARA,POSHO NA UNAPEWA MAJIBU YA DHARAU,.. NA WENGINE KAMA VIONGOZI KUJIONGEZEA(during the same period of our claims), HAPO NDIPO COMPARISON INAPOTOKEA, NA KULAZIMISHA TUFANANE NA NYIE!!
  Katika hospitali tajwa hapo juu, Wakurugenzi, wakuu wa idara wamekuwa wakifanya vikao na kulipwa 50,000/=TSHS@SIKU toka mgomo kuanza 23.06.2012.., Je, wananchi mnayajua haya? Jiulize kuna idara ngapi katika hospitali hizi? Nani anayetoa pesa hizi? Zitatoka hadi lini? Lengo kuu ni kushawishi, kushurutisha madaktari turudi kazini… !!

  VYOMBO VYA HABARI:
  Katika “episode” mbili za “series” yetu hii ya Mgomo wa Madaktari, vyombo vya habari vilianza kuripoti kuwa hakuna migomo, hadi pale watu wa HAKI ZA BINADAMU walipoingilia kati!!

  Nasikititishwa sana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), kutotoa taarifa halisi wakati watu wanazidi kupoteza maisha, kweli hawaoni? Hawajui au wanapuuzia?

  Halafu mnatuita madaktari si wazalendo? KWELI?? Napata shida sana kuelewa inakuwaje watanzania wanaumia na viongozi kutotilia maanani madai yetu, ni kweli uhai wa mtu hauwekwi rehani lakini hatukuingia katika mgomo huu kwa kuweka maisha ya watanzania wenzetu katika mizani, na ndio maana muda wa mazungumzo ulikuwepo na hata kabla ya mgomo, muda wa wiki mbili ulitosha kujipanga, kwamba kama Serikali ikishindwa kutekeleza madai, AU kuonyesha njia mbadala ya kuyatatua basi ijipange kuhudumia wananchi.

  Kama leo hii tunaangalia luninga(TV-mfano Mh. W/Afya pale Star TV kukimbia), tunasikiliza redio lakini mambo yanayofanya na serikali ni haya, umekwisha jiuliza ingekuwaje, ama Serikali yetu ingetutendea nini kama tungekuwa hatuwaoni wanachofanya pale Bungeni(Mfano Takwimu za uongo), na kwingineko? Hali hii itaendelea hadi lini? wewe unayesoma utabadilisha mfumo huu lini?


  MKAKATI:

  Usalama wa taifa wako kila hospitali, swali ni hili
  1. Ni usalama wa Taifa au wa chama tawala?
  2. Wanatumia pesa ya nani?
  3. Last ‘episode” walileta wanajeshi,

  KAMA MADAI YA MADAKTARI SI YA MSINGI NA SERIKALI IKO SAHIHI KWANINI WANAJESHI HAWAJATOA HUDUMA KAMA WALIVYOTOA HAPO MWANZO??

  KWANINI HAWAKUWA TAYARI HATA WALIPOOMBWA KUFANYA KAZI MNAYYOIITA KAZI YA WITO????


  MAKOLIGI (colleague)??
  Ni lini wananchi waliingia mkataba na sisi juu ya afya zao??sasa mbona wanatulalamikia na kutushambulia??..nadhani wananchi mnakosea kidogo, dhamana ya afya zenu ni kwa hiyo serikali “sikivu”, hivyo lawama, maombi, na hisia zote pelekeni huko….ila sisi kurudi ni hadi pale madai yataposikilizwa, this time si kwenda kazini halafu yafanyiwe kazi? HAPANA..HII IELEWEKE VIZURI..HATUDANGANYIKI… hadi yafanyiwe kazi na kuthibitishwa au njia mbadala.
  Najua wanasema when you get in a fight you should dig, two graves but I guess you should not fight with someone who has NOTHING to loose,.. We either overestimated the power of Government’s responsibility or They(Government) underestimated our power, and I really doubt of the latter because they KNOW they cant stop us.. you cant stop what you cant catch, because the more they will push us the worse this is going to get…
  ..Solidarity forever..
   
 2. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Upuuzi ni kugoma.
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono mgomo kwani wanasiasa hawa ni wabinafsi wakubwa yaani posho, marupurupu, seating allowance zipo lakini inapofikia pesa kwa ajili ya waalimu au madaktari serikali pesa hakuna.

  Silaha mliyokuwa nayo ambayo serikalini tukutuku inaweza kusikia ni moja tu nayo ni MGOMO.

  VIVA MGOMO.
   
 4. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Go on Mkuu!! tuko nyuma yenu Hii gov. wasanii sana still wanadhani watz bado tuko kwa 70s 80s that they can fools us kisa wanamiliki kila kitu !! i wish teachers nao wange wa join muwabane upside down:dance:
   
 5. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,632
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Umoja ni nguvu dokta! Wananchi wameamua kujitoa mhanga kwa ajili yenu, msimu huu 'mmeshika mpini na serikari sikivu imeshika makali' Acha usalama wa taifa na mdogo wake green guards wajitose kwenye vita ya kuwinda upepo!
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wewe Radhia Sweety unajifanya kuwapuuzia madaktari madai Yao kwavile mna uwezo wa kutibiwa kwa hela za kifisadi kwa taarifa zimeshaanza kukamatwa heshima itarudi tuu
   
 7. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  madaktari komaeni kwani mkilegeza uzi tu mmekwisha... haya nimatusi tena ya nguoni kusema kuwa hakuna fedha za kununulia vitendea kazi... ooh serikali haina fedha za kuwalipa madaktari ilihali serikali hii hii ya CCM inaendela kutanua uwigo wa matumizi kwa kuongeza mikoa mipya, wilaya zaidi na majimbo zaidi ya uchaguzi...

  Hawa CCM wamefisadi madini, maliasili, ardhi yetu na sasa wanapiga deal la mafuta na gas...watoto wetu wanaendelea kukalia mawe, akinamama wanajifungulia sakafuni kutokana na ukosefu wa vitanda, walimu na watumishi wengi hali zao niduni masikini wakutupwa...wakulima na wafugaji wako hoi bin taaban... NIUKWELI USIOPINGIKA KUWA TEGEMEO LETU LIKO KWA MADAKTARI wengine tutafuata soon... MSHIKAMANO DAIMA mpaka kieleweke.....
   
 8. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,137
  Likes Received: 10,495
  Trophy Points: 280
  Niko nanyi madaktari na watumishi wengine wa afya..
   
 9. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ninapoandika andika hapa sasa ninao friends of mine 10 specialists wamepata kazi Botswana baada ya serikali sikivu lakini imeziba masikio kuwaambia haitawapandisha vyeo coz kwa sasa hawahitajiki watakapo wahitaji ndo watawapandisha vyeo sasa wameamua kuondoka kwenda wanakowahitaji.
  Hawa wamesomeshwa na serikali na kodi za wananchi lakini serikali inasema haiwahitaji. Na sasa serikali imepitisha waraka ambao umesambazwa kwa wakurugenizi nchi nzima kwa lengo la kutowapandisha vyeo watumishi wa kada zote coz serikali imefulia. Sasa shime watanzania tushikamane hatuwezi kuwa ombaomba duniani wakati utajiri tumekalia, serikali inakosa ubunifu wa kuweka vipau mbele vizuri ili tujitegemee. Afu Rais mzima na akili zake anasema hatuwezi kuishi bila misaada kwel!!!!!!!!!! Sasa hii akili au matope? Any way solidarity forever
   
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nilimsikia katibu wetu mwenezi akisema eti huu mgomo unashabihiana na M4C. Nilistuka sana, kwani yale madai yenu si yakuyatafuta huko mahospitalini. Bilashaka aliwachanganya na wale jamaa wa Apolo. Wamewafanya nyinyi ni watu wa kutoa vibali/referral za kwenda India na kwingineko. Ndiyo maana hata yule naibu waziri wa awali alitoa taarifa ya serikali bungeni kuwa episodes I & II hazikuwa na madhara yoyote. Hata sasa hawana wasiwasi, kwani hayatatokea madhara yoyote. Hawa ndiyo walituambia kuwa watatawala milele. Poor me!
   
 11. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Umeandika vizuri sana na kufafanua kwa kina justification ya mgomo unaondelea.
  Ni ukweli usiopingika kuwa katika ufisadi huu unaotangazwa kila siku bado kuna fani adhimu ambayo hawalipwi vizuri na inaelekea kuna watu ambao hawajali maslahi yao.

  Ni wazi kuwa serikali imeshindwa kutoa kipaumbele kwa madai ya madaktari.
  Ninashukuru pia kutufafanulia kuwa mostly walio kwenye mgomo ni madakatari wote ispokuwa AMO (assistant medical officers) na hili linanipa faraja kwani ndo wengi katika hospitali za wilaya na mikoa ambapo idadi kubwa ya watu wanatibiwa.Najaribu kutafuta tafsri sahihi ya neno daktari ili niweze kuchangia kipengere hicho vizuri.

  Hata hivyo kwa mnasaba hu huo wa kuanza kuweka madaraja katika mgomo huu naomba niingie katika mojawapo ya madai yenu ya kuwa mnahitaji mazingira bora zaidi na vitendea kazi.Dai hili lilipaswa kuwakilishwa na hao ambao hawapo kwenye mgomo huu kwani tukiangalia ratio ya MD kwa AMO katika hospitali zinazohudumia watanzania wengi utagundua ya kuwa hao wanaotengwa kwa sasa ndo wengi zaidi na hivyo ndo wanahudumia katika mazingira magumu zaidi.

  Naomba sasa nitoe mtizamo wangu kuhusu suala hili ingawa nimefanya hivyo katika thread nyingine.
  Pamoja na kukubaliana na madai yote napingana na nyie katika hatua ya kugoma.
  Naomba niweke katika mtindo wa maswali,


  1. Je Daktari akigoma na nani anayeathirika zaidi?
  2. Katika kufikia malengo (pursuing for goals) binadamu anakuwa anaongozwa na nguvu au mategemeo fulani,je mlioamua ku pursue for medical field mlikuwa mnaongozwa na mtizamo gani?
  3. Inawezekana hesabu ikawa hivi,tugome,wananchi wafe,wananchi waichukie serikali na kisha serikali ianguke ni ije serikali nyingine.Ni nani ana uhakika kuwa wananch wetu (walio wengi)wataungana na Madaktari kuiangusha serikali?
  4. Tumeshuhudia zyama venye sera nzuri vikikosa uongozi kwa kuwa walio wengi hawakuvipigia kura.

  Naungana nanyi katika madai yenu lakini SI KATIKA MGOMO, kuacha watu wafe kwa mtu aliyesomea fani ya kuokoa maisha ni jambo ambalo mwisho wa siku halitamtofautisha na Al qaida anayelipua soko ili kumuua Mmarekani mmoja.
  Serikali imetetemeka basi rudini katika mazungumzo na rudini kazini,TUTAWAONA ni waungwa zaidi.
   
 12. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  kuna taarifa kuwa dk ulimboka ametekwa usiku wa leo saa sita ni kweli?
   
 13. v

  vngenge JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Walikuwa wapi wakati watu wanaficha mabilioni uswisi?, Kamati ya bunge ya mambo ya nje inaenda kuzurura nje na kuacha bunge la bajeti. Are they serious kweli? Kila kona ufisadi tutafika kweli. Huwezi kutumia nguvu kuzima malalamiko ya wengi. mutual consensus is the only soln
   
 14. L

  Leodgard Member

  #14
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kugoma sio upuuzi bali njia zinazotumika kuendessha mgomo ni hatari kwa Watanzania wasiokuwa na hatia!!!
   
 15. humphg

  humphg Member

  #15
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  :whoo:Mimi nafikiri mgomo ni njia sahihi kwa madoctor na hata sector nyingine kama walimu, wanasheria nk. kwa sababu serikali ilipewa grace period ndefu sana kutatua matatizo hayo, lakini haikuitumia vema badala yake wamefanya usanii kutuliza hali kwa muda na kuahidi mabadiliko kwenye maslahi ya wafanyakazi bila kutendea kazi ahadi zake! Hivyo ni bora mtu adai chake mapema kabla awamu nyingine kuingia na kupewa longo2 zaidi!!
   
 16. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Kijana tatizo lako ni kubwa sana, wait until you are taken out of the water like a fish!!
   
 17. humphg

  humphg Member

  #17
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo mengine yanaonekanatu bila hata ya kumulika kwa touch!! kama uliahi kitufulani basi tekelezaaa!!!!! :smow:
   
 18. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  hata mie naunga mkono sana huu mgomo...madaktari wana haki ya kugoma kwani siasa zimeingizwa hata kwenye mambo ya msingi ya hili taifandio maana utaona hata vyombo vya habari hasa vya taifa vinapindisha ukweli wa mambo..madai ya madaktari hajaanza leo..toka enzi zile suaye ni waziri mkuu nakumbuka mgoomo ulikuwepo sasa kwa nini kuwatupia lawama madokta??
   
 19. n

  nkansee Member

  #19
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i support you 100%
   
 20. N

  Nambombe Senior Member

  #20
  Jun 27, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la kada ya afya ni ubinafsi,kila sekta ina chama chake.Maabara,famasia,nesi,x ray... kila watu na chama chake.Madaktari wao wanajiona bora kuliko kada zingine za afya jambo ambalo si kweli kwani kada zote za afya zinategemeana.Wakigoma manesi au maabara au watu wa usingizi je daktari ataweza kufanya kazi.Wewe ndg ellyjr8 wacha
  kupotosha umma,hayo yote yanatokea ni kwa sababu mmekosa umoja kwenye sekta ya afya sababu ya ulafi wenu.
   
Loading...