Frequency 50 hertz inamaana gani?

Electromagnetism

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
482
Reaction score
127
Napata ugumu kuelewa hii concept nini maana ya 50hertz yani 50 cycles per second yani ni mzunguko wa turbine mara 50 per second au ni nini?
 
Umeiona wapi hiyo? Ina applications nyingi mno.
 
Napata ugumu kuelewa hii concept nini maana ya 50hertz yani 50 cycles per second yani ni mzunguko wa turbine mara 50 per second au ni nini?

Inategemea unaongelea frequency ya kitu gani, kama ni turbine mfano wind turbine basi 50hz maana yake ile turbine inazunguka mara 50 kwa sekunde moja...

Kama ni ya camera maana yake inapiga picha 50 haraka haraka kwa sekunde moja (kwenye camera kwa lugha nyingine wanaita fps(frames per second))....

Kama ni kwenye monitor ya computer maana yake inadisplay picha 50 kwa sekunde moja...

Kama unaongelea electricity basi 50Hertz ni oscillations 50 za current kwa sekunde moja.... na mengine meeeeengi!! frequency ipo kwenye kila object hata mwili wako. For as long as kitu kina energy basi kina frequency flani pia.
 
asante mkuu
 

I can imagine a turbine revolving/moving in a cycle on its own axis 50 times per second-quite imaginary ndio maana inamchanganya
 
kwenye umeme mkuu

Kama ni kwenye umeme maana, aina hiyo ya umeme inaitwa "Umeme mkondo geu" ama Alternating current, A.C kwa kiingereza. Basicaly katika umeme kuna nyaya mbili kuu, positive ambao huwa mwekundu/brown na negative ambao huwa mweusi/mweupe.

positive terminal ya AC electric system hubadilika polarity with respect to neutral wire kadri muda unavyokwenda. Kwa kuwa mkondo wa umeme wa A.C hubadilikabadilika polarity kadri muda unavyokwenda, hivyo kunakuwa na maximum na minimum polarity magnitude/size ya umeme huo. Hivyo basi kitendo cha mkondo wa umeme kukamilisha mzunguko mmoja wa kutoka zero magnitude, kwenda maximum, kurudi zero kwenda tena minimum na kurudi tena zero ndani ya sekunde moja kitaalamu huwa denoted as 1 Hz.

So kwa 50 Hz ni kuwa kitendo nilichokielezea hapo juu kinajirudia mara 50 ndani ya sekunde moja. Na mostly umeme unaotumika majumbani unakuwa sinusoidal in shape kama hizo parameters (voltage & current ) zikiwa plotted kadri muda unavyokwenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…