MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,051
Mwanzoni mwa mwaka huu tulishuhudia Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe akizunguka sehemu mbali mbali nchini kuzindua vikosi vya vijana wanaoitwa Red Brigade kwa ajili ya kuwaandaa kukilinda chama na kuzuia wizi wa kura kwenye Uchaguzi Mkuu.
Mbowe alienda mbali zaidi na kudai CHADEMA imejipanga katika Uchaguzi Mkuu na hakutakuwa na wizi wa kura hata moja.
Kwa sasa Mbowe anamwaminisha Lowassa kwa kumwambia ameibiwa kura wakati anafahamu hakuna kura iliyoibiwa kwa sababu vijana wake wa Red Brigade aliowapa mafunzo ya ulinzi walizilinda kwa umakini kura za CHADEMA/UKAWA.
Mbowe anatakiwa amweleze ukweli Lowassa hasa ikichukuliwa Lowassa alikuwa hafahamu mikakati ya CHADEMA katika kuzilinda kura ambazo pia zimemwezesha Mbowe kurudi tena bungeni.
Kama anachokisema Mbowe siyo ulaghai kwa Lowassa, basi inabidi awaambie pia wabunge wote wa CHADEMA/UKAWA wayakatae matokeo yote ya uchaguzi, hii ni pamoja na matokeo ya udiwani na ubunge. Wasiingie bungeni tena ili wawaache wabunge wa CCM waisimamie serikali yao ya Rais Magufuli iliyopatikana kwa wizi wa kura za Lowassa!
Kuingia bungeni na kuanza kuisimamia serikali ya Rais ambaye amepatikana kwa wizi wa kura ni kumlaghai na kumuhujumu Lowassa.
Gazeti la Nipashe la 10th February 2015 lilimnukuu Mbowe akisema,

Hizi ni baadhi ya thread nyingi zilitueleza mikakati ya Mbowe na CHADEMA katika kuzilinda kura za Uchaguzi Mkuu,Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kimejipanga kuhakikisha katika uchaguzi Mkuu hawaibiwi kura.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freemon Mbowe wakati akizindua mafunzo ya Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha chama hicho (Red Brigade), kwa vijana 200 wa Kanda ya Kati pamoja na Kikosi maalum cha Karate.
?Katika uchaguzi huu hatutaki kulalamika tena kwamba tumeibiwa kura na tutahakikisha tutaomba kura kwa wananchi na tutazilinda,? alisema Mbowe.
Alisema endapo watakubali kuibiwa kura maana yake hawapo tayari kuongoza.
Mbowe aliwataka vijana hao wa Brigade kutokukilinda chama peke yake bali pia kiwe chachu ya ulinzi kwa jamii inayowazunguka kwenye maeneo yao. Alibainisha kuwa Chadema kitaendelea kutoa mafunzo ya ulinzi kwa vijana nchi nzima.
"Vijana hawa lazima wajenge moyo wa kujitolea, chama kilijengwa na watu wenye moyo huo ambao baadhi walipata madhara mbalimbali ikiwamo kupoteza maisha,? alisema Mbowe.
Alisema wajenge sifa ya kuwa wakombozi wa Taifa na malipo mengine siyo lazima walipwe hapa duniani bali watapata kwa Mungu.