Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,934
Siku zote msamaha anaombwa aliyekosewa.
Kwa kila mwenye akili, mkweli wa nafsi, anayemtumikia Mungu wa kweli, na mwenye Roho wa Mungu, hawezi kusita wala kuwa na kigugumizi kutamka kuwa Mh. Mbowe amekosewa mara nyingi, si mara moja wala mara mbili.
Kama itakuja kutokea siku moja Taifa letu likabahatika kupata uongozi wenye hekima, uongozi unaojua maana ya umoja, upendo, utu, haki, na unaojua umuhimu wa tunu hizi katika kuleta maendeleo ya kweli, Mh. Mbowe ni mtu ambaye atatakiwa kuwa wa kwanza kuombwa msamaha kuliko mtu yeyote, kwa uovu mwingi aliotendewa wakati mbalimbali:
1. Mbowe, mashamba yake yaliwahi kuteketezwa kwa uonevu.
2. Mbowe, club yake ya Bilcanas iliwahi kunyang'anywa kwa uonevu.
3. Mbowe amewahi kuwekwa mahabusu mara nyingi kwa uonevu.
4. Mbowe amewahi kuhukumiwa kulipa mamilioni ya pesa kwa uonevu.
5. Mbowe amewahi kubambikiziwa kesi zisizo na vichwa mala miguu kwa nia tu ya kumkomoa.
6. Mbowe akaunti zake za benki ziliwahi kufungiwa kwa uonevu.
7. Mbowe, hoteli yake ya familia imewahi kubambikiziwa kodi zinazozidi mapato maradufu.
Mbowe, mpaka leo bado anaonewa, na yumkini ataendelea kuonewa, lakini bado kitambo kidogo, ushindi wa haki utapatikana. Siyo ushindi wa Mbowe, bali ni ushindi wa haki dhidi ya uovu.
Makaburu kule Afrika Kusini waliowaonea sana wapigania haki wazalendo, wakiongozwa na kiongozi shupavu, mzalendo wa kweli wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela. Utawala wa makaburu, chini ya Fredrick De Clerk, ulipoijiwa na hekima, ulitaka maridhiano na Waafrika weusi waliokuwa wakibaguliwa. Jambo la kwanza, walimwachia Nelson Mandela na wapigania haki wote. Ukafanyika uchaguzi huru, huru hasa siyo kama hivi viinimacho vyetu vya Tanzania.
Mandela aliposhinda kwenye uchaguzi huru, alitaka Afrika Kusini yenye umoja na upendo, naye akanena, 'kama ubaguzi wa mzungu dhidi ya mtu mweusi haukuwa mzuri, basi vivyo hivyo, ubaguzi wa mtu mweusi dhidi ya mzungu, hautakuwa mzuri. Mandela hakutaka roho ya kisasi miongoni mwa wananchi wa Afrika Kusini. Aliamua kuunda tume ya maridhiano. Kisha wahalifu na waliofanyiwa uhalifu walitakiwa kwenda mbele ya Tume. Walikutanishwa. Wahalifu walieleza uovu wao wote, kisha waliofanyiwa uhalifu waliombwa msamaha, nao baada ya kutoa msamaha, wahalifu walikabidhiwa vyeti vya kusamehewa ambapo walihakikishiwa kuwa kamwe wasingeshtakiwa kwa makosa waliyoyatenda ambayo wameyakiri mbele ya Tume. Kama umeficha uhalifu, na baadaye ukapatikana ushahidi wa uhalifu wako, ujue utashitakiwa na kuhukumiwa.
Rais Samia anasema tusahau yaliyopita, tuanze upya. Je, anafahamu kanuni za maridhiano? Unaweza ukafanya maridhiano na mtoto, huku baba yake au kaka yake, umemfunga pingu kwa kumwonea?