Kwanza napenda kutangaza political interest yangu kwamba mimi ni mfuasi wa kawaida wa CCM sina hata kadi ila nimetokea kukipenda chama hicho na niliwapigia kura wagombea wote kuanzia udiwani, ubunge hadi urais kupitia CCM.
Imefika wakati lazima niseme ukweli sasa ninaouamini mimi mwenyewe, Freeman Mbowe umejitahidi sana kuijenga CHADEMA kwa hali na mali, umekuwa mtu usiyependa kujikweza, umekuwa mvumilivu sana lakini kikubwa zaidi umekuwa mkali pale unapoona kiongozi yeyote anataka kuihujumu CHADEMA.
Umeonekana mpinzani wa kweli na huongeki na maasimu wako ili ukiuwe chama. Big up brother umefanya mengi kukijenga chama sasa kimekuwa maradufu kila uchaguzi mkuu ukifanyika mnaongeza idadi ya madiwani, wabunge na mnaongeza idadi ya kura ya mgombea wa urais kupitia chama chenu huku ndio kukua kwa chama kukua kwa CHADEMA.
Kimsingi kukua kwa CHADEMA au chama chochote cha upinzani kutaifanya serikali iliyoko madarakani kutimiza ahadi zake na hii italeta tija kwa wananchi wote bila kujali itikadi, kama maji tutapata wote, kama elimu tutapata wote, kama afya tutapata wote n.k.
Freeman Mbowe unastahili pongezi kama tunavyompa pongezi Rais Dr Magufuli kwa kuanza kuyatumbua majipu. Wote wanaokukejeli, kukutupia vijembe, kukutukana, kukuteng'enezea majungu wewe mwenyewe au CHADEMA ni wafuasi na wapenzi wa CCM.
Wana CCM nikiwemo mimi hatupendi kuona ukipanga na kutekeleza mikakati ya kukijenga CHADEMA kama ilivyo kwa wana CHADEMA hawapendi kwa CCM.
Mbinu nyingi zimetumika na wafuasi wa CCM kukuchafua lakini hukati tamaa matokeo yake CHADEMA inakubalika maeneo mengi tofauti na miaka ya nyuma.
Hii inaonyesha kuwa wananchi wamepuuza propaganga za kipuuzi dhidi yako na chama chako,wamesema sana CHADEMA ni chama cha Kikanda lakini tumeona mmechukua majimbo ya Dar, Serengeti, Mkoani Morogoro mmechukua Mikumi, Ifakara na Mlimba.
Wafuasi wa CCM wanaakili sana wanajua adui wao mkubwa ni wewe, ukiyumba tu na chama kinakufa nasema "HAKI YA MUNGU"Ndio maana kilakukicha ni Mbowe tu mara kafanya hivi mara kafanya vile, ukitaka kumuua kirahisi KIFARU mpige risasi ya kichwa usimpige mguuni atachelewa kufa au atakimbia sasa tunaona CCM ikitafuta kichwa cha Kifaru sijui itafanikiwa au la! CCM ukiwa tishio kwao utakula makombora ya propaganda za kisiasa lakini ukiwa sitishio"INACTIVE"watakupenda na kukusifu kwa mapambio.
Siku zote wana CCM huvisifu vyama vya upinzani ambavyo ni vichanga au dhaifu,huwasifu pia na viongozi wao kuwa hawa ni wapinzani wa kweli.
Freeman Mbowe wewe ni "oppositional politician model"Unajua vema kuwapanga watu kwa kuzingatia nafasi zao na kuzingatia kukubarika kwa watu, siasa ni watu, kama huna mvuto kwa watu huwezi kufanya siasa ni kupoteza muda tu, siasa sio uproffesor, udokta, idadi nyingi za degree au usomi mkubwa la hasha!
Ukitaka kuwa mwalimu lazima usome ili upate kazi,ukitaka kuwa dakitari hospitalini ni vyeti tu sio kupendwa na watu. Freeman Mbowe usivunjike moyo zege hailali mapambano yaendelee, panga safu yako ya uongozi iliyoimara ili upinzani ukue zaidi na zaidi na hatimaye mshike nchi na ninyi CCM iwakosoe kwa utendaji kazi wenu.
Upinzani imara utaifanya serikali iliyoko madarakani kutimiza ahadi zake kwa kiasi kikubwa,Upinzani dhaifu utaifanya serikali iliyoko madarakani kuzembea.
Mimi kama mwananchi wa kawaida napenda kuona upinzani ukikuwa kwani sina cheo chochote CCM,sina nafasi kubwa serikalini,maisha yangu ni yakawaida tu na wale majirani zangu ambao wana itikadi tofauti.
Kiujumla sina cha kupoteza.Nawaombea pia vyama vingine vya upinzani vijiimarishe na vijijenge visipende kuunda urafiki na CCM huo ni urafiki wa mashaka.
MAY GOD BLESS OPPOSITIONAL POLITICAL PARTIES IN TANZANIA