Freeman Mbowe amekomaa sana Kisiasa

Freeman Mbowe amekomaa sana Kisiasa

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,486
Reaction score
9,594
Kuna wanasiasa wengi wenye busara na weledi waliopata kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu lakini kwa kizazi chetu hiki nadhani ndugu Freeman Mbowe ni mfano halisi wa ukomavu wa kisiasa, huyu anapaswa awe Mwalimu wa siasa kwa wanasiasa chipukizi hotuba zake hususani hii ya leo ni moja ya hotuba nzuri kabisa za kisiasa , bila hata ya kushika nyadhifa yoyote ile Serikalini bado ndugu Mbowe anasimama kama nembo muhimu ya siasa za Tanzania.

Ningefurahi kama upinzani ungekuwa na watu hata kumi wa aina yake hakika serikali ya CCM ingepulizwa na pumzi ya moto. Ila kwa sasa acha kina mzee Makamba waendelee kulamba asali huenda siku yetu iko karibu.
 
Jela panafunza,unapata muda wa kutosha kufikiri,sijasikiliza hotuba,Ila Kama ni kweli Basi Jambo zuri
 
kuna wanasiasa wengi wenye busara na weledi waliopata kuwah kutokea katika historia ya nchi yetu lakini kwa kizazi chetu hiki nadhani ndugu freeman mbowe ni mfano halisi wa ukomavu wa kisiasa ,huyu anapaswa awe mwalimu wa siasa kwa wanasiasa chipukizi hotuba zake hususani hii ya leo ni moja ya hotuba nzuri kabisa za kisiasa , bila hata ya kushika nyadhifa yoyote ile serikalini bado ndugu mbowe anasimama kama nembo muhimu ya siasa za Tanzania .ningefurahi kama upinzani ungekuwa na watu hata kumi wa aina yake hakika serikali ya ccm ingepulizwa na pumzi ya moto.Ila kwa sasa hacha kina mzee makamba waendelee kulamba asali huenda siku yetu iko karibu.
Sio wanasiasa sema wasomi wangekiwasha pia kumpa nguvu mbowe
 
Back
Top Bottom