Free seminar - jinsi ya kupata mchumba

Free seminar - jinsi ya kupata mchumba

Nduka Original

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
1,012
Reaction score
817
Nimeona niweke special thread jinsi ya kuwasaidia vijana namna ya kupata wachumba, Nimeshuhudia vijana wengi sana wakiteseka katika harakati za kutafuta mwenzi wa maisha. Siku zote nimekuwa mshauri kwa wale ambao niko karibu nao na huwa moja kwa moja nawashauri kama ifuatavyo.

1. Kuchague mtu awe mwenza wako wa maisha si jambo la maigizo ivyo unatakiwa ufanye uamuzi sahihi na kwa muda muafaka. Hivyo basi unatakiwa uzingatie yafuatayo.

A. Fanya uamuzi sahihi toka moyoni mwako, kwamba huyu anafaa kuja kuwa mume/mke wangu na isije ikawa kuna msukumo fulani umekufanya ufanye hayo maamuzi. Wewe una nafasi kubwa sana ya kuchagua mchumba wako kuliko mtu mwingine yeyote kama tu utakuwa utakuwa umefanya maamuzi sahihi. Shida vijana wengi anataka kuchagua mchumba kwa predict public response pale watakapokuwa wanandoa. Ndio maana utaona kijana anatafuta mchumba ndio anakuja na cinditions i) awe na kazi/kipato, ii) awe na shahada, iii) awe na gari, vi) awe na nyumba etc. Kumbuka vitu vyote hivyo vinatafutwa. Binafsi wakati namuoa mke wangu nilikuwa sina nyumba wala kiwanja, gari wala degree tena hata kazi nilikuwa sina. Mchumba wangu mwenyewe alikuwa na chumba cha matope. Ila kwa sasa tunamiliki vyote hivyo na pia tumejiendeleza kielimu kwa kiwango cha shahada. Kikubwa cha kuangalia je huyu mtu ni focused??? determined? wise? committed, agressive and not those degree things and all those bizarre stories. Honestly hili ni tatizo kubwa sana na ndio maana ndoa nyingi sana za sasa hivi hazikai kwa muda mrefu. Unakuta kijana kaona mdada ana Prado, Ghorofa sijui manager wa bank basi anarukia anaowa. Sisemi wao wasiolewe ila je umefanya research ya kutosha?

Suggestions
1. Fanya maamuzi sahihi
2. Mhusishe Mungu kwa maombi na sala
3. Wahusishe waliokuzidi umri - wazazi, ndugu au jamaa

Asanteni na anaetaka ushauri zaidi anaweza aka ni PM
 
Wewe unavyolalamika mara kwa mara kuhusu wanawake(mke wako) ulizingatia hayo uliyoandika?
 
Back
Top Bottom