"Free Esther" wanajitukanisha wenyewe

"Free Esther" wanajitukanisha wenyewe

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,072
Hawa walioandaa hili tamasha la "Free Esther" wanaishiwa ubunifu kwa kasi ya moto wa nyikani.

It doesn't make sense wao kutumia slogans kama "Uhuru wa Burudani" at the same time wameipiga ban Music label inayofanya vizuri zaidi Tanzania na nje ya Tanzania.

Huo uhuru wa burudani wanaouzungumzia ni upi kama wameshindwa kabisa kuheshimu competition?

Wanajitamba kuwa na "A" list artists ila cha kushangaza zaidi ambaye wanasema ndiye msanii mkubwa zaidi Tz walikuwa hawachezi nyimbo zake kwenye vituo vyao kwa miaka mitatu mpaka pale alipohama kwenye Music label ambayo hawaipendi ndio wanaanza kumpa sifa zake.

Kingine ni promo wanazozifanya, ukifuatilia hili tamasha ni sawa na wamefanya bure tuu kutokana na tickets za Free Esther kuwa nje nje na yote hayo wanayafanya kuonekana bado wanaweza kushawishi hadhira ya Muziki lakini mwisho wa siku jibu linabaki kuwa moja ambalo ni kwamba wamepungikiwa ushawishi mno maana kama mtu anauza tickets kwa Tsh elfu 10 hadi laki 2.5 we uuze zako buku 3 na karibia zote ugawe bure kwa promo za hapa na pale nani kati yenu mwenye ushawishi!?

"Free esther " imekufa vibaya mno, wale wa kwenda kupigwa roba mbao Tmk mjiandae mapema maana kwa hizi tickets za bure wazee wa kazi lazima wajae mule.
 
Back
Top Bottom