Nihzrath
Member
- Jan 15, 2013
- 51
- 116
NA
Nihzrath Ntani Jnr
Mwili wa Fredrick Richard mwenye umri kati ya miaka 25-33 ukiwa tayari umegandamizwa na mchanga katika shimo la futi sita kwenda ardhini. Ni katika ardhi inayomeza wapendwa wetu. Kifo hakina huruma.
Fredrick Richard hakuwa maarufu kabla ya kifo chake.Baadhi yetu hatukuwa tukimfahamu Fredrick Richard. Nini kilipelekea Fredrick kuwa maarufu? Bila shaka aina ya kifo chake ndicho kilichoshangaza wengi na ghafla akajikuta kuwa maarufu lakini akiwa tayari maiti.
Ndoto za Fredrick Richard zikafikia hitimisho ndani ya dunia hii iliyojaa machungu na furaha.
Mapenzi yalikatisha uhai wa Fredrick. Ndoto ya wazazi wa Fredrick kufaidi matunda ya elimu waliompatia mtoto wao ikayeyuka mithili ya nailoni kwenye moto.
Uamuzi wa kujinyonga kwa Fredrick baada ya kusalitiwa na mwanamke aliyempenda sana na mwanamke huyo kutaka kuolewa na rafiki yake aliyemuamini sana.Inaumiza sana.
Ndio mapenzi yanaumiza sana. Lakini inahitajika akili, nguvu za ziada kuyakabili. Bahati mbaya Fredrick hakufahamu kuwa mapenzi ni sanaa. Unahitajika kuwa muigizaji mzuri kuyaongoza mapenzi.
Mpaka sasa sitaki kumlaumu Fredrick na uamuzi wake. Ameshakwenda na hawezi kurudi tena.Mola atampa anachostahili.Kifo cha Fredrick kinaweza kutufundisha mengi tuliobakia hai. Ni kweli mapenzi yanaumiza lakini tunaweza kuyakabili.
SHUJAA NI THOMAS STRUNZ KATIKA MAPENZI..SIKILIZA STORI HII?
Mnamo mwaka 1990. Stefan Effenberg aliwasili katika viunga vya uwanja wa SABENER STRABE.Ni uwanja wa mazoezi wa timu ya Bayern Munich akiwa kijana mdogo. Ni mahala hapo ndipo alipokutana na mvulana mwingine aliyeitwa Thomas Strunz. Wote wawili walikuwa wachezaji wa Bayern Munich.
Stefano Effenberg akitokea Borrusia M' gladbach huku Thomas Strunz akiwa hapo tangu 1989 akitokea MSV Dulsburg. Ni katika viwanja vya Sabener Strabe. Urafiki wa wanaume hawa wawili ulipozaliwa.Wote wawili wakicheza nafasi ya kiungo klabuni hapo.
Miaka miwili baadae marafiki hawa walitengana. Stefano alirejea Borrusia M'gladbach huku Thomas akienda VFB Stuttgart. Miaka mitatu baadae Thomas alirejea tena Bayern Munich akiwa tayari ameoa.Mwanamke mrembo aliyeitwa Claudia Strunz.
Miaka saba baadae tangu alivyoondoka Bayern. Stefano alirejea kunako klabu ya Bayern Munich akiwa naye ameoa mwanamke aliyeitwa Martina. Urafiki wa Stefano na Thomas ukashamiri tena.
Mwaka huo huo siku moja katika majira ya kiang'azi. Yaani mnamo mwaka 1998. Familia za marafiki hawa wawili zilijumuika katika ukumbi wa starehe wa P1 Club uliopo katika mji wa Munich.
Thomas Strunz akiwa na mkewe wa ndoa na mama watoto wake wawili Claudia Strunz huku Stefano Effenberg akiwa na mkewe wa ndoa na mama watoto wake watatu Martina Effenberg walikutana kwa mara ya kwanza.
Ni mahala hapo kwa mara ya kwanza macho makali ya Stefano Effenberg yalipotua machoni mwa Claudia ambaye ni mke wa Thomas. Moja kwa moja hisia za kimapenzi zikaibuka kati kati yao.
Si Stefano wala Claudia aliyeweza kuvumilia.Kila mmoja alimuona mwenza wake wa ndoa kuwa sio chaguo sahihi. Mapenzi yana nguvu sana.Baada ya tukio hilo hayakuwepo mapenzi ya dhati tena kwa wenza wao.Kiapo cha kanisani kikawekwa kapuni.
Wakaanza kusaliti na miaka miwili baadae Stefano Effenberg alimtaliki mkewe Martina kwa uchungu mwingi. Ni wakati huo huo Claudia Strunz naye akiomba talaka kwa mumewe Thomas Strunz. Ndoa zikavunjika.
Mnamo mwaka 2004. Stefano Effenberg na Claudia walifunga ndoa kwa furaha kubwa.Mpaka hivi leo wanaishi kwenye ndoa yenye furaha sana wakiwa katika jimbo la FLORIDA nchini Marekani.
Miezi michache baadae Thomas Strunz alihojiwa na jarida moja la ujerumani kuhusiana na kunyanganywa mke na rafiki yake ambaye alikuwa mchezaji mwenzake.
Strunz alieleza kuwa;
" Ulikuwa wakati mgumu kwa upande wangu kukubali hali hii.Nilikuwa na vitu vingi kichwani, hata hivyo niligundua kila kitu kilichotokea kilikuwa na sababu. Pengine Claudia aliumbwa kwa ajili ya Stefano na kuwa nami ilikuwa kama njia ya kutimiza maandiko"
Bila shaka ilikuwa ngumu kukabili na miezi miwili au mitatu sikuweza kuamini.Niliumia sana lakini nilitumia muda mwingi kusoma vitabu.Ni vitabu pekee vilinipa faraja na kuchukulia kama jambo la kawaida."
Tukio hili lilinipa changamoto kubwa katika maisha yangu. Kwa sasa sina tatizo na Stefano, pia sina tatizo na Claudia.Siku zote napenda kuwaona wakiwa na furaha" alimaliza
Stefano Effenberg na Thomas Strunz walikuwa katika kikosi cha Bayern Munich kilichokuwa kinatisha enzi hizo wakiwemo Mehmet Scholl, Oliver Kahn, Lothar Matthaus, Mario Basler n.k.
Maskini Fredrick hakutambua kile alichokitambua Thomas.Kuwa kila jambo hutokea kwa sababu. Kifo cha Fredrick kinaacha funzo katikati yetu. Makala haya yanaweza kubadili mtazamo wako.
Inawezekana huyo mkeo hakuumbwa kwa ajili yako.Uko nayer kwa kuwa ni lazima apitie kwako ili kumfikia aliyeumbwa kwa ajili yake. Hapa anaweza kuwa rafiki yako kuwa ndiye mume wa mwanamke unayemuita mke wako.ASANTE...