Bumpkin Billionare
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 1,332
- 621
Hivi huyo cheka nae mbna hapganagi na watu wa nje.. Yeye daily anaishia kuwaonea vijana wa keko
au hata angeenda olympic basi!!!Hivi huyo cheka nae mbna hapganagi na watu wa nje.. Yeye daily anaishia kuwaonea vijana wa keko
mkuu una maanisha anaweza kuwa anatumia mambo ya wahenga kushinda mapambano!!!huenda eeee!!Ashapigana mapambano kadhaa huko nje na yote kapigwa....huyu jamaa sio bondia aisee...jaribu kuangalia mapambano yake utakubaliana na mimi.....kamkimbia rasta kaseba wakamfuata huyu muuza karanga ili kumuongezea point cheka...boxing tanzania iliishia na akina matumla basi......
Huyu Cheka ana kama miaka kumi hivi mfululizo sijasikia amepigwa!
Kama Tanzania ingekuwa inajali kila mchezo, bila shaka huyu Cheka angeipa sifa nchi yetu!
Haya ndio ya kuongea mkuu! Lkn kudhani cheka anaweza kwenda mwenye tu njea ya nchi na kuanza kupigana, ni wazimu!
Haya ndio ya kuongea mkuu! Lkn kudhani cheka anaweza kwenda mwenye tu njea ya nchi na kuanza kupigana, ni wazimu!
Tatizo hakuna anayekubali kufanya kwa maslahi ya Taifa, kila mtu anachunguliwa maslahi binafsi kwa kila jambo! Hawataki kumuunga mkono Cheka kwa sababu hawaoni namna ya kumnyonya, kwa hiyo wanamuacha tu amalize kipaji chake hapa hapa hadi atakapozeeka na kufa maskini.
Kaka ndondi sio kucheza marede....cheka sio bondia ...period...yeye na mchumia tumbo wote wabeba viazi sokoni....ndondi tanzania inabakwa na viongozi wa vyama vya ndondi ....wanafanya kama miradi yao....ukiona mtu anapigana kibongobongo jua kuwa kakosa kazi nyingine ya kufanya....vijana wadogo hawaandaliwi kama matumla alivyoandaliwa na baba yake toka utotoni ndio maana mpaka kesho ndio bondia pekee aliyekuwa na ubavu wa kucheza mapambano makubwa nje na kurudi na mikanda...cheka hata umri ushamtupa nje....miaka 30 ni umri wa kustaafu
Kwa bahati nzuri nilipata bahati ya kushuhudia mapambano yote waliyowakutanisha Cheka na Matumla, kiasi kwamba unanipa wasiwasi ndugu yangu kwa unavyosema kuwa Cheka sio Bondia, ila Matumla ndio Bondia.
Cheka ni mmoja wa Mabondia wachache nchini wanaopigana kwa kutumia akili sana wawapo ulingoni, na kubwa zaidi ana ngumi kali, na hili suala la Cheka ngumi kali hata Matumla amekiri mara nyingi ninapozungumza naye.
Labda tatizo lililopo ni kuwezeshwa tu kwa Cheka (au mchezo mzima wa ngumi nchini), ukiwa ni uwezeshaji ambao ungemfanya Cheka azidi kuwa bondia mkali na kuipa sifa Tanzania katika medani ya michezo.
Niweke wazi kwamba, sikuwahi kufurahia mapambano ya ngumi nchini kama nilivyofurahia mapambano yaliyowakutanisha Cheka na Matumla, hasa lile lililopigwa pale Luxury Pub, Tandika!
Omba Mungu, Matumla awe fiti tena halafu liwepo pambano lake na Cheka, nitataka sana mimi na wewe tukae kwenye viti vilivyo jirani tukishuhudia pambano, ukumbi huwa kimya wakati fulani na sauti pekee inayosikika huwa ni ngumi tu.
Hivi huyo cheka nae mbna hapganagi na watu wa nje.. Yeye daily anaishia kuwaonea vijana wa keko
Aende mara ngapi mkubwa.....jamaa hajawahi kushinda pambano la nje hata moja na kishapigana mara kibao tu....hii hapa rekodi yake
mkubwa sasa mbona unachekesha....cheka alipigwa na matumla enzi hizo matumla wa ukweli kabla hajazeeka na kuchoka....cheki rekodi ya cheka utaona pambano lake la kwanza kupigwa....matumla sasa hivi kachoka vibaya sana hata wewe unaweza kumpiga....ni kama tyson alivyochoka sasa ......mimi nataka cheka akapigane nje sio kuchagua wauza karanga kujiongezea pointi.......nitamkubali akishinda angalau mapambano matatu tu ya nje na sijui itakuwa lini maana jamaa na yeye umri ushamtupa mkono....
Wabongo bwana wakitaka kumdisco mtu. Ok then, kama unamuona nyanya basi maana yake Tanzania imekwisha kwani yeye ndio top.