Frame ya duka natafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Frame ya duka natafuta

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Steven Sambali, Jun 29, 2011.

 1. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Wakuu,

  Natafuta Frame ya duka maeneo ambayo yanafikika kiurahisi. Isiwe kubwa sana na wala ndogo sana.

  Ningelipendelea maeneo kama Kinondoni, Mwenye, Sinza, Ilala na Ubungo.

  Lengo hasa ni kuuza vipodozi (Perfumes) kwa bei ya rejareja na jumla.

  Naomba tuwasiliane kwa email SSAMBALI@hotmail.com au nipe PM.
   
 2. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kimya kabisa? Ntaendelea kukumbusha na msinichoke.
   
 3. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Nakumbusha tena wandugu. Msinichoke.......
   
 4. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Utamudu $600 kwa mwezi? karibu na bestbite
   
 5. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kwa bei hiyo ndiyo imenikimbiza Kariakoo. Kwa bei hiyo ningelitafuta hata kwenye mall za bei juu na kuuza vipodozi kutoka Coty au Cosmopolitans. Kwa sasa nataka zaidi kusambaza na si kuuza rejareja. Kwa maana hiyo sihitaji sehemu nzuri saana zaidi ya kitu kama Stoo ambapo itakuwa ni rahisi watu kuja na kununua kwa jumla na wao kwenda kuuza na kupata faida nzuri tu kuzidi hata mie (Kwa chupa moja).

  Ndiyo maana natafuta sehemu za bei nafuu ili nisipandishe bei ya uuzaji wa jumla. Siku nikianza kuchukua kutoka COTY ambako nina contact zao zote basi nitakutafuta na kuwa tayari kulipa hiyo gharama ya dola $600 kwa mwezi. Kama kwa mwezi ntaingiza faida ya dola walau $2,000 why not?

  Karibuni wanafunzi ambao wanaweza kununua na kwenda kuuza vyuoni kwao. Hadi sasa kuna wanafunzi kadha walichukua kwa majaribio ila kwa sababu vyo vimefungwa, uuzaji wake kidogo kasheshe. Nina uhakika mtu akinunua kwa jumla, ataweza kwenda kuuza na kifaida chake kupata siku vyuo/shule zikifunguliwa. Product zote made in EUROPEAN UNION na bei ni nafuu sana ukilinganisha na ubora

   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Sasa wewe unaweza kodi mapaka ngapi kwa maeneo hayo?
   
 7. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Natafuta kisehemu kidogo kwa bidhaa chache zitakazokuwepo hapo Stoo. Kama kuna mtu atataka bidhaa nyingi basi ataweza kuacha anwani na tunampelekea dukani kwake/nyumbani kwake. Hivyo bidhaa nyingi hazitakuwepo hapo zaidi ya chache kwa wanunuzi wa rejareja na Testers. Hii yote ili kukimbia kupandisha bei ya bidhaa zangu ambazo zitakuwepo zaidi kwa wanaotaka kununua jumla.

  Nipo tayari kulipa hadi Tsh 150,000 kwa mwezi. Zaidi ya hapo naogopa kupandisha bei bidhaa zangu kwani siku zote ni mteja hupandishiwa gharama. Si lazima iwe sehemu nzuri saana. La muhmu kwangu iwe ni sehemu inayofikika kiurahisi na ipo maeneo hayo niliyoyataja. Nataka gharama zangu ziwe chini sana ili mwisho wa siku, wanunuzi wa jumla, wanunue kwa bei nafuu.

   
 8. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #8
  Jul 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Bado nipo nipo tu nazidi kuwambusha.......
   
 9. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #9
  Jul 2, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Habari za Jumamosi wana mtandao? Nilikuwa napita tena.....
   
 10. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,332
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Go ahead kijana. Pia waone madalali na friends waliokaribu na maeneo hayo ili wasaidie kupata hiyo room...... Nadhani utafanikiwa.
   
 11. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wewe unataka kuongeza idadi ya posts nini? Kama huna la kusema sio lazima upost kitu. Ukipita na kusoma ya wenzio ni lazima utujulishe kama umepita....gggrrrrr
   
 12. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #12
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Nashukuru kwa msaada wa mawazo Mkuu. Je unaweza kunipa contact za hao madali kama unazo? Mie si mwenyeji sana wa Dar kwa sasa.

  Asante tena kwa kupita hapa na kuchukua muda wako kuweka mstari huu chini.

   
 13. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #13
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ghost, nashukuru sana kwa msaada wako na mawazo yako naahidi ntayafanyia kazi. Samahani kwa kukukwaza na kukuletea kichefuchefu. Maelezo yako yamenisaidia sana kupata Frame. Ubarikiwe.
   
 14. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, pale Kinondoni Studio kuna frame mpya bei zake sio mbaya 200,000 kwa mwezi
   
 15. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #15
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu Chatu dume, nashukuru sana kwa habari/ujumbe wako. Kama nilivyosema, bei sintataka kuzidi 150,000 kwa mwezi kwa sababu sitaku kuuza kwa bei juu maana mie ntataka zaidi kuuza kwa jumla na kwa maana hiyo, itakuwa vema nikiwa ninapunguza matumizi kwa kila hali na pia kupunguza faida yangu kwa kila hali maana bei chini kwa bidhaa nzuri, itanisaidia bidhaa zangu zijulikane kwa haraka kwa watu wengi.

  Tangazo langu la biashara litakuwa "kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza." Nafahamu kuwa kwa dunia ya leo, hilo haliwezekani kwa kufanya direct translation. Ila ninaamini kuwa kila atakayejaribu, ataipenda na kununua na nyumbani atawaambia wengine na wao waje kununua.

  Anyway, kama utaweza kunipa anwani haswa, ntashukuru sana. Vinginevyo basi ntawaagiza jamaa zangu waende hapo Kinonondoni Studio na kuulizia juu ya hiyo Frame. Ubarikiwe.

   
 16. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #16
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kumbe tupo wengi hapa wenye shida hii. Tujulisheni basi hata simu za hao madalali:

   
 17. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu jitahidi sana kuhakikisha bei ya frame inakuwa chini, ukienda pupa utapigwa bei ya juu na kama ujuavyo mambo ya business cycle yalivyo. Nimependa sana jinsi ulivyo plan namna ya kuifanya business yako na msimamo ulionao. Japo pia unaweza kulazimika kubadili uamuzi wako wakuhusu pango la mwezi. But vuta subira na MUNGU atakusaidia utapata tu sehemu.
   
 18. u

  ureni JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka kuna madalali pale kinondoni wanakaa pale kwenye maduka ya msikiti wa mtambani walishawah kunitafutia nyumba nzuri tu kinondoni,nenda pale uulizie jamaa mmoja anaitwa mohamed namba yake sina tena maana ni mda kidogo.
   
 19. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #19
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Richa Dad, asante sana kwa kunipa moyo na ushauri wako kwa ujumla. Ni kweli kuwa bei nitapandisha baadaye maana hadi sasa nimepigana na jamaa wananiuzia kwa nusu bei kama promotion. Wakianza kunicharge bei ya kawaida, kuna kupanda sana na labda kutoka bei hiyo ya max. 20,000/- hadi kwenye 30,000/- kwa chupa moja.

  Ila maadamu nataka kujijenga kama msambazaji wa kuaminika, ntajitahidi kuweka bei ziwe chini sana kwa mie kutafuta kipango cha bei nafuu. Ningelikuwepo mwenyewe basi ningeiomba kuwa na kikabati katikati ya hall maeneo kama Mlimani City au Super market nyingine wanakupa kachumba kadogo tu kwa bidhaa zangu chache.

  Huko mbeleni, nataka niwe nachukua moja kwa moja kutoka Ufaransa au Spain maana huko ndiko viwanda vikubwa na vizuri vya perfumes na cosmetics kwa ujumla. Hapo itabidi sasa kuvamia hao akina Mlimani City ila sasa si kama muuza jumla ila muuzaji wa rejareja.

   
 20. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #20
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ureni, asante sana sana. Sasa wewe ndiyo umenipa habari kamili maana nimekuwa naambiwa vitu ila mwenyewe sielewi kinachoendelea maana si mwenyeji wa Dar kwa sasa. Ntawaambia jamaa waende hapo kuwatafuta hao madalali maana naona huwezi kupata kitu kwa sasa bila wao. Huu umafia kwa sasa naona unakuwa dunia nzima. Ntafanyia kazi maelezo yako. Weekend njema wadau wote mliotokea hapa.
   
Loading...