Upatikanaji wa flemu Mwenge, Sinza, nk - dar na bei zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upatikanaji wa flemu Mwenge, Sinza, nk - dar na bei zake

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Masomi, Jul 14, 2011.

 1. M

  Masomi Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana - JF nina mpango wa kufungua kijiduka cha VIPODOZI maeneo ya MWENGE, SINZA au sehemu nyingine inayofaa kwa biashara hiyo kulingana na ushauri wenu wadau.

  Naombeni msaada wenu wa namna ya kupata flemu kwenye maeneo hayo niliyotaja au hata sehemu nyingine ilimradi iwe na mkusanyiko wa watu na inayofaa kwa biashara hiyo, makadirio ya bei za flem kwenye maeneo husika yatanisaidia pia.

  Pia natumai nitapata ushauri mzuri kutoka kwa wadau wa biashara hiyo juu ya changamoto zake na namna ya kukabiliana nazo maana ndio niko kwenye mchakato na najaribu kufanya reserch kabla sijaingia rasmi.


  Asanteni..... naomba kuwasilisha! ​
   
 2. duda

  duda Senior Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ongea na madalali ndo wanajua frem
   
 3. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Wewe ni Muha au Mchaga kama sio wa hayo makabila ni ndoto kupata fremu za biashara pale Mwenge watu wa asili ya makabila hayo mawili ndio wamehodhi fremu zote pale Mwenge
   
 4. M

  Masomi Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli natambua kwamba nahitaji kuongea na madalali lakini hapa pia kuna wadau wengi wakiwemo madalali pia wanaoweza kunipa angalau mwongozo wa kufuata, ushauri dhidi ya changamoto za biashara yenyewe pia ni muhimu na unapatikana kwenu wadau!

  Nashukuru na nazidi kusubiri msaada wenu.
   
 5. M

  Masomi Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah jamani hata kwenye ujasiliamali kuna ufisadi na ukabila pia, anyway naomba nisiamini katika ukabila cha msingi ninaimani humu kuna wadau wengi wanaoweza kunisaidia kwa ushauri, hata hivyo si lazima iwe Mwenge bali hata sehemu nyingine ilimradi iwe na sifa za kuweka duka la vipodozi!
   
 6. bank

  bank Senior Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  magomeni fundikira zipo za kumwaga sema tu biashara pale haijachangamka.
  Kupta fremu zipo ulizia fremu za mmiliki tarakea restaurant bei ni kubwa kidogo nafikiri kuanzia laki 8 kwa mwezi na kuendelea
  Otherwise tumia dalali kupta fremu nzuri ni vigumu kujua bila kuwatumia wale
   
 7. M

  Masomi Member

  #7
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana Bank, nitayafanyia kazi hayo yote ila tu hapo kwenye red sijakuelewa vizuri, nitashukuru kama utanifafanulia zaidi hilo eneo liko wapi?
   
 8. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  fremu mwenge zinapatikana!ila tatizo ni eneo!zipo zile za vichochoroni hata leo ukitaka utaipata tuu!cha muhimu tia timu hapo mwenge ulizia madalali watakuonyeshea kila kona na bei pia watakuambia.
   
 9. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #9
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Masomi,

  Mie nina shida hiyohiyo na niliandika tangu wiki jana. Mie nahitaji kasehemu kadogo tu kwa ajili ya Sample chache na Tester maana zaidi nataka kuwa nauza kwa JUMLA. Product zangu zote zatoka Europen Union na hivyo ni quality nzuri ukilinganisha na bei. Kama ukipata sehemu ndogo na ukawa huitaki (Isizidi 150,000 kwa mwezi) basi nijulishe mie.

  Kama wee wahitaji sehemu kubwa basi nikipata sehemu kubwa ntakujulisha. Pia kama utahitaji Perfumes au vipodozi vya aina fulani, nijulishe kwani naweza kuwa nakutafutia na kukuzia kwa bei nafuu sana. Lengo langu ni kuwa nijulikane kama Msambazaji na si kutajirika kwa siku mbili. Hiyo inanifanya niuze kwa bei nafuu sana na wauzaji wa rejareja wanapata faida kuzidi hata mie kwa chupa.

  Ukipata simu za hao madalali, na ukawa umemalizana nao, basi ntashukuru na mie ukinitumia.

  Thanks in Advance.
   
 10. M

  Masomi Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru parachichi, next week nitakuwa Dar nitafika maeneo hayo japo vya uchochoroni inawezekana visinifae sana maana si unajua biashara ya vipodozi inafaa sehemu yenye mkusanyiko wa watu, anyway nitafika nionane na hao jamaa.
   
 11. M

  Masomi Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekupata vizuri sana ssambali, labda ungeniambia hiyo ndogo iwe angalau na vipimo gani na sehemu gani unazopendelea ili nikipata inayofanana ndo nikujulishe, vilevile hata mm si lazima iwe kubwa sana lakini hata size ya kati (10ft. x 8ft.) inaweza kunifaa pia.
  Cha msingi ni kwamba angalau wewe utakuwa unatafuta na mm natafuta pia na nguvu zetu zikiwa pamoja tutafanikiwa. Suala la hivyo vipodozi nadhani nikishapata flemu ndo tutaongea vyema maana nitahitaji.

  Thanks
   
 12. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Nipigie tuongee 0754 827198
   
 13. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Nipigie upate frem mwenge 0716099463
   
 14. M

  Masomi Member

  #14
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wana JF, bado naendelea na huu mchakato, yeyote mwenye taarifa zinazoweza kunisaidia afanye hivyo.
   
Loading...