Mbalamwezi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2007
- 800
- 175
Ni kweli kwa hapo ya 6cylinder itakula mafuta kidogo kuliko ya 4cylinder sababu hiyo ya 4cyl itakuwa na nguvu kubwa sana ya kujichimbia inapokuwa katika mwendo hivyo kutumia mafuta ya cc 2000 kenda umbali mfupi wakati ile ya 6cyl kwa cc hizohizo 2000 itaenda mbali zaidi maana haina nguvu ya kujichimbia ikiwa katika mwenda (inachanganya mwendo haraka).Logic ni kuwa kama gari ina cyljnder 4 na cc 2000 ni sawa na gari ya cylinder 6 ya cc 2000 ambapo ulaji wa mafuta ya 6 itakuwa na nafuu kidogo.
Zipo mbona mkuu au hauna utalaam hata kidogo na magariSijawahi Kuona Gari ya 6cylinders ikawa Na 2000cc. Huku north America Gari zote za V6 zinaanzia 3000cc hadi 4200cc. Wanajuwa zaidi fafanueni
Ndiyo maana nikasema kuwa sijaziona.. Sibishi unalolisema lakini kwa huku north America Magari hayo sijayaona, labda kwa Magari ya kijapani au ulaya. Ndiyo maana Nikasema nipewe elimu na wataalamu. Sina utaalamu wa Magari bali ni dereva wa muda mrefuuu. AsanteniZipo mbona mkuu au hauna utalaam hata kidogo na magari
swali lako kama sijakuelewa vizuri hivi .unataka utofauti wa nini mkuu muonekano nguvu? au ulaji wa mafutaaHabari wakuu naomba kuweka kwenu huu mjadala mtu anayetumia cc 2000 lakini four cylinder na anayetumia cc 2000 lakini six cylinder.
Hapo tofauti ni nin
Umejibu kihandisi kabisa. Na umefafanua vema kabisa mkuu.Cylinder zinawakilisha Horsepower (HP) ni kipimo cha nguvu zinazotumiwa au zinazozalishwa katika engine ya gari ambazo zinaanzia 4 mpka 12 au vinajulikana kama V4 ,V6,V8na V12 wakati cc, inasimamia kwa sentimita za ujazo kipimo ni 1/100 ya lita moja ya mafuta. rating ya mafuta katika injini horsepower kwa kawaida inatolewa na mtengenezaji kwa kasi maalum ya injini.
Haya mambo ya CC na clyinders hua ni changamoto.Niliwahi kununua Mazda rx 8 ya 2005 ina cc 1300 na 4 clyinders ila ulaji wa mafuta ilikua 1litre inaenda km 6.5 highway ila inakimbia sana kuliko altezza na hizi gari nyingine sa saizi yake.Tatizo cc ndogo lkn mafuta inakula v8 vile
Upo sahihi kwa 99%, ndio ukweli wenyewe...Nahisi unataka kuelewa jambo fulani muhimu sana ila ambalo ni pana na linachanganya kwa kiasi fulani kwa sababu ufafanuzi wake unahusisha vitu vingi vya mfumo wa injini. mbaya zaidi nahisi swali lako hujaliweka vizuri kutosha kueleweka unachotaka kutofautishiwa.
hata hivyo mm ntajifanya ulikuwa unaulizia hivyo vitu kwenye gari.
4 cylinder ni tofauti na 6 cylinder kwa upande wa nguvu ya gari pia matumizi ya mafuta.
kwanza fahamu kuwa cylinder ni mtungi unaopokea mafuta na kuyachoma ili yaweze kutengeneza nguvu ya kusukuma gari. mtungi huu una kitu kiitwacho pistoni kilichozama ndani yake na kina uwezo wa kuingia ndani na kutoka mithili ya pampu ya baiskeli unapojaza upepo tairi. pistoni hupanda na kushuka ndani ya cylinder, wakati pistoni inapanda huruhusu mafuta kuingia ndani ya cyinder na wakati inashuka hukandamiza na kuunguza mafuta yaliyoingia ambayo hutengeneza nguvu ya kusukuma gari. zoezi hili hurudia rudia kwa haraka sana na ndipo gari hutembea.
kujibu swaki lako
Ukisikia 4cylinder maana yake kuna mitungi minne ya kuchoma mafuta kwa wakati mmoja.. na 6 cylinder maana yake mitungi sita ya kuchoma kwa wakati mmoja...
1. ikiwa kila cylinder ina ujazo sawa wa lita 0.5 kwenye injini ya cylinder 4 basi kwa mpigo mmoja kila cyinder ya injini itachoma mafuta hivyo cylinder 4 zitachoma o.5 * 4= 2litre (2000cc)
japo kuna vitu vingine lkn kiwango cha mafuta yanayochomwa kwa mpigo mmoja huchangia kuamua nguvu ya gari.
ikiwa hiyo gari ya 6cylinder pia kila cylinder ina ujazo wa lita 0.5 inamaana kwa mpigo mmoja mafuta yanayochomwa ni 0.5*6= 3Litre (3000cc).
kwa hesabu hizo maana yake gar ya 4cylinder itakula mafuta kidogo kuliko ya ile ya 6cylinder, pia ya 4cylinder itakuwa na nguvu kidogo kuliko ya 6cylinder
2. sasa ili gari zenye idadi tofauti ya cylinder zile kiwango sawa cha mafuta itakuwa namna hii
Ikiwa injini ya 4cylinder inkula cc 2000 maana yake kila cylinder inabugia 500cc yaani cylinder moja ina ujazo wa 500cc tu, na kwa kadri vyilinder inavyoweza kuchoma mafuta mengi kwa pamoja ndivyo gari inavyokuwa sio na nguvu tu bali pia kasi japo kuna vigezo vingine vya kuamua.
ikiwa injini ya 6cyilinder inakula cc 2000 pia maana yake kila cylinder inabugia 333.3cc yaani cylinder moja ina ujazo wa 333.3cc tu. hivyo kwenye mpigo mmoja kila cylinder inachoma mafuta kidogo kuliko inavyofanyika kwenye injini ya cylinder 4. hivyo gari hii itakuwa na nguvu ndogo kuliko hiyo ya cylinder 4 japo itakuwa na uwezo wa kukimbia zaidi kuliko hiyo ya cylinder 4.
Kumbuka: nahisi ni nadra sana kukuta gari yenye cylinder nyingi kuwa na cc sawa na gari yenye cylinder chache. Mara nyingi kama sio zote gari ya cylinder nyingi huwa ina cc kubwa pia.
Koki za ukibwa gani maana kuna ½ ,¹ ,¾ n.kUmejibu kihandisi kabisa. Na umefafanua vema kabisa mkuu.
Kwa kuongezea na kwa muktadha wa swali ufafanuzi mdogo ni kuwa kwa mfano una tank zako say SIM TANKS ZA LITA 2000 ziwe mbili. Kisha ukajaza maji kwa ujazo huo wa Lita 2000 full capacity. Baadae kwenye Tank lako moja ukaweka cork 4 na lingine ukaweka cork 6. Halafu kwa wakati mmoja ukafungu koki za kila tank.
Maana yake hapo ni kuwa tank lenye cork6 zitatoa maji mengi na kuwahi kumaliza maji yote, wakati tank lenye cork4 litachelewa, na kimahesabu ya kawaida, lile lenye Cork 6 lina uwezo mara moja na nusu.
Hivyo kwa ulaji wa mafuta nadharia iko hivyo, sasa kwa engine ya gari pia inahusisha na nguvu kubwa kwa V6 Kuliko v4.
Elimu ya kuunga unga mna maswali ya shombo mno.Koki za ukibwa gani maana kuna ½ ,¹ ,¾ n.k
Elimu ya kuunga unga mna maswali ya shombo mno.
Umejibu kihandisi kabisa. Na umefafanua vema kabisa mkuu.
Kwa kuongezea na kwa muktadha wa swali ufafanuzi mdogo ni kuwa kwa mfano una tank zako say SIM TANKS ZA LITA 2000 ziwe mbili. Kisha ukajaza maji kwa ujazo huo wa Lita 2000 full capacity. Baadae kwenye Tank lako moja ukaweka cork 4 na lingine ukaweka cork 6. Halafu kwa wakati mmoja ukafungu koki za kila tank.
Maana yake hapo ni kuwa tank lenye cork6 zitatoa maji mengi na kuwahi kumaliza maji yote, wakati tank lenye cork4 litachelewa, na kimahesabu ya kawaida, lile lenye Cork 6 lina uwezo mara moja na nusu.
Hivyo kwa ulaji wa mafuta nadharia iko hivyo, sasa kwa engine ya gari pia inahusisha na nguvu kubwa kwa V6 Kuliko v4.
Zipo mark 2Sijawahi Kuona Gari ya 6cylinders ikawa Na 2000cc. Huku north America Gari zote za V6 zinaanzia 3000cc hadi 4200cc. Wanajuwa zaidi fafanueni
Tunatofautina kwenye blue, kwa sababu kwa muktadha wa cylinder hizo za V6 au V4 ni sawa na simtank kama nilivyotaja. Na kwa gari simtank ni lile tank la mafuta, na koki ni zile nozzle zinazopitisha mafuta. Kwamba ukiwasha gari lenye nozeli 4 na mwenzako akawasha gari lenye nozel 6 na mwingine awashe la nozel8, katu hicho kitu ulichokisema hakipo. Kwa nadharia ya Fluid Mechanics na Discharge, nadharia yako haiko hivyo.Mkuu naomba nitofautiane na wewe kwenye mfano wako.
Mkuu Unapozungumzia cc (Cubic Centimeter) au ci (Cubic Inch) ni metric/imperial units kama zilivyo kph, kg, meter, Ampere etc. So inapokuwa subjected to equal amount to each other maana yake inakuwa ni sawa sawa, mfano 1kg = 1 kg haibadiliki hata kama ni 1kg ya hewa vs ya kokoto. Hapo kitakachotofautiana ni vitu vingine mfano ujazo etc.
- Huu mfano ni sawa na mtu akauliza pikipiki ikiwa kwenye speed ya 100 kph na mark x ikiwa kwenye speed ya 100 kph kipi kitakimbia zaidi?
- Au Kati ya Kg 1 ya Pamba na 1 Kg ya mawe kipi kizito.
Now turudi kwenye mfano wako, Masimtanki mawili moja lina koki 4 na jingine lina koki 6. Kwa jinsi mleta mada alivyomaanisha ni kuwa hizi koki kwa kila tank zinatofautiana idadi lakini zikiwa combined koki 4 ujazo wa maji unaopitisha kwa kila sekunde moja ni sawa na ujazo unaopitishwa na koki 6 kwa sekunde. Hivyo ukifungulia zote kwa pamoja at the same time maji katika matank yote yataisha kwa wakati mmoja kwa kuwa discharge yake ni ya kiwango kimoja.
Turudi kwenye engine, ni sawa kabisa na nilivyoelezea hapo juu (Bolded blue). Now kwa kuwa Cylinder 4 combined zitakuwa na ujazo (cc) sawa kabisa na Cylinders 6. Hapa tofauti iliyopo ni kuwa kwa kuwa kila cylinder inatwanga/fires mara mbili kwa revolution moja, so a V6 itatwanga mara 3 kwa revolution, a V4 fires 2 times kwa revolution. Hapa inamaanisha kuwa cylinder 6 inakuwa na balance nzuri zaidi kuliko cylinder 4 in a row. So tafuti kubwa itakayokuwepo ni kuwa 6 cylinder will run significantly smoother than 4 cylinder. Hata acceleration ya 6 ni nzuri kuliko ya 4 cylinder.
Kuhusu Horsepower tofauti itakuwa ndogo sana kwa kuwa nguvu ya engine inategemea na kiasi/kiwango kinachochomwa chember ya combustion. Nguvu inayopatikana kutoka pistoni moja katika 4 ni kubwa zaidi ya inayopatikana kutoka pistoni moja katika 6 clyinder engine. So combined unaweza kuta tofauti ni ndogo sana.
Nipo tayari kuwa corrected.
Najitahidi kuelewa ulicho andika, vipi hapo una assume kuwa combustion chambers na pistons zina same measurement?Tunatofautina kwenye blue, kwa sababu kwa muktadha wa cylinder hizo za V6 au V4 ni sawa na simtank kama nilivyotaja. Na kwa gari simtank ni lile tank la mafuta, na koki ni zile nozzle zinazopitisha mafuta. Kwamba ukiwasha gari lenye nozeli 4 na mwenzako akawasha gari lenye nozel 6 na mwingine awashe la nozel8, katu hicho kitu ulichokisema hakipo. Kwa nadharia ya Fluid Mechanics na Discharge, nadharia yako haiko hivyo.
Concept ya tank niliyoitaja haijaangalia ile Horse power au kama gari ni full umeme (hybrid) bali ni normal case. Ulaji wa mafuta kwa normal case unazingatia concept ya uwingi wa nozzle ambazo ni zao la hizo Cylinder,na concept ya discharge capacity inakuja hapa. Hii ni elementary concept ambayo ukishaanza nayo inakufikisha kwenye uhalisia.