Habari za muda ndugu zangu wana JF, natumai mu wazima wa afya.
Awali ya yote ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa mkuu
ONTARIO na wachangiaji wengine wengi kama mashujaa wetu katika suala zima la kufamishana na kuelimishana kuhusu biashara hii ya Forex.
Katika pita pita na harakati zangu za kuhakikisha tonge linaenda kinywani ndipo nikabahatika kukutana na mnaijeria mmoja ndani ya bus la kuelekea mjini Mbabane nchini Swaziland kutokea Maputo nchini Msumbiji akiwa ameshika simu yake busy huku akifurahi mwenyewe na kucheka.
Ghafla uvumilivu ulinishinda na kutaka kufahamu ni nini haswa jamaa yule alikuwa akifanya maana alipatwa na furaha isiyo na kifani.
Baada ya kutupia jicho ndipo nikaona namba za bluu na nyekundu zikisoma kwenye kioo cha simu yake, kutazama kwa umakini ndipo nilipogundua kuwa alikuwa anatrade forex na kwa kuwa nilikuwa nimeshapata mwangaza wa taarifa kadhaa kutoka kwa boss
ONTARIO miezi kadhaa iliyopita humu JF ikanibidi nimsalimie bwana yule na kumuuliza ni nini haswa kiini cha furaha yake.
Katika maongezi ikabidi nimueleze ukweli kuwa mimi ni 'mweupe' kabisa yaani sifahamu ni jinsi gani ya kutrade forex ingawa nilikuwa nimeshapata kusikia kidogo ni nini forex.
Ndipo hapo aliponiambia kuwa laiti kama ungalijua utamu wa kitu hii wala usinge poteza muda wako kufanya mambo mengine. Baada ya kufika Mbabane akanipatia namba yake pamoja na FOREX pdf file ambayo nitaiattach hapa kwa ajili ya kujifunza na akaniomba nisisome kwa pupa wala haraka na pindi nitakapo maliza nisisite kumtafuta kwa msaada wowote ule.
Nimejaribu kuanzia mbali kidogo ili nanyi ndugu zangu muweze kupata picha halisi how really this Forex thing is, katika kipindi hiki ambapo tunasubiri Mafunzo zaidi kutoka kwa mkuu
ONTARIO .
This PDF file is very informative kwa beginners wote ambao wana nia ya kufahamu na kufanya FOREX TRADING.
Na pia si vibaya kuongezea hapa resources zozote ambazo zitasaidia kujinoa kuhusiana na forex trading maana walio wengi bado hawajapata mwangaza katika forex trading, maana haitakuwa vizuri kuingia darasani tukiwa vichwa vitupu.
Napenda kuwasilisha. Ahsanteni.