....Mtu alipotoka uko anakuambia heslb nayo n haramu...
...Daah na
Uislam ukikuingia inafika pahala unakua kama unaweweseka iv ata kama mama yako n mkrstu bas utamuona kafir
...
...
Kulikua na mzozo ukristu sio dini kwa sababu haijawai kuandikwa kwenye kitabu kuwa ukristu n dini kama ilivyo uislam n dini ya kwel na ya haki...
....
Nilikutana na mtoto anakuambia napenda sana madrasa kuliko shule yan anataka kuacha shule na baaz ya waislam niliokua nao wakashadadia kabisa....
..
Aya mtuletee maandio FOREX NI HARAMU
...
Halafu iyo tabia ya kulala na kuamkia kuvitia vitu uharam aisee mtafikia pabaya... Ulizuka mzozo kikombe cha babu loliondo n haram kuna waislam wengne walikataa kabisaa mbona imeswii
Leo hii fisi maji wawil watatu mnataka kulisha wenzenu ujinga, nakemea sana hii tabia, achen mara moja
Sijui akil zenu zpo wap, kuna mashek wanatia mikeka daily lakn apo apo kuna wengne wanakuambia haram[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Nae anatakiwa kuambiwa kitimoto haramKuna ustadh hafanyi Forex lakini anapiga kitimoto
Pole sana mkuu, nani tena aliyekufanyia huo mchezo??? 😀😀😀
Mkuu mbn jazba badala ya kuibua au kujibu hoja!Hawa waislamu wanaoishi dunia ya tatu ni wapuuzi sana(baadhi lakini akiwemo mleta mada) wana complications za ajabu kiasi kwamba hata ambao wamewaletea sheria za hiyo dini yao huwa wanawashangaa na kuwaona ni kama visiki tu wasivyojua dunia inaenda wapi. Kwa tasfiri fupi tu huyu jamaa ana twambia technology inapingana na dini yake!.
Anaongelea riba na speculation kama vitu haramu kwa muislamu yeyote kujihusisha navyo, anasahau kwamba hata serikali yake yenyewe tu inafanya speculation kwenye upangaji wa bajeti, anasahau kwamba hata wao wenyewe kuandama kwa mwezi huwa wana speculate.
Anatwambia forex ni haramu wakati cha kustahajabisha huko Dubai kwenye waislamu wenyewe ndio wamejaa ma forex traders kibao tu, yaani hawa waislamu wa bongo pasua kichwa wanasemaga eti hata mpira ni haramu wakati mataifa yaliyoshika dini ya kiislamu hapa afrika kama Egypt,Algeria,Tunisia ndio yanayofanya vizuri kimpira. Hawa macomplicator kama huyu mleta mada ni wakupuuza kabisa
Aisee bora muiache mtatupunguzia idadi ya wahitaji kwakweli. Na kitimoto pia ili kishuke beiSawa ndugu zangu waislam... Vp mikopo ya vyuo vikuu maana wanadai usipoanza kulipa baada ya mwaka mmoja tuuu unavyo maliza chuo kuna kariba pale kanapenyezwa... Na ukichelewa zaidi wana double.. Je! Mikopo nayo ya vyuo vikuu ndugu zangu waislam tuiache?
Hawa jamaa kila kitu ni dhambi hadi kuishimwisho wa siku mtasema kutumia JF kwa muislamu ni dhambi.
Assalam Alaykum,
Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyoeleza, uzi huu utajikita kujaribu kutoa mwanga kwa wasiofahamu juu ya uharamu wa biashara ya forex kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu.
Kwa siku za hivi karibuni, kumekuwa na uhamasishaji mkubwa sana juu ya biashara hii ya forex kupitia mitandao ya kijamii hapa nchini Tanzania. Waislamu wengi wa Tanzania, kwa kutofahamu dini yao ama kwa kughafilika tu, wamejikuta wakiingia kichwa kichwa kwenye biashara hii pasipo kuelewa kama ni halali ama haramu kwa mtazamo wa sheria ya dini yao.
Binafsi niliifahamu biashara hii ya forex ( na nyinginezo kadhaa) na kufungua Forex Trading Demo Account kati ya mwaka 2010 na 2011 wakati nipo chuo kikuu nje ya nchi (sitoitaja nchi), kipindi nasoma undergraduate. Kiukweli ni biashara inayolipa sana japo ni wachache sana wanaofikia daraja (level) ya kuwa washindi (in a long-term basis), wengi hupoteza pesa kwa sababu ni biashara inayohitaji elimu na uzoefu wa muda mrefu na uvumilivu wa hali ya juu na bahati pia.
Namshukuru Mwenyezi Mungu aliniongoza na nikafahamu kuwa biashara hii hainifai mimi kama muislamu na nikaweza kuachana nayo (japo iliniuma kimtindo, maana ni biashara inayolipa). Mimi nilichoangalia ni radhi za Mwenyezi Mungu kwangu hivyo nikaacha kujishughulisha na kuingiza kipato cha haramu kupitia hii biashara. Binafsi, Akhera kwangu ni muhimu kuliko Dunia.
Niliipoona biashara hii ya Forex imepamba moto nchini, nilijisikia vibaya kuona vijana wenzangu wa kiislamu wakiingia kichwa kichwa. Najua wengi ni kutojua dini tu, maana hata mimi nilikuwa vivyo hivyo mwanzoni. Hivyo niliona dhima kubwa ya kuwafikishia onyo juu ya kujihusisha na biashara hii. Nimeutua mzigo na mbele ya haki kwa Mwenyezi Mungu nitakapoulizwa nitajibu kwamba nilijitahidi kuwaeleza waislamu juu ya uharamu wa hii biashara.
Muhimu
Kuuza na kununua currencies tofauti (kama tanavyofanya kupitia Bureau de Change) si haramu kwa sheria ya kiislamu, kinacholeta uharamu kwenye biashara ya Forex ni System inayoendesha biashara yenyewe (yaani STP na ECN brokerage Systems).
Masheikh wengi wa Tanzania bahati mbaya hawana elimu ya Dunia, na hata hiyo elimu ya dini wengi wapo juu juu tu. Hivyo kamwe usijisumbue kwenda kuwauliza kuhusu Forex. Wengi hata hawajui Forex ni kitu gani kama ambavyo watanzania wengi walikuwa hawajui forex ni kitu gani.
Nakuletea Sheikh Hacene Chebbani kutoka Algeria ambaye anaishi Canada tokea mwaka 1997. Sheikh Hacene ana Masters in Islamic finance (UK, 2012) pia ana BA in Islamic Sharia kutoka Islamic University of Madinah (1993).
Nakuomba fuatilia lecture aliyoitoa Sheikh Hacene kwa wanafunzi kupitia Youtube kuhusu uharamu wa biashara ya Forex kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu.
Sheikh anazungumzia masuala mbalimbali ya hii biashara, tafadhali ewe muislamu usiache kuitazama lecture hiyo ili upate elimu juu ya masuala hayo.
Kwa wale watakaoshindwa kuitazama, angalau ondoka na Summary ifuatayo ambayo nimeiwasilisha kwa mtindo wa maswali na majibu (Q&A) kama ifuatavyo:
Swali: Je biashara hii ina Riba??
Jawabu: Ndiyo, Kuna riba kwenye biashara ya Forex
Swali: Je, Islamic forex Trading Accounts (Swap Free Accounts) zipo na brokers wanatoa hii huduma??
Jawabu: Ndiyo zipo. Forex brokers karibia wote duniani wanatoa huduma ya account maalum kwa ajili ya waislamu tu (Islamic Forex Trading Accounts).
Swali: Je, Islamic Trading Accounts zinahalalisha biashara ya forex kwa mtazamo wa Sheria ya kiislamu?
Jawabu: Hapana, Islamic Trading Accounts bado hazihalalishi biashara hii ya Forex kwa waislamu.
Pia Sheikh Hacene amezungumzia masuala mengine kama Margin, Leverage na nidhamu ya ukopeshaji/ukopeshwaji wa mtaji.
Nimetua dhima hii na kilichobaki ni juu yako wewe muislamu, chagua kutii ama kukaidi, Dunia ama Akhera. Hilo ni juu yako.
Namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu
Ahsante.
Pia soma fatwa hii hapa chini kutoka jopo la wanazuoni wa kiislamu:
Hapa utabaki wewe tu. Siwezi kuacha forex sababu ya upuuzi huu uliouleta hapa. Yaani dini yetu tunaroho mbaya sana, suala lolote lenye mafanikio ni haramu ndo tunaishia kwenye migogoro kama wenzetu Middle East
Too much, waislam wa bongo wasingeweza mshukuru mpo kwenye secular lawFuata sharia kijana... Usiwe kama wapenda dunia