Forex: Biashara Haramu kwa Muislamu

Forex: Biashara Haramu kwa Muislamu

nisaidie hili, hivi katika uislamu sharia zenye makatazo (yaani zinazotaja dhambi) ni ngapi? je zile za kuhalalisha nazo ziko ngapi? this is only out of curiosity.
Umenifurahisha sana, mimi nakupa jibu jepesi. Hao watu wao kila kitu haramu hawajui kuongea mazuri au kuja na njia mbadala ni watu kujifanya kujuwa dini wakati elimu yao ya mashaka. Ishi maisha yako vitabu vipo na omba Mungu akusamehe ikiwa umekosa ni yeye mpekee ana rehma za kusamehe.
 
Soma vizuri mada dada yangu.. Nimeelezea hilo.

HESLB hawakutozi riba maana wao sio wafanyabiashara. Wewe unalipa pesa nyingi kuliko ulizokopeshwa kwa sababu thamani ya pesa "ndogo" uliyokopeshwa kipindi unasoma ni sawa sawa kimanunuzi na pesa "nyingi" unayolipa sasa. Thamani ya manunuzi ni ile ile.
Kama kuna mtu anakatwa milioni 3 n mwengine milioni 10 n watu hao wanatofautiana kwa mwaka mmoja tu jee hapa unaelezeajee?
 
Mkuu, niambie maana ya riba?
Riba ni kile kiasi (fedha/mali) unachopata baada ya kufanya biashara (iwe ya kukopesha ama nyingine) , tofauti na mtaji wako wa awali. Najua wengi tafsiri yenu inaishia kwenye riba ya mkopo. But mkuu, mimi naheshima imani yako.
 
Assalam Alaykum,

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyoeleza, uzi huu utajikita kujaribu kutoa mwanga kwa wasiofahamu juu ya uharamu wa biashara ya forex kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu.

Kwa siku za hivi karibuni, kumekuwa na uhamasishaji mkubwa sana juu ya biashara hii ya forex kupitia mitandao ya kijamii hapa nchini Tanzania. Waislamu wengi wa Tanzania, kwa kutofahamu dini yao ama kwa kughafilika tu, wamejikuta wakiingia kichwa kichwa kwenye biashara hii pasipo kuelewa kama ni halali ama haramu kwa mtazamo wa sheria ya dini yao.

Binafsi niliifahamu biashara hii ya forex ( na nyinginezo kadhaa) na kufungua Forex Trading Demo Account kati ya mwaka 2010 na 2011 wakati nipo chuo kikuu nje ya nchi (sitoitaja nchi), kipindi nasoma undergraduate. Kiukweli ni biashara inayolipa sana japo ni wachache sana wanaofikia daraja (level) ya kuwa washindi (in a long-term basis), wengi hupoteza pesa kwa sababu ni biashara inayohitaji elimu na uzoefu wa muda mrefu na uvumilivu wa hali ya juu na bahati pia.

Namshukuru Mwenyezi Mungu aliniongoza na nikafahamu kuwa biashara hii hainifai mimi kama muislamu na nikaweza kuachana nayo (japo iliniuma kimtindo, maana ni biashara inayolipa). Mimi nilichoangalia ni radhi za Mwenyezi Mungu kwangu hivyo nikaacha kujishughulisha na kuingiza kipato cha haramu kupitia hii biashara. Binafsi, Akhera kwangu ni muhimu kuliko Dunia.

Niliipoona biashara hii ya Forex imepamba moto nchini, nilijisikia vibaya kuona vijana wenzangu wa kiislamu wakiingia kichwa kichwa. Najua wengi ni kutojua dini tu, maana hata mimi nilikuwa vivyo hivyo mwanzoni. Hivyo niliona dhima kubwa ya kuwafikishia onyo juu ya kujihusisha na biashara hii. Nimeutua mzigo na mbele ya haki kwa Mwenyezi Mungu nitakapoulizwa nitajibu kwamba nilijitahidi kuwaeleza waislamu juu ya uharamu wa hii biashara.

Muhimu
Kuuza na kununua currencies tofauti (kama tanavyofanya kupitia Bureau de Change) si haramu kwa sheria ya kiislamu, kinacholeta uharamu kwenye biashara ya Forex ni System inayoendesha biashara yenyewe (yaani STP na ECN brokerage Systems).

Masheikh wengi wa Tanzania bahati mbaya hawana elimu ya Dunia, na hata hiyo elimu ya dini wengi wapo juu juu tu. Hivyo kamwe usijisumbue kwenda kuwauliza kuhusu Forex. Wengi hata hawajui Forex ni kitu gani kama ambavyo watanzania wengi walikuwa hawajui forex ni kitu gani.

Nakuletea Sheikh Hacene Chebbani kutoka Algeria ambaye anaishi Canada tokea mwaka 1997. Sheikh Hacene ana Masters in Islamic finance (UK, 2012) pia ana BA in Islamic Sharia kutoka Islamic University of Madinah (1993).

Nakuomba fuatilia lecture aliyoitoa Sheikh Hacene kwa wanafunzi kupitia Youtube kuhusu uharamu wa biashara ya Forex kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu.

Sheikh anazungumzia masuala mbalimbali ya hii biashara, tafadhali ewe muislamu usiache kuitazama lecture hiyo ili upate elimu juu ya masuala hayo.

Kwa wale watakaoshindwa kuitazama, angalau ondoka na Summary ifuatayo ambayo nimeiwasilisha kwa mtindo wa maswali na majibu (Q&A) kama ifuatavyo:

Swali: Je biashara hii ina Riba??
Jawabu: Ndiyo, Kuna riba kwenye biashara ya Forex

Swali: Je, Islamic forex Trading Accounts (Swap Free Accounts) zipo na brokers wanatoa hii huduma??
Jawabu: Ndiyo zipo. Forex brokers karibia wote duniani wanatoa huduma ya account maalum kwa ajili ya waislamu tu (Islamic Forex Trading Accounts).

Swali: Je, Islamic Trading Accounts zinahalalisha biashara ya forex kwa mtazamo wa Sheria ya kiislamu?
Jawabu: Hapana, Islamic Trading Accounts bado hazihalalishi biashara hii ya Forex kwa waislamu.

Pia Sheikh Hacene amezungumzia masuala mengine kama Margin, Leverage na nidhamu ya ukopeshaji/ukopeshwaji wa mtaji.

Nimetua dhima hii na kilichobaki ni juu yako wewe muislamu, chagua kutii ama kukaidi, Dunia ama Akhera. Hilo ni juu yako.

Namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu

Ahsante.

Ahsante sana Ust. Abdoun. Jazakallah khayr.
Umetimiza wajibu wako kuwafikishia waislamu wenzako elimu husika. Ni juu yake mhusika kuchukua maamuzi sahihi bila kujali faida inayotokana na biashara hiyo. Hata hivyo wengi waliojaribu biashara hiyo wameangukia kupata hasara na majuto. Humu ndani ya JF wapo wahamasishaji ili watu wajiunge na pia wapo walikwishalizwa.
 
Kununua hisa za kampuni si haramu kiislamu. Sababu unakuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni/biashara. Ila hiyo kampuni unayonunua hisa isiwe inajihusisha na biashara haramu: ( mfano pombe, kamari, hisa za mabenki zinazojihusisha na riba etc)

Mfano kununua hisa za kampuni ya Apple (NASDAQ: AAPL) sio haramu, ni halali kabisa, sababu biashara zao ni kutengeneza simu na computer. Mfano pia hisa za makampuni ya kutengeneza magari, meli, ndege, satellite communication systems, ujenzi etc zote hazina tatizo na ni halali kabisa. Epuka hisa za kampuni za kutengeneza zana za kivita, makampuni yanayokopa kwa riba, utengenezaji wa vilevi etc
Sheikh apple wana Itunes na Apple music,moja inauza muziki na nyengine inatoa huduma ya kustream muziki na muziki kwenye uislamu ni haramu.

Alafu mada yako ndefu lakini hujagusia sababu hasa ya hyo forex kuwa haram.sio wote wataangalia hyo lecture.angalau ungeeleza kinagaubaga sababu halisi ya forex kuwa haram.utakuwa umefanya jambo la msingi.
 
Kaka, nimekuelewa swali lako

Jibu lake ni hivi; Uislamu ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu kuanzia anapoamka mpaka atakapolala. Hivyo kila jambo lina utaratibu wake kidini kuanzia; uchumi, siasa, elimu, afya, lishe, ndoa, mirathi, mahakama, etc Muislamu ni jukumu lake kusoma dini yake na kufuata utaratibu huo wa maisha. Muislamu anatakiwa ajue namna ya kuishi inward as well as outward kulingana na mafundisho. Hivyo basi there is such thing as "idadi" ya dhambi bali mtindo wa maisha.

Nadhani umenielewa kaka

hii ni sawa shekhe. lakini kama mtu anataka kujiunga na ummat naye kaja na desturi alizotoka nazo huko na kuna jambo haliko sawa na sharia akafa kabla hajajua naye anatenda kama vile sio tatizo. huyo atahesabiwa vipi. ni vizuri kama kuna mahali ambapo naweza kurefer ama toka kwenye kitabu chenyewe ama toka khadith. ni kujifunza tu kaka.
 
Ushoga na kufirana sio haramu kwenu?
Vipi uchangudoa?
Onyesha ukomavu wa fikra mzee,usiendeshwe na ushabiki wa kiitikadi.Mada imeandikwa kwaa ajili ya waislamu wewe unaumizwa na nini.hakuna tusi humo wala nini watu wanaelekezana mambo ta dini yao.hata logic ya comment yako siioni.ni sawa aanzishe mtu mada WAKRISTO TUEPUKE WIZI. NI DHAMBI.alafu mie nije na bangi zangu nikomment "kwahyo kuzini na kulitaja jina la bwana bure sio dhambi kwenye dini yenu?",does it make sense?.

Haya basi utuambie wapi umeona uislamu umeruhusu usenge?.grow up dude.dini sio uadui,ni mfumo wa maisha/lifestyle/itikadi,kila mtu ana uhuru wa kuamua afuate mfumo upi.
 
Assalam Alaykum,

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyoeleza, uzi huu utajikita kujaribu kutoa mwanga kwa wasiofahamu juu ya uharamu wa biashara ya forex kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu.

Kwa siku za hivi karibuni, kumekuwa na uhamasishaji mkubwa sana juu ya biashara hii ya forex kupitia mitandao ya kijamii hapa nchini Tanzania. Waislamu wengi wa Tanzania, kwa kutofahamu dini yao ama kwa kughafilika tu, wamejikuta wakiingia kichwa kichwa kwenye biashara hii pasipo kuelewa kama ni halali ama haramu kwa mtazamo wa sheria ya dini yao.

Binafsi niliifahamu biashara hii ya forex ( na nyinginezo kadhaa) na kufungua Forex Trading Demo Account kati ya mwaka 2010 na 2011 wakati nipo chuo kikuu nje ya nchi (sitoitaja nchi), kipindi nasoma undergraduate. Kiukweli ni biashara inayolipa sana japo ni wachache sana wanaofikia daraja (level) ya kuwa washindi (in a long-term basis), wengi hupoteza pesa kwa sababu ni biashara inayohitaji elimu na uzoefu wa muda mrefu na uvumilivu wa hali ya juu na bahati pia.

Namshukuru Mwenyezi Mungu aliniongoza na nikafahamu kuwa biashara hii hainifai mimi kama muislamu na nikaweza kuachana nayo (japo iliniuma kimtindo, maana ni biashara inayolipa). Mimi nilichoangalia ni radhi za Mwenyezi Mungu kwangu hivyo nikaacha kujishughulisha na kuingiza kipato cha haramu kupitia hii biashara. Binafsi, Akhera kwangu ni muhimu kuliko Dunia.

Niliipoona biashara hii ya Forex imepamba moto nchini, nilijisikia vibaya kuona vijana wenzangu wa kiislamu wakiingia kichwa kichwa. Najua wengi ni kutojua dini tu, maana hata mimi nilikuwa vivyo hivyo mwanzoni. Hivyo niliona dhima kubwa ya kuwafikishia onyo juu ya kujihusisha na biashara hii. Nimeutua mzigo na mbele ya haki kwa Mwenyezi Mungu nitakapoulizwa nitajibu kwamba nilijitahidi kuwaeleza waislamu juu ya uharamu wa hii biashara.

Muhimu
Kuuza na kununua currencies tofauti (kama tanavyofanya kupitia Bureau de Change) si haramu kwa sheria ya kiislamu, kinacholeta uharamu kwenye biashara ya Forex ni System inayoendesha biashara yenyewe (yaani STP na ECN brokerage Systems).

Masheikh wengi wa Tanzania bahati mbaya hawana elimu ya Dunia, na hata hiyo elimu ya dini wengi wapo juu juu tu. Hivyo kamwe usijisumbue kwenda kuwauliza kuhusu Forex. Wengi hata hawajui Forex ni kitu gani kama ambavyo watanzania wengi walikuwa hawajui forex ni kitu gani.

Nakuletea Sheikh Hacene Chebbani kutoka Algeria ambaye anaishi Canada tokea mwaka 1997. Sheikh Hacene ana Masters in Islamic finance (UK, 2012) pia ana BA in Islamic Sharia kutoka Islamic University of Madinah (1993).

Nakuomba fuatilia lecture aliyoitoa Sheikh Hacene kwa wanafunzi kupitia Youtube kuhusu uharamu wa biashara ya Forex kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu.

Sheikh anazungumzia masuala mbalimbali ya hii biashara, tafadhali ewe muislamu usiache kuitazama lecture hiyo ili upate elimu juu ya masuala hayo.

Kwa wale watakaoshindwa kuitazama, angalau ondoka na Summary ifuatayo ambayo nimeiwasilisha kwa mtindo wa maswali na majibu (Q&A) kama ifuatavyo:

Swali: Je biashara hii ina Riba??
Jawabu: Ndiyo, Kuna riba kwenye biashara ya Forex

Swali: Je, Islamic forex Trading Accounts (Swap Free Accounts) zipo na brokers wanatoa hii huduma??
Jawabu: Ndiyo zipo. Forex brokers karibia wote duniani wanatoa huduma ya account maalum kwa ajili ya waislamu tu (Islamic Forex Trading Accounts).

Swali: Je, Islamic Trading Accounts zinahalalisha biashara ya forex kwa mtazamo wa Sheria ya kiislamu?
Jawabu: Hapana, Islamic Trading Accounts bado hazihalalishi biashara hii ya Forex kwa waislamu.

Pia Sheikh Hacene amezungumzia masuala mengine kama Margin, Leverage na nidhamu ya ukopeshaji/ukopeshwaji wa mtaji.

Nimetua dhima hii na kilichobaki ni juu yako wewe muislamu, chagua kutii ama kukaidi, Dunia ama Akhera. Hilo ni juu yako.

Namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu

Ahsante.

kwenye kila jambo wapo watakao kuwa tofauti tu.
 
Sasa benki wakukopeshe leo alfu 10 baada ya miaka 5 ulipe alfu 10? Na wao wanafanya kama hao mikopo ya vyuo kufidia loss ya value. Tatizo hakuna shekh yoyote aliyekuja na system mbadala ya bank. Wakati sote tunajuwa kufanya biashara huwezi kuikwepa bank.
Inawezakana tena sana kama uko Dar pm nikupe lecture in any way possible
 
Mfano Lockheed wanatengeneza Ndege, Rocket, Na vifaa vingi vya defense je ni haramu kununua hisa zake au chukulia space X?

Hizo kampuni zilizo kwenye Defence Industry ndio hazifai kabisa.. Hawa jamaa huwa wanasababisha vita makusudi ili wauze silaha.. maana silaha mauzo yanakuwa juu watu wakipigana vita., ndio maana asikudanganye mtu kuwa hizi vita zitakwisha.. watu wanapiga pesa ndefu at the expense of wars., stocks za defense Industry hupanda bei wakati wa vita na hii ina mkono mrefu wanatumiwa hadi CIA kufanikisha.

n.b mgogoro wa Korea Peninsula kamwe hautokwisha.. kwa taarifa tu ni kwamba marekani anauza silaha worth billions of USD kwa nchi kama Japan, South Korea ili kujihami na makombora ya North Korea in the form of T.H.A.A.D Anti-missile systems, latest fighter jets, bombers etc
 
Riba ni kile kiasi (fedha/mali) unachopata baada ya kufanya biashara (iwe ya kukopesha ama nyingine) , tofauti na mtaji wako wa awali. Najua wengi tafsiri yenu inaishia kwenye riba ya mkopo. But mkuu, mimi naheshima imani yako.

Katika kila biashara kuna faida na hasara., Biashara ya kukopesha haina hasara yenyewe siku zote ni faida tu,. usiporudisha mkopo zitauzwa mali zako wapate faida yao.., yani wao hawana kitu kinachoitwa hasara kwenye biashara kwa sababu riba ni always positive.. na hapa ndio unapodhihiri uharamu. Mwenyezi Mungu kakataza Riba sababu ni "a form of Slavery"..
 
jamani zingatieni ma hili kuna pesa ambazo wale wa upande mwnigine ambao kuna vitu ni halali si halamu huwa wana toa misaada hata kwa wasio waislam haijarishi pesa ile ni ujira toka TBA, Kahaba, Forex trader nk...

ile pesa wengine huwa wanapokea.... sitaki enda mbali zaidi na kuhoji ule msaada wa Mh kwenda msikiti wa wilaya moja wapo pale pwani?

kama haya yanafanywa kwa kuto jua ni kwanini huwa hatuoji na kupokea hata halamu ile ikiwa inatoka ktk vyanzo visivyo halali
 
VP kuhusu Treasury bills and bonds ambazo pia hulipwa interms of interest rates from 1 to 15 years inafaa?
 
Katika kila biashara kuna faida na hasara., Biashara ya kukopesha haina hasara yenyewe siku zote ni faida tu,. usiporudisha mkopo zitauzwa mali zako wapate faida yao.., yani wao hawana kitu kinachoitwa hasara kwenye biashara kwa sababu riba ni always positive.. na hapa ndio unapodhihiri uharamu. Mwenyezi Mungu kakataza Riba sababu ni "a form of Slavery"..
Biashara ya mikopo pia ina hasara. Umesahau juzi tu mabenki yamepata hasara kwakuwa yamekopesha watumishi ambao kumbe walikuwa na vyeti feki? Hasara ipo huko kama ilivyo kwenye biashara nyingine.

Pia gharama za uendeshaji zipo kama kwenye biashara nyingine. Utalipa maafisa mikopo, wanasheria, utanunua makaratasi, wino, utakodi jengo la biashara (kama ni bank ama ofisi tu ndogo). Zote hizo ni gharama za uendeshaji wa huo mradi, pia kwakuwa huyu anayekukopesha ana mahitaji kama kula, mavazi n.k. Yote hayo ndio yanaingia kwenye riba ama faida.
 
Back
Top Bottom