foreman,na police nani bosi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

foreman,na police nani bosi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by white wizard, Jun 23, 2011.

 1. w

  white wizard JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 2,462
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  hivi hili jeshi la polisi linatupeleka wapi?kwani vituo vidogo vingi vya polisi vinawatumia mgambo(foremen) ktk kusaidia kwenye ukamataji,cha ajabu kuna kituo kimoja huku kuna mgambo kama wanne ni mwaka wa kumi sasa wapo hapo,hivyo wamekuwa kama mapolisi,na hata kupeleka mahabusu ktk vituo vikubwa.tatizo lao ni.haki za binadam ni msamiati kwao,halafu wamegeuza kituo hiki kama duka la mangi!kwani ukikamatwa dhamana ni pesa,na wameorodhesha viwango vya pesa kulingana na ukubwa wa kosa lenyewe!na wanadai wao wakubwa wa police wanawatambua kuwepo kwao,ila wanapataje kipato cha kuendesha familia zao,hawajui!ina maana wamebariki hiyo hali.na ukienda pale kama kuna ndugu yako amekamatwa,ukimuona mkuu wa kituo anakwambia hadi umuone mgambo akikubali bac tatizo lako limekwisha,ila akikataa basi mtuhumiwa wako hapewi dhamana!tusipoangalia polisi ndio watakao leta matatizo ktk nchi hii,hao wanaotaka kuchoma vituo vya polisi sio wajinga.ni dhuruma imezidi kwani wamegeuka kuwa wanasiasa!
   
 2. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mitaa ya wapi hiyo mkuu? Poleni sana aisee
   
Loading...