Forbidden cures za Dr. Mwaka - Vita ya kimaslahi

Deception

JF-Expert Member
Mar 27, 2014
1,183
3,143
Tukio lililotokea hivi karibuni la serikali kufungia kituo cha tiba za asili cha Dr Mwaka na wengine wachache ni mwendelezo wa vita ya kimaslahi kati ya tiba asilia na tiba za kimagharibi kwa muono mpana zaidi,lakini kwa kwa muono hafifu mahsusi kwa Tanzania unaweza kusema ni vita kati ya wanufaika wachache kutoka katika hospitali za serikali na wale wa tiba asilia.

Kuna msemo unasema,"if a story doesn't make sense,just follow the money and you will find the answer".Vivyo hivyo,kutokana na mtiririko wa matukio ya kufungiwa kwa kituo cha tiba asilia cha Dr Mwaka na wenzake,ukifuatilia kwa undani utagundua kwamba suala la maslahi binafsi ya kifedha linahusika moja kwa moja.Sababu zinazotolewa kwamba ndio kisingizio cha kufungiwa kwa vituo hivi hazina mashiko hata kidogo,lakini bado mwisho wa siku uamuzi wa serikali unabaki pale pale,KUFUNGIA TU.

Kwa mtazamo mpana,niliwahi kusema humuhumu kwenye jukwaa hili kwamba vita kati ya tiba asilia na tiba za kimagharibi ilianza zamani sana,werevu walinielewa kwa haraka sana,lakini wale ambao kwenye ubongo wao hakuna msamiati unaoitwa 'kujiuliza/kudadisi' walipinga papo hapo.Vita hii ilianza kwa uchache miaka zaidi 100 iliyopita.Pengine hata baadhi ya madaktari wa tiba asilia hawaijui vita hii,ndio maana wengine wanadhani kwamba chombo cha serikali(Baraza la Tiba Asilia na Tiba Mbadala) kina kazi ya kuendeleza na kusimamia tiba asilia nchini,fikra hizo si sahihi kabisa.Chombo hiko kingekuwa na kazi hiyo basi haya yote ya kufungia vituo vya tiba asilia kwa sababu zisizo na mashiko yasingetokea.

Nisingependa kujadili historia hii ya vita kati ya tiba asilia na tiba za kimagharibi ilikuwaje kwa undani,maana ni historia pana sana na ndani yake kuna mambo yasiyo na mantiki hata kidogo lakini ndio hayohayo mambo yanayotuua leo hii lakini sisi tunayashabikia pasipo kujua ukweli ulivyo,hii ni hatari sana.Yaani tunajiua huku tunashangilia kutokana na upumbavu tu wa kijinga.

Nina uhakika kuna watu watakurupuka na kuanza kupinga haya ninayosema bila hata kuhoji,hili si geni kwangu,kwa kuwa naijua jamii yetu ya kitanzania jinsi ilivyo.

Watu wamepumbazwa akili mpaka wanaona kwamba tiba asili kuitwa jina la tiba mbadala ni sahihi tu,na tiba za kimagharibi (ambazo ni sumu) kuitwa tiba namba moja ndio sahihi.Hata ukifuatilia vitabu vya dini ambamo ndani kwavyo kumeandikwa tiba zilizokuwa zikitumika kipindi hiko,utaona kwamba tiba asilia ndio zilikuwa tiba namba moja na zile tiba za sumu zilipingwa vikali,sina haja ya kutoa aya yoyote hapa,kwa mtu yeyote anayefuatilia vitabu vya dini analijua hili.Pia kisayansi tiba asilia ndio tiba namba moja,hii unaweza kuilezea kwa mfano mmoja tu kwamba,mtu akila vyakula bora asilia kinga yake itakuwa juu sana na kumlinda asipate magonjwa sugu yasiyoambukizwa na yale yanayoambukizwa,sasa akienda tofauti na asili ilivyo hapo ndipo atakapoanza kuugua.Ingawa pia kuna tiba hizohizo za asili unaweza kupona kabisa kama utatumia pale utakapoanza kuugua,lakini wengine wasiojua hukimbilia kula dawa za kimagharibi.Hivyo basi,ukiona mtu anaugua ujue kwanza kuna tatizo la upungufu wa mambo fulani yanayohitajika kwenye mwili wake au kuna ongezeko la mambo fulani yasiyohitajika kwenye mwili wake,hii inatokana na mtu kushindwa kwanza kufuata taratibu nzuri za maisha au kotokula vyakula bora vya asili.Sasa ukifikiri kwa undani huwezi kuita tiba za asili kwamba ni tiba mbadala.

Kama hata kati ya wagonjwa 20 walioshindikana kutibiwa na tiba za kimagharibi,5 kati yao wakaweza kupona kwa kutumia tiba asilia halafu bado chombo husika kinafungia vituo vya tiba asilia kwa sababu za kipuuzi tu,ujue hapo kuna tatizo,na tatizo hilo lazima litakuwa linahusiana na maslahi ya kifedha tu,fanya uchunguzi wako katika hili.Dr Mwaka anasema kwamba yeye anaponya wagonjwa 7 kati ya 10 walioshindikana katika tiba za kimagharibi,lakini ukweli ni kwamba,hata angefanikiwa kutibu mgonjwa 1 tu kati ya hao ilibidi serikali impongeze kwa hilo,lakini kinachofanyika sasa ni kinyume chake.Hata Dr Mwaka akitoa vithibitisho vya hiyo kazi ya kuponya aliyoifanya ni kazi bure tu,labda wamwachie kwa ujanja ujanja kutokana na aibu waliyonayo tu.

Hili linalotokea sasa kwa Dr Mwaka na wenzake nalifananisha na yale matukio yaliyowatokea waganga wa tiba asilia katika kipindi kilichoanzia miaka ya 1920 ambao waliweza kutibu ugonjwa wa saratani ambao tiba za magharibi zilishindwa.Madaktari hao walipata msukosuko mkubwa kutoka kwenye vyombo vya serikali yao kipindi kile,wengine walifungiwa vituo vyao kama inavyofanyika sasa kwa akina Dr Mwaka,wengine walifungwa kabisa gerezani kinguvu,wengine walichomewa moto vifaa vyao na kufanyiwa upuuzi unaofanana na huo.

Hapa ndipo hasa kile chombo kinachojishughulisha na kutetea haki za binadamu ndio mojawapo ya jambo muhimu sana kulishughulikia kama kweli wao wako makini na kweli wanafanya kazi kwa wito huo.Lakini kwa kuwa najua siku hizi kila kitu kinakwenda kinyume,hili si rahisi kutokea,maana sasa hivi mwizi ndiye anayesujudiwa,vyombo vya haki za binadamu ndivyo vinavyodidimiza haki hizo,viongozi wa dini ndio wanaoharibu maisha ya kiroho ya watu,vyuo vikuu ndivyo vinaharibu elimu,wanasheria ndio wanaodhulumu haki za watu,vyombo vya habari ndivyo vinavyoharibu habari za kweli,na madaktari(MDs) ndio wanaoharibu afya za watu.

Pamoja na hayo yote,najua bado watu hawaoni kama kuna jambo muhimu hapa la kutetea kuhusu afya zao,najua kuna watu wataleta ushabiki na hisia za kipuuzi.Uamuzi huu wa serikali unapaswa kupingwa na kila mtanzania ili kulazimisha chombo husika cha serikali kiache kutoa maamuzi ya kukurupuka kama haya.Mbona kipindi kile cha babu wa loliondo hawakutoa maamuzi kama haya?Au kwasababu kuna viongozi wa serikali nao walihudhuria kwa yule babu?Kama suala ni wagonjwa kutokupona,mbona Muhimbili,Ocean Road nk wanakufa wagonjwa wengi sana?Kama suala ni kutokuwa na sifa fulani,mbona kuna mambo ya kipuuzi sana kama vile wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji kwenye kiuongo kisichohusika pale Muhimbili?

Ushauri wangu kwa madaktari wa tiba asilia:
1.Masuala kama haya ni rahisi sana kushinda kesi zake kama mtaenda mahakamani,narudia,ni rahisi sana,labda mahakimu wawe wameshawekwa sawa tayari na chombo husika cha serikali kilichohusika kuwafungia.Lakini historia inaonesha kwamba kesi kama hizi madaktari wa tiba asilia huwa wanashinda mara zote kama haki itafuatwa.

2.Mimi najua kwamba cancer/saratani,kisukari na hata ile wanayoita HIV/AIDS(ambao si ugonjwa bali ni kasumba tu inayosababishwa na madara ya ARVs baada ya kuzitumia kwa muda mrefu),yote haya yanatibika vizuri kabisa na mtu anapona na kuendelea na maisha yake.Lakini watu hawayajui haya kwa kuwa vyombo vya habari vinaharibu habari.Ushauri wangu kwenu ni kwamba, msiseme hadharani kwamba mna uwezo wa kutibu mambo haya kwa kuwa mkisema hivyo mtakuwa mmeingilia maslahi ya watu,na watu hawa ni wakubwa sana na hamuwezi kupambana nao,ninyi fanyeni tiba zenu za mambo haya kimyakimya tu ili msikumbane na matatizo makubwa kutoka kwa hawa watu.

3.Kwa kuwa vita hii haitaisha leo wala kesho,basi kila mnapotibu jiwekeeni vithibitisho vya pathology katika kesi zote mnazofanikiwa kuzitibu ili mje kuzitumia mahakamani hapo baadaye kuwashinda hawa wadhalimu.Msifikiri kwamba vita hii itaisha leo,sasa jiwekeeni pathological proofs ili zije ziwalinde hapo baadaye watakapojitokeza tena kuwasumbua.

4.Jifunzeni uvumilivu,kwa maana hii ndio dunia tunayoishi sasa,mambo yote yanakwenda kinyume.Undeni chama chenu cha wale ambao ndio mnadhani mnafuatwa fuatwa sana na serikali, na mpange siku za kukutana kujadili jinsi ya kujilinda na watu wasiowatakia mema katika fani zenu.

Words of wisdom 1: "There is no profit in the western medicine if you are alive but healthy or you are dead,the profit only comes when you are alive but always sick".Think about cancer,diabetes and the like.

Words of wisdom 2: "If you want to get a lot of people very angry at you,and you are in health profession,it is fairly simple,just begin to cure 'incurable diseases' "

Fuatilieni hapa vita moja kati ya tiba za kimagharibi na tiba asilia:





Aksanteni.
 
Tiba za kisasa zina fitna kuliko Soka la Bongo, makampuni ya dawa ndio flagship!
 
Ninakubaliana an wewe Mkuu Deception baadhi ya Madaktari wanatupiga Vita sisi Watibabu wa Tiba za Asili na wanaitumia Serikaili katika kutupiga vita kwa ajili ya Maslahi yao.

Na hiyo Vita ipo siku nyingi kati ya hao Ma-Daktari wanaotumia Dawa za Sumu dawa za kizungu na sisi Waganga wa Tiba za Asili tunaotumia Tiba za asili. Na hicho chombo cha Serikali (Baraza la Tiba Asilia na Tiba Mbadala) kimewekwa na Serikali kutupiga vita sisi Wataalam wa Tiba za asili tunajuwa siku nyingi jambo hilo lakini kila lililo na mwanzo halikosi kuwa na mwisho wake. Wata shindwa tu hao Wanaotupiga Vita uchwara.
 
Man Found “Cures For All Diseases” HIV, AIDS, Diabetes, Cancer, Stroke, STDs, arthritis & More….. AND Has The Supreme Court Ruling To Prove It!

DR SEBI.jpg



A true healthcare reformer, who stood up against the American Medical Association in court, the list of diseases he can cure stretches to some of the most unsettling conditions people face today including: bipolar disorder, depression, ADHD, Mesothelioma, acid reflux and drug addiction.

Everyday it seems to become evermore clear that the human body has a powerful ability to heal itself naturally. One man in America took this notion all the way, changing history and widening the path towards the cure of all disease, his name is Dr. Sebi. A healer, pathologist, herbalist, biochemist and naturalist who immigrated from Honduras, he is a man dedicated to service as he shows people how to take care of themselves no matter the obstacles he faces.

In 1988, he took on the Attorney General of New York in a Supreme Court trial where he was being sued for false advertisement and practice without a license after placing ads in a number of newspapers, including the New York Post where he had announced:

“AIDS HAS BEEN CURED BY THE USHA RESEARCH INSTITUTE, AND WE SPECIALIZE IN CURES FOR SICKLE CELL, LUPUS, BLINDNESS, HERPES, CANCER AND OTHERS.”

Pre-trial, the judge had asked Dr. Sebi provide one witness per disease he had claimed to cure however when 77 in person witnesses joined him in court, the judge had no choice but to proclaim the Doctor NOT GUILTY on all accounts, proving he did in fact have the cure to all the diseases mentioned in the newspapers.

Several celebrities have sought out healing through the Doctor including: Michael Jackson, Magic Johnson, Eddie Murphy, John Travolta and the deceased Lisa Left Eye Lopes who proclaims in the video below:

“I KNOW A MAN WHO HAS BEEN CURING AIDS SINCE 1987”



source.Man Found “Cures For All Diseases” HIV, AIDS, Diabetes, Cancer, Stroke, STDs, arthritis & More….. AND Has The Supreme Court Ruling To Prove It!
 
Mleta made uko sahihi kwa kiasi Fulani lakini kwa Upande mwingine UNAPOTOSHA.
Kwa sababu.
1/Sio kweli haya kidogo kuwa Tiba Asili zote zipo kuponya. Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa waganga Wa Tiba Asili Wa ukweli kabisa walikuwa Zamani, katika zama hizi kila kitu ni biashara, na waganga wengi Wa Tiba Asili wa sasa ni waongo, matapeli na wajanja wajanja tu.

2/Sio kweli kabisa kuwa Tiba za kisasa ni Sumu tu, kwamba haziponyeshi. Ukweli ni kwamba Madawa mengi ya Tiba za kisasa yamefanyiwa utafiti Wa kutosha kabla ya kwenda kutumika. Uwezo Wa kutibu na kumuathiri mgonjwa unafahamika wazi wazi katika Tiba za kisasa.

3/Sio sahihi kabisa kuamini Tiba asili ndio tiba sahihi na Tiba za kisasa sio sahihi and vice versa. Usahihi Wa tiba hautegemei ukisasa au Uasili, Tiba yoyote inategemea chemikali iliyomo ndani yake na aina ya ugonjwa husika. Kama utachunguza kwa makini utagundua kuwa sehemu kubwa ya Tiba za kisasa ni matokeo ya kuiboresha tiba ya Asili kuileta kisasa.
 
Zanzibar-ASP, Mkuu unacho zungumza maneno yako sio ya ukweli kama ni wewe umetapeliwa na mganga wa Tiba ya Asili kwanini hukumpeleka mahakamani kumshitaki?
Dawa za Tiba ya Asili zinatibu maradhi mengi ambayo hayawezi kutibika Hospitalini Kwa Mfano

Maradhi sugu Yasiyotibika Mahospitalini Ukimwi,HIV,
Maradhi ya Hepatiti B
Virus, Maradhi ya Saratani (Cancer),Maradhi ya Figo ya aina yoyote yale,
Maradhi Ya Kifuwa Kikuu Maradhi ya Presha,Maradhi ya Moyo, Maradhi ya Kisukari, Maradhi ya Kiharusi (Stroke), Uvimbe kwenye Kizazi (Ovarian cyst) Fibroid,Maradhi ya UTI Sugu, Maradhi ya Pumu,na Maradhi ya Vidonda vya Tumbo
.

Haya tu ni baadhi ya Maradhi hayawezi kutibika Hospitalini na ukienda kwa waganga wa Tiba za Asili unatibiwa na kupona kabisa. Wewe labda ulikwenda kwa Waganga wa Tiba

za kiasili waganga matapeli ndio ukatapeliwa na hukupona huwezi kufananisha Vidonge

vya kizungu aka vidonge vya Sumu na Dawa za Asili alizo umba Mwenyeezi Mungu kuwa ni dawa sawa sio rahisi kabisa. Wazungu wanatengeneza Dawa zao uwe unatumia kila

siku mpaka wakati wako wa kuondoka duniani (Kifo) ukifika upate kuondoka na huponi tofauti na dawa za Asili ukitumia unapona ingawa unatakiwa utumie kwa muda mrefu.Mimi nina

kubaliana na Mleta Mada kwa karibu asilimia 100%100 anayoyasema ni ukweli mtupu.Ujumbe wangu soma hapo chini.

''THE PHARMACEUTICAL INDUSTRY DOES NOT CREATE CURES THEY CREATE CUSTOMERS''
 
Zanzibar-ASP,
Mkuu,huu ndio ukweli ila hii vita ya kibiashara ni two way.Usitegemee kuwa MziziMkavu atakuja kusifia dawa za kisasa.Wanachotakiwa kujifunza ni kuwa dawa nyingine za kisasa ni hizi hizi za kienyeji

Quinine ni magome ya Cinchona tree
Aspirin ni magome ya willow tree
Opioids hizi zatoka kwenye poppy plant

Usitegemee traditional herbalists watasifia dawa za kisasa kwa sababu nao pia zinawaulia soko lao
 
Just from one of your sentence TIBA ZA KIMAGARIBI NI SUMU???
Wewe huna habari kuwa Vidonge ni Sumu? na vina madhara kwa afya yako?

Madhara ya kutumia Dawa ya Diklofenaki


Madhara

Diklofenaki,diclofenac, inaweza kuleta madhara inapotumika katika matibabu, ingawa mara nyingi huleta maudhi madogo madogo. Hatari ya madhara ya diklofenaki huongezeka kadri inavyotumika kwa muda mrefu.

Diklofenaki inaweza kuleta madhara yafuatayo :

  • Vidonda vya tumbo na damu kutoka tumboni
  • Huongeza hatari ya kupata shambulio la moyo au kiharusi
  • Kupandisha shinikizo la damu (hypertension)
  • Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
  • Upungufu wa damu
  • Ini kushindwa kufanya kazi (liver failure)
  • Shambulio la pumu kwa watu wenye pumu
  • Kuwashwa mwili na kutokwa na vipele
Madhara mengine ni kama maumivu ya tumbo, kiungulia, tumbo kujaa gesi, kichefuchefu, kuharisha, kutapika na kizunguzungu.

Acha kutumia diklofenaki (diclofenac) na wasiliana na daktari wako pale unapopata yafuatayo;

  • Kutapika damu au kupata choo cheusi
  • Mwili unakosa nguvu sana
  • Macho au ngozi yako kuwa rangi ya njano
  • Vipele kwenye ngozi
  • Kuvimba miguu na mikono
  • Maumivu makali ya tumbo


FAHAMU KUHUSU MADHARA YA MATUMIZI YA DAWA YA PANADOL

Panadol


Watu wengi wana mtizamo kuwa dawa zinazouzwa katika maduka ya dawa baridi na maduka ya kawaida ya vyakula, yaani zile ambazo hazihitaji agizo la daktari ( over-the-counter (OTC) drugs ) ni salama.
Ukweli ni kwamba hali haiko hivyo kabisa. Nyingi ya dawa zilizoko katika kundi hili huko nyuma zilikuwa ni miongoni mwa zile zilizosimamiwa na kuratibiwa kwa karibu, huku zikitolewa tu kwa agizo la daktari.

Pamoja na kuondolewa katika kundi la dawa zinazohitaji kutolewa kwa agizo la daktari, bado dawa za OTC ni kemikali ambazo mara nyingi haziondoi kiini cha tatizo ulilonalo, na zinaweza kukupelekea kupata madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na kifo.

Mfano mmoja wapo ni dawa ya panadol, ambayo pia hujulikana kama paracetamol, acetaminophen, tyenol, nakdhalika.
Panadol ni dawa maarufu kweli kweli. Ni dawa maarufu hasa kutokana na uwezo wake wa kutuliza maumivu na pia kushusha homa haraka.

Watu wengi hunywa panadol bila ya kujiuliza chochote kuhusu usalama wake. Kupitia kwa wazazi na walezi wao, watoto wengi sana pia ni wabugiaji wa dawa hii.

Hii ni kutokana na wazazi/walezi wao kuamini kuwa kila mtoto anapolia basi mtoto ana maumivu, na au kila anapopata homa basi kuna ulazima wa kuishusha homa hiyo.

Kwa kiasi kikubwa tabia hii imejengwa na madaktari na wafamasia ambao nao hutoa dawa hii kwa wagonjwa bila kuzingatia usalama wake, na hivyo bila kutoa ushauri wowote kana kwamba dawa hizi ni salama kama maziwa!

Hatuna miundo mbinu ya kubaini idadi ya watu wanaoudhuriwa na matumizi haya ya kiholela ya panadol, lakini kwa kuangalia takwimu za nchi nyingine, bila shaka watu hao watakuwa ni wengi sana.

Nchini Marekani utumiaji uliopindukia wa panadol (overdose) umetambuliwa kuwa ndio sababu kuu ya simu zinazopigwa kuomba msaada katika vituo vya udhibiti wa sumu (Poison Control Centers) nchini humo, kila mwaka.

Panadol pia inatuhumiwa kuwa kila mwaka inasababisha kiasi cha watu zaidi ya 56,000 kupatiwa matibabu ya dharura, watu 2,600 kulazwa hospitalini, na kiasi cha watu 458 kupoteza maisha, katika taifa hilo. Sababu ya madhara haya inatajwa

kuwa ni kushindwa kwa kiwango cha juu kwa ini kufanya kazi.
Taasisi ya chakula na dawa ya Marekani (US Food and Drug Administration (FDA)) mnamo mwaka 2009 ilitoa maelekezo kuwa vifungashio vya dawa hii viwekewe onyo kuhusu uwezekano wa dawa hii kuharibu ini la mtumiaji.

Hatua hii ilikuja miaka 32 baada ya jopo la wataalamu kutoa ushauri kwa FDA kuwa onyo hili lilikuwa ni suala la ‘lazima’!

Katika hatua nyingine, kwa nia ya kupunguza madhara, mnamo tarehe 14 Januari, 2014 FDA ilitoa kauli iliyokuwa ikiwahimiza wataalamu wa afya kuacha kuandika maagizo ya dawa

(prescriptions) kwa dawa mchanganyiko ambazo miongoni mwake kulikuwa na vidonge (au vimiminika) vilivyokuwa na kiambata cha panadol kilichokuwa kikifikia kiasi cha miligramu 325.

Ni vizuri kuzingatia kuwa baadhi ya dawa za maumivu zinazotolewa kwa maagizo ya daktari kama vile Vicodin na Percocet, pia zina kiambata cha panadol na kwa hivyo hazipaswi kuchanganywa na dawa zingine zenye kiambata hiki.

UTUMIAJI WA PANADOL WAKATI WA UJA UZITO UNAWEZA KUCHOCHEA UGONJWA WA UTUKUTU MKUBWA KWA WATOTO

(Attention Deficit Hyperactivity Disorder –ADHD)
Hivi sasa kuna kundi la watafiti ambao wanahoji matumizi ya panadol kwa kina mama wajawazito.

Hoja yao ni kwamba matumizi ya dawa hii katika kipindi cha ujauzito yanaweza kusababisha mtoto atakayezaliwa kuwa na tabia ya utukutu uliokithiri.

Matokeo ya utafiti yaliyochapishwa katika jarida la JAMA Pediatrics, yanaonyesha kuwa panadol ni kitibua homoni ( hormone disruptor), na uwepo wa homoni usio wa kawaida mwilini wakati wa ujauzito unaweza kuathiri maendeleo ya kukua kwa ubongo wa mtoto anayeendelea kubadilika na kukua tumboni.

Utafiti huu ambao ulijumuisha takwimu zilizohusisha zaidi ya kina mama na watoto 64,000 kutoka katika kituo cha Taifa cha Kujifungulia cha Denmark (Danish National Birth Cohort), ulionyesha kuwa zaidi ya 50% ya wanawake waliohusishwa walitoa taarifa za kutumia panadol wakati wakiwa waja wazito.

Utumiaji huu wa panadol kwa wanawake hao olionyesha matokeo yafuatayo:

• Ongezeko la 30% la hatari ya mtoto kukumbwa na ADHD katika miaka saba ya kwanza ya maisha yake.
• Ongezeko la 37% la hatari ya mtoto kukumbwa na ugonjwa wa hyperkinetic disorder (HKD), ambao ni aina ya ADHD iliyopindukia mipaka.

Utafiti pia ulibaini kuwa kiwango cha madhara kilitegemeana na dozi. Kadri mama mjamzito alivyotumia panadol kwa wingi wakati wa ujauzito ndivyo jinsi ambavyo uwezekano wa mtoto kukumbwa na magonjwa yenye uhusiano na ADHD ulivyoongezeka.

Aidha kwa mujibu wa utafiti huu watoto wa wanawake ambao walitumia panadol kwa majuma 20 au zaidi wakati wa ujauzito walikuwa na kiwango karibu mara mbili cha hatari ya kukutwa na ugonjwa wa HKD.

MADHARA MENGINE YA KIAFYA YANAYOHUSISHWA NA MATUMIZI YA PANADOL

Ukiondoa uharibifu wa ini, panadol pia imehusishwa na madhara mengine ya hatari kama uharibifu wa figo pale inaponywewa na pombe, saratani za damu, madhara yanayopelekea ngozi kukumbwa na magonjwa kadhaa kama Stevens-Johnson Syndrome (SJS), toxic epidermal necrolysis (TENS), na acute generalized exanthematous pustulosis (AGEP), na kuzuia chanjo zisifanye kazi vizuri pale vinapotumiwa pamoja..

KUDHIBITI MAUMIVU
Kwa kuwa watumiaji wengi wa panadol, hasa kwa watu wazima, hufanya hivyo kwa nia ya kupambana na maumivu, ni muhimu wakajifunza mbinu salama na mbadala za kuondoa hayo maumivu.

Moja ya mbinu mujarabu sana katika suala hili ni kuhakikisha kuwa muda wote mwili wako haukabiliwi na uhaba wa maji. Mwili wako unapokabiliwa na uhaba wa maji akili iliyoko mwilini

mwako inawasha mfumo wa mgawo wa maji kidogo yaliyoko ndani ya mwili, ili kuzuia shughuli muhimu zinazotakiwa kuendelea mwilini zisije zikasimama.

Mfumo huu huratibiwa na kusimamiwa na homoni ya HISTAMINE, ambayo kunapokuwa na haja ya mgawo mwili huizalisha kwa wingi.

Kwa bahati mbaya ni kwamba katika harakati za kufanya kazi yake homoni hii pia huzalisha kiasi fulani cha maumivu katika maeneo mbalimbali ya mwili.

Ukiondoa uhaba wa maji mwilini, pia viko aina ya vyakula ambavyo huuchochea mwili kuzalisha kiasi kikubwa cha

HISTAMINE.
Ulaji wa vyakula hivi ni kichocheo kikubwa cha maumivu ndani ya mwili kwa muda wote.

Mungu akipenda katika post yetu ijayo tutaviongelea vyakula hivi kwa kina.

Tatizo lingine linalosababisha maumivu mwilini ni seli za mwili kukumbwa na mfuro/uvimbe mwako (inflammation) kutokana na baadhi ya vyakula tunavyokula, au kutokana na kuugua ugonjwa wowote ule.

Mfuro/uvimbemwako ni zao la kinga za mwili pale zinapoingia katika mapambano na magonjwa mbalimbali.
Mfuro/uvimbemwako unapotokea kwa muda mfupi tu siyo tatizo sana.

Tatizo linakuwa pale ambapo mfuro/uvimbemwako huo umekuwa ni kitu cha kudumu.
Miongoni mwa dawa nyingi za kifamasia utakazopewa na daktari wako kwa ajili ya maumivu ni zile zinazolenga kuzuia mfuro/uvimbemwako.

Hata hivyo kutokana na dawa nyingi za kifamasia kuwa na usalama unaotia shaka ni bora mtu ukajaribu njia za asili (natural) za kuzuia mfuro/uvimbemwako.

Upunguzaji wa vyakula vya wanga, hususan vile vilivyochakatuliwa, na upunguzaji wa matumizi ya mafuta ya kupikia yanayotokana na mbegu (polyunsaturated fats) ni moja ya njia nzuri sana za kudhibiti hali hiyo.

Baadhi ya vitu vinavoliwa pia ni visawazishaji vikubwa vya mfuro/uvimbemwako.
Hivi ni pamoja na chai ya kijani (green tea), manjano (turmeric), karafuu, vitunguu saumu, matunda ya jamii ya berries (mfano zambarau), zabibu, na vitamini C.

Tatizo lingine linalosababisha maumivu ni makovu yanayojitokeza ndani kwa ndani mwilini kufuatia kuumia kwa tishu mbalimbali ndani ya mwili.

Ulaji wa vyakula vyenye vimeng’enya vyenye uwezo wa kuyeyusha makovu hayo (proteolytic enzymes) ni njia moja mujarabu sana katika kupambana na maumivu ya aina hii.
Bromelain ni kimeng’enya kinachopatikana katika kigogo cha katikati ya tunda la nanasi. Kimeng’enya hiki kimebainika kuwa na nguvu sana katika kufanya kazi hii.

Kimeng’anya kingine kinachpatikana katika matunda ambacho pia kinaweza kufanya kazi kama bromelain ni papain.
Papain ni kimeng’enya kinachopatikana kwa wingi katika tunda la papai.

Sababu nyingine kubwa ya maumivu ndani ya mwili ni kemikali zinazoitwa prostaglandins.
Prostaglandins ni kemikali muhimu sana katika kuratibu shughuli kadhaa za baadhi ya viungo ndani ya mwili kama vile utambuzi wa maumivu, upanukaji na usinyaaji wa mishipa ya damu,

ufanyaji kazi wa mafigo, ufanyaji kazi wa mfumo wa uzazi wa mwanamke, ufanyaji kazi wa utando wa ndani wa njia ya chakula, nakadhalika.

Kutokana na moja ya kazi za prostaglands kuwa ni utambuzi wa maumivu, basi mfumo wa tiba za kisasa huchukulia kwamba kemikali hizi ni moja ya vyanzo vikubwa vya maumivu, na zimebuniwa dawa nyingi za kuzuia mwili kuzalisha kemikali hizi, au kuzizuia zisifanye kazi pale ambapo tayari ziko mwilini! Moja ya dawa maarufu sana katika suala hili ni asprin.

Tafiti za kisasa zinaonyesha kuwa asprin inafanya kazi hii kwa weledi mkubwa mno kiasi kwamba inafikia kuharibu seli za utando wa ndani wa njia ya chakula na kumsababishia mtumiaji vidonda hatari vya tumbo! Hata hivyo tafiti pia zimebaini kuwa

kiungo cha tangawizi ni mujarabu sana na salama katika kudhibiti maumivu yanayooanishwa na prostaglandins. Chai ya tangawizi ya moto itakuondolea tatizo hili na kukuacha huru bila maumivu, lakini pia ukiwa salama kabisa.

Mbinu ingine ya asili na salama inayotumika kutuliza maumivu, hasa ya misuli, ni kutumia losheni au cream zenye kiambata cha menthol. Menthol ni kemikali inayochujwa kutoka katika kiziduo cha mmea unaoitwa mint au pepper mint. Losheni au cream

yenye menthol hupakwa kwenye eneo lenye maumivu.
Menthol inapenya na kuingia ndani ambapo hupelekea mishipa ya damu katika eneo hilo kupanuka na kuongeza mtiririko wa damu katika eneo hilo. Kutokana na hali hii kemikali na virutubisho vinavyohitajika kufika katika eneo hilo na

kurekebisha tatizo hufika kwa wingi ndani ya muda mfupi na kufanya kazi yake. Menthol pia hujenga mazingira ya kufanya eneo husika lijione kama limeingiwa na ubaridi. Ubaridi huu hupelekea kupoozwa kwa hali ya kujisikia moto kunakozalishwa na mfuro/uvimbe mwako katika eneo hilo.

KUDHIBITI HOMA
Tofauti na inavyodhaniwa na watu wengi, homa ya kawaida siyo kitu kibaya. Homa inakuwa tishio tu pale joto la mwili linapopanda sana na kuzidi nyuzi joto 104 katika kipimo cha Fahrenheit sawa na nyuzi joto 40 katika kipimo cha Celcius.

Homa ni silaha inayotumia pia na kinga za mwili katika jitihada za kukulinda. Vimelea vingi vya maradhi havina uwezo wa kuishi mwilini na kuzaliana katika joto la mwili linalofikia nyuzi joto hizi. Joto la mwili linapozidi nyuzi joto hizi kunakuwa na hatari ya kuzuka kwa uharibifu wa protini za mwili, haswa vimeng’nya pamoja na mafuta ya mwili.

Kutokana na hali hii ni vizuri kuisimamia homa yoyote kwa ukaribu kuhakikisha kuwa joto haliendi nje ya mipaka iliyokusudiwa. Homa yoyote ambayo joto litakuwa ndani ya mipaka iliyokusudiwa itakuwa ni msaada mkubwa kwa mgonjwa

katika kuhakikisha kuwa anapona haraka.
Ni vizuri kuwa na kipima joto nyumbani kwa ajili ya kazi hiyo, badala ya kukimbilia kunywa panadol kila tunapoona kuwa homa imepanda. Kupitia kipima joto tukiona kuwa homa inataka

kupindukia mipaka ni vizuri kutumia sponji au kitambaa kilicholowekwa kwenye maji ya baridi kumkanda mgonjwa na pia kumpa maji ya kunywa ya kutosha. Mbinu hii itasaidia kushusha joto la mwili la mgonjwa bila kumsababishia madhara. Dawa

kama panadol zitumike tu pale ambapo jitihada nyingine zote za kurejesha joto katika hali ya kawaida zimeshindikana.

Credit : HERBAL IMPACT
 
MziziMkavu,
Hapa ndipo hua siwachukulii serious, story kama hiyo huna uhakika wowote ule kama ni ya kweli, umeitoa kwenye website yenyewe inaitwa conspiracyclub, huwezi thibitisha chochote zaidi ya story iliyoandikwa na mtu moja, hakuna cure ya AIDS ni maneno tu ila mkiwa comfroted kuprove mnabaki mnashangaa.

Mimi ni web developer, hizi kazi za kutunga story online ili kupiga hela nimezifanya sana tu toka zamani, na zinalipa sana, page kama hizo zinapata visits nyingi mno kwa speed, kutengeneza $100 kwa story kama hiyo ni kitendo cha fasta, ndiyo sababu watu wanazidi kuzitunga. Real information inapatikana kwenye real new sources, leta proof kutoka kwenye reliable sources, usikae ukajidanganya kua haya makampuni ya habari yanalipwa na drug companies kuficha ukweli maana ndiyo hua mnakimbilia huko.
 
Uluchosema ni kweli kabisa ila umeweza kusema kwa kuwa kuna watu walifanya tafiti na hizo dawa unazoita za magaribi na ndio maana kuna tahadhari?je kuhusu hizo za kikwetu kwetu ambazo hazijulikani kuwa na madhara gani kwa mtumiaji japo kwa kifupi zipo zilizo sababisha kupata matatizo ya figo na watu kuishia kufa au kufanyiwa dialysis?

Tofauti ni kwamba wanapamba upande mmoja tu na hawajui madhara ya wanazoziita dawa za asili? Kuna wengi wamepata kudhurika organ zao kama figo na ini wengine wameishia hospital wengine haihulikani? Kwa hiyo shida ni kutokua na ufahamu vizuri na hizo wanazoita dawa ndio maana nasema use them at your own risk sababu at the end kama ni kudhurika utaanza wewe na sio mimi.
 
Back
Top Bottom