Fomu za NIDA sasa zinauzwa hatari sana lazima tufikie uchumi wa kati

muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
2,115
4,801
Wakuu, wiki hii katika mihangaiko ya hapa na pale nilikuwa mkoani kigoma wilayani Kibondo. Kulikua na zoezi la uchukuaji fomu za kujaza kwaajiri ya vitambulisho vya taifa.

Zoezi hili lilikuwa ni kwaajili ya ambao majina yao hayakuonekana kwenye uhakiki na wale ambao hawakujiandikisha.

Cha kushangaza fomu zinauzwa kila fomu shilingi mia mbili.

Aisee hii sasa hatari nchi hii kwa sasa kila kitu kinauzwa, pesa inatafutwa kwa udi na uvumba.

Nahisi vitambulisho vikitoka tutauziwa pia.

Uchumi unazidi kuimarika

#Tanzania ya viwanda kuelekea uchumi wa kati
 
Tumezoea vya bure sana..nchi yyetu yenyewe bado maskini ila tunataka kuipa mizigo tuu! sasa 200 mtu analalamika kweli kuchangia 200 ktk nchi yako unapungukiwa nini? Tusiangalie vitu kwa Jicho tofauti...Nunua Fomu bwana mkuu acha lawama...umepoteza 200 ngapi hadi leo?
 
NIDA wenyewe wamesisitiza kuwa zoezi zima la upatikanaji kitambulisho cha UTAIFA ni bure kabisa.

Hakuna mahala ambapo utatakiwa kutoa fedha.

Hao wanao uza fomu hizo ni wapiga dili kama wengine.

Wakikamatwa hukumu yao ni pamoja na wahujumu Uchumi.
 
Mwanangu usipotoa watakuzungusha kweli.
Mimi nilienda mara moja nikaambiwa nifuate fomu kawe.
Sijarudi ten
 
Tumezoea vya bure sana..nchi yyetu yenyewe bado maskini ila tunataka kuipa mizigo tuu! sasa 200 mtu analalamika kweli kuchangia 200 ktk nchi yako unapungukiwa nini? Tusiangalie vitu kwa Jicho tofauti...Nunua Fomu bwana mkuu acha lawama...umepoteza 200 ngapi hadi leo?
Hujui haki zako?hata ingekua 50 sio sawa kutoa
 
Leta taarifa Kamila ni serikali ndio inauza au ni pesa ya kutoa copy ukiwa mvivu kufuata form kwenye kituo usika
 
Back
Top Bottom