Fomu za kugombea uongozi wa CCM zadoda Zanzibar ~ vijana wazisusa

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
792
1,144
DSC_1592-564x272.jpg

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk Ali Mohamed Shein wakinong’ona na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini,Unguja, Mohamed Raza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu mbali mbali za mpira wa soka. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Skuli ya Dunga, Kusini Unguja 28/4/17 :picha na Ikulu ya Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewaambia vijana na makada waliosusia kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho, kuwa ni aibu kutoa kauli ya namna hiyo kwa nchi yao.

Kauli hiyo ya Dk Shein imefuatia ile ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Sauda Mbamba aliyesoma taarifa ya mkoa huo mbele ya Dk Shein katika hafla maalumu ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vijana wa Jimbo la Uzini, akisema vijana wengi hawachukui fomu hizo.

Ikiwa ni kama majibu kwa vijana hao, Dk Shein amesema suala la msingi ni kuwa na uzalendo ambao ndiyo mwongozo sahihi katika kulinda heshima na nidhamu ya mtu kwenye jamii na taifa kwa ujumla.

“Kilio kikubwa cha vijana hao inawezekana ikawa ni suala la ajira, lakini suala hilo ni gumu kwani haiwezekani kila mtu kuajiriwa na serikali kama wengi wanavyotaka,” alisema Dk Shein.

Makamu huyo wa Mwenyekiti wa CCM amesisitiza ajira ni changamoto kubwa kutokana na kuwa kwa sasa idadi ya watu visiwani humo ni kubwa hali inayosababishwa na Wazanzibari kuzaliana kwa wingi ikilinganishwa na nchi nyingine.

“Hivi sasa Zanzibar tumeongezeka sana na hili linachangiwa na sisi wenyewe kwa kuzaa sana, hivyo ni vigumu kila mmoja kupata ajira serikalini kwa kuwa utaratibu wa ajira hauko hivyo,” alisema Dk Shein.

Awali, Sauda alimwambia Dk Shein kuwa pamoja na chama kutangaza kwa vijana kuchukuwa fomu za uongozi, bado fomu hizo zimedoda matawini.

Pia, Katibu huyo wa Mkoa wa CCM alisema jambo hilo linahitaji nguvu ya pamoja ya viongozi wakuu wa chama hicho kuwashawishi vijana kuchukuwa fomu hizo, ili kuomba uongozi katika ngazi za CCM.
 
Hhhh saivi watu wanaakili... Bado Walio funga maagano na damu ya kijani... Heri wenye uvumilivu maana Hao watauona ukombozi.
 
Kusini unguja na has a Dunga, kidimni, urowa, chwaka yaani ni eneo lilojaa wamakonde sasa kama ccm imesuswa ni balaaa. Ni eneo lenye vikosi viwili vya JW, Dunga na Ubago. Hatari xana
 
Wazenji wakicheza watashangaa CCM inaruhusu wabara kuja huko kununua viwanja na kufanya kazi hapo ndipo akili zitawarudi.
 
Kheeee kheeee mwanzo wa mwisho wa MACCM Zanzibar, lakini wahuni wanaweza kuwachukua buku 7 Ali mradi tu wanajua kuimba A E I O U wakagombee kule.

DSC_1592-564x272.jpg

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk Ali Mohamed Shein wakinong’ona na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini,Unguja, Mohamed Raza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu mbali mbali za mpira wa soka. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Skuli ya Dunga, Kusini Unguja 28/4/17 :picha na Ikulu ya Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewaambia vijana na makada waliosusia kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho, kuwa ni aibu kutoa kauli ya namna hiyo kwa nchi yao.

Kauli hiyo ya Dk Shein imefuatia ile ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Sauda Mbamba aliyesoma taarifa ya mkoa huo mbele ya Dk Shein katika hafla maalumu ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vijana wa Jimbo la Uzini, akisema vijana wengi hawachukui fomu hizo.

Ikiwa ni kama majibu kwa vijana hao, Dk Shein amesema suala la msingi ni kuwa na uzalendo ambao ndiyo mwongozo sahihi katika kulinda heshima na nidhamu ya mtu kwenye jamii na taifa kwa ujumla.

“Kilio kikubwa cha vijana hao inawezekana ikawa ni suala la ajira, lakini suala hilo ni gumu kwani haiwezekani kila mtu kuajiriwa na serikali kama wengi wanavyotaka,” alisema Dk Shein.

Makamu huyo wa Mwenyekiti wa CCM amesisitiza ajira ni changamoto kubwa kutokana na kuwa kwa sasa idadi ya watu visiwani humo ni kubwa hali inayosababishwa na Wazanzibari kuzaliana kwa wingi ikilinganishwa na nchi nyingine.

“Hivi sasa Zanzibar tumeongezeka sana na hili linachangiwa na sisi wenyewe kwa kuzaa sana, hivyo ni vigumu kila mmoja kupata ajira serikalini kwa kuwa utaratibu wa ajira hauko hivyo,” alisema Dk Shein.

Awali, Sauda alimwambia Dk Shein kuwa pamoja na chama kutangaza kwa vijana kuchukuwa fomu za uongozi, bado fomu hizo zimedoda matawini.

Pia, Katibu huyo wa Mkoa wa CCM alisema jambo hilo linahitaji nguvu ya pamoja ya viongozi wakuu wa chama hicho kuwashawishi vijana kuchukuwa fomu hizo, ili kuomba uongozi katika ngazi za CCM.
 
Rais anasema wamekosa ajira kwa sababu wanazaliana sana, wachina wangekuwa na hali gani?
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk Ali Mohamed Shein wakinong’ona na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini,Unguja, .
Ila ZNZ kuna majina ya kiaina aina mfano Mchambawima, Kibandamaiti, sasa na hili tena (bold)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom