Fomu za Edward Lowassa zilitimia?

Fomu za Edward Lowassa zilitimia?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Jana,wagombea wa CCM na CHADEMA walikwenda Mahakama Kuu ya Tanzania kusaini fomu za kuwasilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kulingana na matakwa ya Sheria za Uchaguzi. Wote wawili walijitokeza mbele ya Jaji Kihiyo.

Wakati Magufuli akiwasilisha fomu 40 za kusainiwa,Lowassa aliwasilisha fomu 6. Hiyo ni kwa mujibu wa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Mh.Kayoza. Kimahesabu,Lowassa hakuwasilisha fomu 34.

Fomu nyingine za Lowassa ziko wapi? Kwanini siziwasilishwe nazo kwa kusainiwa? NEC yaweza kumuengua asipotimiza masharti.

=================================

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli pamoja na mwenzake kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa, wamepigana vikumbo mahakamani huku kila mmoja akisaka kiapo cha mahakama kuthibitisha rasmi kuwania nafasi hiyo.

Magufuli na Lowassa kwa sasa wamekuwa mahasimu wa kisiasa tangu waziri mkuu huyo wa zamani alipotangaza kuihama CCM baada ya mchakato wa urais uliofanyika mjini Dodoma Julai mwaka huu.

Wagombea hao walikwenda jana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kupewa fomu kila mmoja kwa wakati wake ya kumthibitisha kuwania nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa nchi.

Wagombea hao walithibitisha fomu hizo mbele ya Jaji Sakieli Kihiyo kwa matakwa ya kanuni za uchaguzi wa Rais na Bunge za mwaka 2015.

Magufuli na Samia

Dk. Magufuli alikwenda mahakamani hapo akiwa ameandamana na mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan mbele ya Jaji Kihiyo saa tano na walikaa katika chumba cha mahakama kwa zaidi ya saa moja kwa ajili ya kusaini.

Baada ya kumaliza kuapa na kusaini Dk. Magufuli alitoka nje ya mahakama na kuzungumza kwa kifupi na wanahabari.

"Katika fomu ya kugombea nafasi ya urais inaeleza kwamba mtu anayetaka kushika madaraka makubwa azingatie kanuni na sheria zilizoainishwa .

"Kilichonileta hapa leo (jana) ni kukamilisha sehemu ya kanuni na sheria, kukagua fomu kwa ukamilifu na kusaini kiapo, naomba Watanzania waniombee,"alisema na kuondoka.

Lowassa atua

Waziri Mkuu Mstaafu, Lowasa alifika eneo la mahakama saa saba adhuhuri na kuelekea moja kwa moja katika chumba cha mahakama kwa ajili ya kuapa na kusaini fomu ya kugombea urais.

Lowassa alichukua nusu saa kumaliza mchakato huo na kutoka na alipotakiwa kuzungumza na waandishi wa habari alisema hawezi kusema chochote.

"Siwezi kusema lolote, tusubiri Tume ya Uchaguzi ikinipitisha nitazungumza,"alisema kwa kifupi Lowassa.

Msajili Mahakama Kuu

Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Msajili wa Mahakama Kuu John Kahyoza, alisema katika fomu za kugombea udiwani, ubunge na urais kuna kipengele cha tamko au kiapo cha kisheria cha mgombea.

"Leo wagombea urais wamekuja kuthibitisha kwa kiapo waliyoyajaza katika fomu ya kugombea nafasi hiyo ni sahihi, wamefanya hivyo kwa matakwa ya kanuni za uchaguzi na Bunge za mwaka 2015.

"Miongoni mwa wanayothibitisha ni kwamba wao ni raia wa Tanzania, wametimiza umri unaohitajika kisheria, hawajawahi kutiwa hatiani na kufungwa kwa kosa lolote ikiwemo kukwepa kodi.

"Fomu ikisharudishwa na kubainika kwamba miongoni mwa waliyoapa walisema uongo ni kosa la jinai hivyo aliyeapa anastahili kuchukuliwa hatua,"alisema.

Alisema madiwani na wabunge wanatakiwa kuapa mbele ya hakimu lakini haikueleza ni hakimu wa mahakama gani hivyo wanaweza kuapa kwa hakimu wa mahakama yoyote.

Alipoulizwa sababu ya Dk. Magufuli kutumia zaidi ya nusu saa, Kahyoza alisema wagombea urais walitakiwa kupita katika mikoa kumi kwa ajili ya kusaka wadhamini hivyo fomu zinatakiwa ziwe 40.

"Kundi la kwanza lililoingia la Dk. Magufuli lilikuwa na fomu zote 40, zikathibitishwa na kusainiwa.

"Kundi la pili la Lowassa waliingia na fomu zao nne, nikawauliza wakajibu ndizo walizoelekezwa, nikawashauri wakaongeze mbili, walifanya hivyo zikathibitishwa na kusainiwa.

"Kwa maana hiyo fomu 34 hazikuingia kwa ajili ya kusainiwa, sisi hata mgombea akija na fomu moja anasainiwa,"alisema na kuongeza kwamba hiyo ndiyo sababu iliyofanya mmoja atumie muda mwingi na mwingine atumie muda mfupi," alisema

Chanzo: Mtanzania
 
Mkuu, hiyo hoja hata mimi imenichanganya. Ina maana NEC walifanya makosa kumpatia fomu pungufu ama kuna fomu ambazo hakutimiza masharti yake? Tatizo ninaloliona mimi kwa miaka mingi ni masharti ya ujazaji fomu kuwachanganya wagombea. Nakumbuka kesi ya Sambwee Shitambala
 
Sijaelewa kinachoendelea.Labda wanasheria itabidi watueleze.Forms 40 na forms 6.Inamaana zote zinatakiwa zisainiwena MAHAKAMA au kuna zile za muhimu zinazotakiwa kuwasilishwa?Kama ni kweli inamaana mwanasheria aliyeenda naye hakujua hayo?

Ni kitendawili???Au ni ile ya kwamba ametumwa kuua upinzani????:scared::scared:
 
Kwenye picha alionekana Wakili Mabere Marando
 
Yuko sawa kwa kua fomu zinazosainiwa ni zile alizoombea wadhamini tu katika mikoa aliyopita
 
Kimsingi hua wanapewa fomu zote 40 kwa ajili ya kukusanya wadhamini lakini fomu 6 tuu ndizo zinakua na haja sana NEC ingawaje hata ukipeleka zote 40 wanapokea

Mkuu mbona pana umbali mkubwa kati ya 6-40…!! Ni kweli hizi 34 zote ni makapi tu…!???? Mhh sijui labda kweli
 
Kimsingi hua wanapewa fomu zote 40 kwa ajili ya kukusanya wadhamini lakini fomu 6 tuu ndizo zinakua na haja sana NEC ingawaje hata ukipeleka zote 40 wanapokea
Umeandika ukweli kabisa wale wanaojua watakuwa wamekuelewa
 
Petro E.Mselewa kwa bahati nzuri gazeti la Mwananchi walitaka ufafanuzi NEC na wakaambiwa fomu zinazotakiwa kurejeshwa NEC ni nne tu. Usihofu kwani tunao wanasheria mahiri waliobobea na ndio wanaotuongoza. Tutafika tu...
Jana,wagombea wa CCM na CHADEMA walikwenda Mahakama Kuu ya Tanzania kusaini fomu za kuwasilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kulingana na matakwa ya Sheria za Uchaguzi. Wote wawili walijitokeza mbele ya Jaji Kihiyo.

Wakati Magufuli akiwasilisha fomu 40 za kusainiwa,Lowassa aliwasilisha fomu 6. Hiyo ni kwa mujibu wa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Mh.Kayoza. Kimahesabu,Lowassa hakuwasilisha fomu 34.

Fomu nyingine za Lowassa ziko wapi? Kwanini siziwasilishwe nazo kwa kusainiwa? NEC yaweza kumuengua asipotimiza masharti.
 
Ndiyo maana nasema siielewi maana simuamini Lowassa isije ikawa kaja kuua upinzani kabisa

Usiwe na wasi wasi kila kitu kiko sawa mwaka huu hakuna hujuma zozote za kuua upinzani sitazofanikiwa tuna wanasheria makini sana .mwaka huu lazima ccm iondoke madarakani
 
Sijaelewa kinachoendelea.Labda wanasheria itabidi watueleze.Forms 40 na forms 6.Inamaana zote zinatakiwa zisainiwena MAHAKAMA au kuna zile za muhimu zinazotakiwa kuwasilishwa?Kama ni kweli inamaana mwanasheria aliyeenda naye hakujua hayo?

Ni kitendawili???Au ni ile ya kwamba ametumwa kuua upinzani????:scared::scared:

Acha uoga ndugu! Jiaminiiiiiii!!!!!!
 
Kuna wagombea kila wanachofanya ni habari:mod:, hii inadhihirisha kwamba mgombea husika anawapa hofu washindani wake?
 
Wana ni wengi sana,mbinu chafu ya kisiasa safari hii ni kikomo yao daaadeki•••••••••••••••••••piga kura hapa chini acha longolongo weee kijana mwenzangu

Piga kura yako ya maoni hapa Vote now and share results.
Matokeo utawez kuyaona live. Share na magroup mengne tuwez kupat pcha ya raisi ajaye.

VOTE ONLINE FOR TANZANIA PRESIDENT | #VOTE4TPO | Mayocoo , Special Voting portal

Wakuu angalieni lisijekuwa ndo bao la mkono lenyewe hilo!! Wakizingua tunahamishia kura zetu kwa Mwigamba (ha ha ha ha haaaaaaa!!)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom