ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 55,590
- 130,959
Upo sahihi kabisa, japo mimi nafikiri kuwe na zonal bus stands, kila zone iwe na stand kubwa yenye standards za ile ya Magufuli. Tegeta/Bunju kuwe na stand kubwa yenye viwango, Temeke/Mbagala kuwe na stand ya viwango vikubwa. Hii inq maana kuwa kama kampuni ya mabasi ya Shabbiby(mfano) anaweza kuwa na mabasi yake kwenye stands zote, mtu anayeishi Mbagala/Temeke akitaka kwenda Dodoma asilazimike kufika Mbezi, safari yake inaanzia Mbagala hadi anakoenda, mtu anaishi Mbezi/Tegeta, hana sababu ya kufata bus huko Mbagala ili kwenda Mtwara, safari yake ianzie Tegeta na kwenda anakotaka.Tatizo ni Fikra za hovyo za kuwa na stand Moja ya MBEZI inayolazimisha mabasi zaidi ya mia nane kuanzia safari zao pale.
Mabasi zaidi ya mia nane yenye abiria 50 ni idadi kubwa sana ya watu kuanzia safari sehemu Moja. Ikiwa na maana Kuna watu zaidi ya 40,000 wanaotakiwa kufika eneo Moja la MBEZI kila siku Kwa ajili ya safari TU achilia mbalili wanaokwenda Kwa ajili ya shughuli za kibiashara n.k.
Hali hii inasababisha tatizo lililokuwa Ubungo liwe limehakishiwa MBEZI. Daladala karibu Jiji Zima zinakua na Ruti ya Kwenda MBEZI Kwa wakati mmoja na Kwa Lengo Moja.
Haya ni matumizi mabaya ya akili ya Wataalamu wetu wanaohusika na jamii na miundo mbinu yao.
Miundo Mbinu inapaswa kulenga Ustawi wa watu na mazingira mazuri ya jamii kuishi vizuri bila Karaha ya kukosa hewa na Joto kwenye daladala Kwa masaa zaidi ya matatu. Kuchelwa kufika makazini na kwenye Biashara.
Kukosa muda wa kuwahi kufika majumbani na kupumzisha akili na kutafakari vyema masuala ya kazini na ufanisi wa kazi. Ndio maana utendaji unakua uko chini sana Kwa sababu watu hawapati muda wa kufikiri sawasawa zaidi ya kufika nyumbani saa Tano za usiku na kuamka saa Tisa. Kutumia muda Mwingi kwenye Foleni na mafuta kutumika sana kwenye magari hivyo kuwafanya watu kutumia ujanja ujanja wa kupata pesa za ziada za Kununua mafuta. Daladala kutanua Barabara na kuharibu miundo mbinu na kuisababishaia serikali hasara ya kukarabati miundo mbinu Kwa muda mfupi.
Tatizo ni wajanja wachache walioko kwenye mamlaka ya miji na majiji . Ubinafsi wa kutafuta tenda za kusimamia Standi na makusanyo ya ushuru ndio unaowaumiza watanzania.
Kwa Nini kila Wilaya Isiwe na Stand yake na mabasi yakaanzie Huko Huko na kuendelea na safari zao badala ya kulazimisha kila basi kuanzia na kuishia Sehemu Moja. Pangekua na Stend Kinondoni ,Ubungo (MBEZI), Ilala, Temeke na Kigamboni . Daladala zigawanyike kupeleka watu kwenye stand hizo ili huduma kubwa ibaki kuwa ni ya kuwapeleka watu maofisini na kwenye baisahara zao sio kuwapeleka watu standi Kwa ajili ya safari.
Tunamshukuru Mama Dr. Samia Suluhu Kwa kuimarisha Democrasia. Tunaomba aendelee kuimarisha na mfumo mzima wa Uchaguzi na Katiba ili tupate viongozi wenye uwezo na wazalendo halisi . Uchaguzi uwe huru na haki tuwapate viongozi makini sio Hawa wa kuwaza tenda za Jiji ndio maana chaguzi za madiwani na mameya zinageuka kuwa vita kubwa. Sio Kwa ajili ya kutatua Kero za wananchi Bali kupata tenda kwenye miradi na usimamizi wa ushuru.
Watanzania tufanye maamuzi sahihi wakati wa Uchaguzi . Tusiangalie Rangi za mashati na vyama Bali uwezo na hoja na maono ya mtu. Vyama vimetuangusha sana na vimekua ni kichaka Cha wezi kupitia na kujitajirisha kupitia fedha za umma huku wananchi wakiteseka .
Sijui kwa nini watawala hawafikirii nje ya Box.
Stand ya Mbezi ni nzuri, miundombinu ya kuingia na kutoka iko poa sana, ila ni kweli kuwa kuna idadi kubwa sana na daladala za kwenda-kutoka Mbezi hivyo kufanya kuwa na idadi kubwa sana ya watu katika eneo moja.