A
Anonymous
Guest
Foleni ya kutoka Mbagala Kizuiani kwenda Mbagala Rangi Tatu ni foleni ambayo haina ulazima kama askari wataamua kusimamia.
Unakuta muda askari wapo tu na vyanzo vya foleni wanaviona ila hawana muda navyo, wao wanaelekza nguvu zao kusimamisha Daladala ili kufanya yao huku Wananchi tukiendelea kuteseka kila siku.
Pia, watu wengine wanaochangia uwepo wa foleni ni Machinga, wanapanga vitu hadi barabarani, yaani inakuwa kero kero.
Barabara ya Watembea kwa miguu wamechukua yote na saizi wengine wanashuka hadi kwenye barabara kubwa wanapanga vitu.
Mamlaka zipo zinatazama tu, watembea kwa migu wanakosa pa kupita, magari nayo yanatembea kidogokidogo ili kutokuwajeruhi wafanyabiashara.
Imekuwa kero kubwa sana hii, tutaendelea na hali hii hadi lini?
Pia soma ~ Mbagala (Dar): Baadhi ya maeneo ya barabara yaliyokuwa yanazibwa na 'machinga' yaanza kuwa wazi