jT0078
JF-Expert Member
- Sep 26, 2016
- 430
- 331
Habari wadau!
Mimi ni miongoni mwa wakazi wanaoishi Kisemvule mkoa wa Pwani.
Tunatumia sana hii barabara ya kilwa kutoka au kwenda katika michakato yetu ya kila siku. Changamoto tunayokutana nayo ni foleni isiyoisha ya magari ukianzia hapo kokoto kuna mlima unashuka daraja la mzinga hadi unafika Kongowe.
Hili eneo ni changamoto na linakera sana, maana unaweza toka mjini mapema ila ukifika hapo unaweza kaa hadi masaa 5 kuvuka Kongowe.
Mamlaka zinazohusika sijajua hawana taarifa au huyu Mbunge wa huku sijawahi sikia akiongelea hii issue.
Tunateseka sana. Kwanza barabara imeshakuwa ndogo (nyembamba) ikiharibika roli ni vigumu kupishana.
Tunaomba TANROAD waje huku waone namna ya kutatua.