Foleni Dar: Tatizo ni traffic light au Polisi?

Foleni Dar: Tatizo ni traffic light au Polisi?

pilau

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
1,595
Reaction score
450
Hali inazidi kuwa tete, hakuendeki si asubuhi si jioni wala mchana, hakuna nafuu. Vipi ni bora trafiki waziachie taa za barabarani zijiendeshe au wao ndio waamue magari gani yapite?!
 
Huwa nashangaa sana unakuta traffic lights zinafanya kazi ila bado ma traffic wanahangaika, huwa najiuliza kwamba madereva sio wastaarabu au nini hasa. sababu sijawahi ona traffic wakihangaika maeneo ya posta na mnazi mmoja labda huwa wapo sijawahi kubahatika kuwakuta. ila tunahitaji centre maalumu itakayokuwa na wataalamu waliobobea kwaajili ya kusimamia na ku control traffic lights za jiji zima. wawe wana monitor kwa kutumia technolojia za kisasa. watumie hata cctv cameras
 
Taabu ni pale Taa na polis wanafanya kazi kwa pamoja. Mi huwa nachukia kitendo cha kuacha taa zinawaka halafu polis anarukia barabarani na mapolisi wengi ni wafupi. Mi ninatoka mbali nimeangalia taa ghafla polis huyo ... Inakera sana. Naomba watengenezaji was hizi taa waweke swichi za kuzima taa pindi polisi wanapokuwa katikati ya barabara
 
Huwa nashangaa sana unakuta traffic lights zinafanya kazi ila bado ma traffic wanahangaika, huwa najiuliza kwamba madereva sio wastaarabu au nini hasa. sababu sijawahi ona traffic wakihangaika maeneo ya posta na mnazi mmoja labda huwa wapo sijawahi kubahatika kuwakuta. ila tunahitaji centre maalumu itakayokuwa na wataalamu waliobobea kwaajili ya kusimamia na ku control traffic lights za jiji zima. wawe wana monitor kwa kutumia technolojia za kisasa. watumie hata cctv cameras

nadhani huwa ni flow ya magari...kuna kipindi Fulani kuna barabara zinakuwa na magari mengi hivyo kuhitaji huduma ya trafiki...nina fikiri ndo sababu!
 
Tatizo magari ni mengi ambayo ni ishara ya maisha bora kwa kila mtanzania
 
Tatizo sio trafic light wala polisi...tatizo ni junctions hizo.... kungekuwa na flyovers foleni ungeionea kwenye movies tu
 
Kuna junctions zinahitaji marekebisho! Tee juction ni very poor design! Mfano juction ya ubungo mabibo external magari yanakinzana! Very poor design hata police tunawalaumu bure
 
Sasa ni saa11:30 alfajiri na tayari foleni kama kawaida TAZARA. Tatizo kubwa ni junction. Kinachotokea licha ya kutokuwepo kwa flyovers ni magari yasiyohusika kukaa kwenye foleni. Traffic control management haijaangaliwa vizuri. Nitatoa mfano. Mtu anaetoka Tabata kwenda Posta anaweza kupita barabara ya Mandela kupitia Buguruni(Uhuru road na au Nyerere road,achana na ile ya Tabata dampo-Kigogo)

Sasa akifika tu Matumbi anakutana na foleni, ambapo kama anataka kupitia njia ya Uhuru atasubiri sawa na yule anaetaka kupitia Njia ya Nyerere. Kumbe ingewezekana kabisa kwa huyu ambae haendi Through yaani Weaving/diverging angetumia service road na kupita pale Sheli ya Buguruni na akaenda zake. Kwa anaekumbuka vema, ilikua ukitoka Buguruni kwenda Tabata, hadi ufike Tabata junction ilikua kazi kubwa. Lakini tangu ruhusa ya kutumia service road kuanzia matumbi kwenda Tabata, foleni haipo kabisa. Jambo la kuzingatia hapa ni Kuboresha tabaka la lami kwa maeneo ambayo service road inatumika kama diverging road, na kamwe mtu anaenyoosha asiruhusiwe kupita kwenye service road, nakuambia itapubgyza foleni sana kama ilivyotokea Junction ya Tabata ukitokea Buguruni. Folen nyingi ni za kujitakia kabisa. Hakuna ulazima mtu atokae Temeke kwenda Gongo la Mboto kukaa muda mrefu wakati service road kuanzia Vetenary iko empty, ingeandaliwa namna bora tu kama ilivyofanyika pale Tabata, lakini iwe strictly tu kwa wale wanaoenda kushoto. Anaenyoosha akikamatwa apewe adhabu kali. Pale Tabata imeonyesha mafanikio makubwa!
 
Tatizo sio trafic light wala polisi...tatizo ni junctions hizo.... kungekuwa na flyovers foleni ungeionea kwenye movies tu

Kwanini inatokea siku nyingine tena ya kazi na in asubuhi/jioni kuna kuwa hakuna foleni kabisa utafikiri ni jumapili. Nazungumzia Mandela road hasa tazara/ubungo kwasababu ndio njia yangu ya kuelekea kazini.
Junction ndio chanzo ila askari wengi nao hawako smart ndio maana kuna hizi variation ya urefu wa msururu Wa magari.
 
Hali inazidi kuwa tete, hakuendeki si asubuhi si jioni wala mchana, hakuna nafuu. Vipi ni bora trafiki waziachie taa za barabarani zijiendeshe au wao ndio waamue magari gani yapite?!

Mkuu foleni wewe unaitaka mwenyewe. Panga muda wako wa kufanya mambo kamwe hutapata kukumbana na foleni. Mathalani unatakiwa kwenda ofisini asubuhi ukiwahi unakutana na wote wanataka kuwahi ila ukichelewa utawahi kufika maana foleni itakuwa imepungua.hapa Mimi nasubiri ifike saa moja nitoke mbezi ya kimara niende posta natumaini saa mbili nitakuwa nimefika.
 
Tatizo ni Polisi,kwa nini hawa achii taa zikaongoza magari,Polisi ni binadamu wakati mwingine wanajisahau na kusababisha msongamano mkubwa wa magari,cha kufanya ni kuwezesha traffic lights kuwa programmable ili Traffic Polisi akiona msongamano wa magari umezidi anakwenda kwenye taa za kuongozea na ku set manually enough time ya kuruhusu magari kila upande say robo saa au nusu saa kutegemea ukubwa wa msongamano.

Alternatively waweke barabarani sensors karibu na traffic lights ambazo zitawezesha taa kujirekebisha zenyewe kwa kuruhusu barabara yenye msongamano mkubwa wa magari yapite kwa muda mrefu kuliko kule kwenye msongamano mdogo.
 
Kwa kasi ya muheshimiwa jpm basi mpaka january barabara zitakuwa nyeupe, foleni itabaki historia, magari mengi yatapaki majumbani. No wese
 
Tatizo miundo mbinu haisapoti,mazingira ya uendeshaji hivyo vyombo bila ujanja ujanja
 
Vyombo vya usafir ni vingi sana ukilinganisha na ukubwa wa mji, uwingi huo unatokana na idadi kubwa ya watu kuishi katika mji huo mdogo na wengi wao wanafanyakazi katikati ya jiji. Ili foleni zipungue hakuna budi kuwezesha fursa za kutosha mikoani ili kuwe na uwiano unaofaa wa watu katika miji yetu.
 
Back
Top Bottom