Foleni Dar: Tatizo ni traffic light au Polisi?

Foleni Dar: Tatizo ni traffic light au Polisi?

Duniani kote, hususan kwa wenzetu waliotutangulia kiuchumi na kwenye magari mengi, usafiri wa treni ndio ulioonyesha matokeo chanya. Matumizi ya usafiri wa treni unapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya usafiri binafsi. Sio kwamba watu wanapenda kutumia gharama kubwa ya kuendesha magari yao binafsi bali usafiri tulionao wa daladala hauna staha, ni wa kero na kuibiwa juu na vibaka.

Binafsi, tatizo la foleni kwa mapana yake halitokani na polisi bali miundombinu yetu imezidiwa. Ukienda Posta ama Kariakoo ukiwa na gari binafsi tatizo lingine utakalokumbana nalo ni sehemu ya parking. Hivyo, tukijenga flyovers, say, Tazara, Chang'ombe, Ubungo, nk tutasaidia flow ya magari kuwa kubwa. Swali ni je, huko yanakoelekea kumeandaliwa kupokea magari kwa wingi?

Nadhani strategy ambayo itasaidia ni kuja na mkakati wa usafiri wa umma ambao ni bora, utakaovutia hata wenye magari kupaki magari yao majumbani. Jawabu ni usafiri wa treni. Huwa nasikitika mradi wa DART kama tungekuwa tuliamua kujenga reli basi jiji la Dar lingekuwa limepitiwa na reli kila kona kwa kuwa ujenzi wa reli ni gharama ndogo kuliko barabara. Hivyo tngekuwa tumefanikiwa kutatua kero ya foleni kwa kiasi kikubwa, kama si kuimaliza kabisa.




Tatizo ni Polisi,kwa nini hawa achii taa zikaongoza magari,Polisi ni binadamu wakati mwingine wanajisahau na kusababisha msongamano mkubwa wa magari,cha kufanya ni kuwezesha traffic lights kuwa programmable ili Traffic Polisi akiona msongamano wa magari umezidi anakwenda kwenye taa za kuongozea na ku set manually enough time ya kuruhusu magari kila upande say robo saa au nusu saa kutegemea ukubwa wa msongamano.

Alternatively waweke barabarani sensors karibu na traffic lights ambazo zitawezesha taa kujirekebisha zenyewe kwa kuruhusu barabara yenye msongamano mkubwa wa magari yapite kwa muda mrefu kuliko kule kwenye msongamano mdogo.
 
nadhani huwa ni flow ya magari...kuna kipindi Fulani kuna barabara zinakuwa na magari mengi hivyo kuhitaji huduma ya trafiki...nina fikiri ndo sababu!

Umesema vyema ndugu. Kama sio peak time, traffic light zinafaa lakini wakati wa peak, traffic right hazifai kwani zenyewe zina allocate muda ule ule kwa kila direction wakati direction nyingine kwa wakati huo hazina magari mengi. Traffic uwa wanaingilia has baada ya kupokea taarifa kwamba upande Fulani wa barabara foleni imekuwa ni ndefu sana, hivyo anaingilia kuokoa jahazi. Kimbembe ni pale traffic kwa makusudi anapoamua kuvuta magari ya upande mmoja ili mshikaji wake apite kwanza halafu ndio haki iendelee kutendeka.
 
Huu mji yaani hata ukiwa na gari kazi buree kabisa!ni afadhari kukamata pikipiki tu! Jana natoka ukonga asubuhi kwenda mwenge nimetumia karibu masaa matatu, tena hapo ni baada ya kuamua na kuchukua boda boda.
Hii kero itafutiwe ufumbuzi.
Miundo mbinu na mipango haikodhi.
 
Kwanini inatokea siku nyingine tena ya kazi na in asubuhi/jioni kuna kuwa hakuna foleni kabisa utafikiri ni jumapili. Nazungumzia Mandela road hasa tazara/ubungo kwasababu ndio njia yangu ya kuelekea kazini.
Junction ndio chanzo ila askari wengi nao hawako smart ndio maana kuna hizi variation ya urefu wa msururu Wa magari.

Mimi natumia barabara hii mwaka wa saba huu kila siku. Ukiona hivyo ujue pale TAZARA taa ndio zinaongoza magari. Mimi naona ni makosa makubwa sana kuwaachia askari kufanya maamuzi ya ku manage traffic flow. Hivi wataalamu wa chuo cha usafirishaji wako wapi watapatie alternative way au angalau watuthibitishie kuwa mfumo wa sasa ndio bora kuliko mwingine.

Kuna haja ya wataalamu wa social science na human behavior kufanya utafiti traffic police wanafaidika na nini kuongoza magari. Maana haiwezekani siku ya Jumapili saa moja asubuhi unamkuta trafiki anaongoza magari wakati hakuna magari mengi na taa zinafanya kazi. Au unakuta mchana wa jua kali au mvua inanyesha unaona na taa zinafanya kazi lakini trafiki yupo tu kuongoza magari

Lazima mkuna material au psychological benefit wanapata sio bure...............
 
Umesema vyema ndugu. Kama sio peak time, traffic light zinafaa lakini wakati wa peak, traffic right hazifai kwani zenyewe zina allocate muda ule ule kwa kila direction wakati direction nyingine kwa wakati huo hazina magari mengi. Traffic uwa wanaingilia has baada ya kupokea taarifa kwamba upande Fulani wa barabara foleni imekuwa ni ndefu sana, hivyo anaingilia kuokoa jahazi. Kimbembe ni pale traffic kwa makusudi anapoamua kuvuta magari ya upande mmoja ili mshikaji wake apite kwanza halafu ndio haki iendelee kutendeka.

Hii ni kweli kama kuna an uneven distribution ya magari...lakini kwa hivi sasa DSM njia zote zina magari mengi. Chukulia pale TAZARA......magari toka njia zote ni mengi sasa unajifariji kwa kuvuta muda mrefu ya kutoka mjini lakini unaongeza foleni ya bandarini au toka Tabata.

After all saikolojia ya foleni inaendana sana na taa kuongoza magari maana angalau unasogea kidogokidogo husikii maumivu sana kama kugandishwa dakika 45
 
Trafiki ni zaidi ya taa kusababisha folen

Mafikiri wanapigaga madili na watu wa boda boda, yaani, oya!! Ebu stopisha hii kitu tupige hela.
Teh teh teh!
Binafsi nafikiri flyover zingepunguza sana foleni! Mfano ubungo, hakutakuwa na haja ya mtu anayeenda mwenge asubirishwe na mabasi ya mkoani au ma magari yanayotoka/ yanayoenda kimara.
Pia mipango iboreshwe!
 
wale matrafki huwa wanapigiwa simu na mademu zao kuwa wanapita hivyo kuamua kuvuta magari ya upande mmoja ali baby awahi home!
 
Tatizo Kubwa ni Madereva ! Kila Mmoja Anaharaka !
Inatakiwa Elimu itolewe Kwa Madereva Na Watumiaji wengine wa Barabarani!
Unakuta Dereva Anaona Kabisa Kuwa Hawezi kwenda Mbele kuna foleni lakini atalazimisha Na Matokeo yake Anafunga njia Kabisa !
Mfano Kuna Makutano ya njia Nne Taa imekurusu upite lakini unapokwenda Gari zimeshonana Na huwezi kwenda Huna Sababu ya kusogea! Lakini unakuta Dereva Analazimisha Kwenda Matokeo yake Anafunga njia Na Gari Kutoka njia Zote 4 Zinasimama ! Anakuja mwingine Anatanua kushoto! Mwingine Analazimisha kupita Kulia ! Matokeo yake njia Zinafungika !
Ushauri Kwa Mtazamo wangu Ni Elimu kwa Madereva, Sheria Zifuatwe Na ukifunga/Ukiblock njia Kwa Uzembe upigwe Fine Kubwa Tu !
 
Hali inazidi kuwa tete, hakuendeki si asubuhi si jioni wala mchana, hakuna nafuu. Vipi ni bora trafiki waziachie taa za barabarani zijiendeshe au wao ndio waamue magari gani yapite?!

Tatizo ni kila mtanzania anataka kuishi dar, na kuacha maeneo mengine yakiwa wazi, ndo maana tumemwomba mheshimiwa rais ahamishie serikali dodoma Utaona kama jam itakuwepo
 
Tatizo madereva wengine wanaendesha magari kwa mwendo kama msafara wa harusi huku wanashangaa majengo ya Mji wa Dar... hahahaaaa!!


Kama foleni imekukera rudi kwenu kijijini ulikotoka kusikokuwa na foleni..
 
Dar haijafurika hata kidogo. Ila
1. Mipango miji ya hovyo
2. Hakuna njia mbadala matokeo yake woote inabidi mjirundike njia kuu
3. Baadhi ya barabara kugeuzwa parking hivyo huchangia foleni
4. Barabara zetu mbovu huchangia foleni
5. Barabara nyembamba(hazina tofauti na chochoro) na bado zimegeuzwa parking hata wenda kwa kiguu hawana pa kupita
6. Kukosekana kwa flyovers nayo huleta majanga...kwenye hili trafic watalaumiwa buuureeee

flyover zijengwe Dodoma. Dar kumeshafurika.
 
Ile kazi ya polisi usalama barabarani kucmama badala ya taa huwa hata wao hawaipendi na ikifika zamu yake utamwona anavyokuwa mpole. Ile ni kaz ngumu sana wadau.

MATATIZO:
1. Barabara zetu sio za kisasa.
2. Askari analazimika kukaa barabaran asubuh na jioni ili kuruhusu zaidi magari ya upande mmoja wakat wa kwenda asubuh na wakati wa kurud jion. Hapo inahitajika ballancing ili kama ni jion basi yanayotoka yawe mengi zaid kuliko yanayoingia na vile vile kwa asubuhi.
3. TIMING LIGHT SETTING.
Waziseti zile taa ili Mandela Road ikiruhusu pale Tazara basi Buguruni sheli iruhusu, Tabata iruhusu na Ubungo iruhusu. Hata hvy hili c jambo rahisi linahitaji utafit wa kihesabu ulio shiba.

Ili folen ipungue waweke flying overs na kupanua barabara, hii ndio suluhu.
 
Hili jiji mipango yake ilikuwa ovyo baada ya uhuru
 
Tatizo la foleni ni miundombinu tu ndio.
✅Njia moja kwenda posta,tegeta,ubungo...Yaani ukitaka kwenda hayo maeneo lazima upige njia moja tu no alternative roads.

✅Njia chache kwenye barabara zetu,waongeze njia @ lst ziwe tatu kwenda tatu kurudi.
 
Back
Top Bottom