Flyover TAZARA Imetengewa Bajeti - Magufuli

Mkuu hapo kwenye Rangi unamaana gani? Miaka 50 ndio wanayakumbuka hayo?

Mkuu wangu, serikali inatekeleza mambo mbali mbali kulingana na mahitaji. kwa sasa jambo hili ni muhimu sana, ili kusiwe na visingizio vya kutoka kazini mapema kusingiia foleni.
 

naona umeamua kuolewa na magufuli, hivi unajua flyover ni kitu gani? Ulishawahi kiona fyover? Tanzania hakuna barabara halafu unaongelea flyover, huu ni wendawazimu
 

thank for the lecture, you have taken me back to my highway engineering course, the info you have provided should act as a complete idiot guide to every ccm fool out there.
 
Kwanini tunasifia watu kwa kutimiza wajibu wao? Si wanakusanya kodi ndio kazi yake. Suala ni vipi unatumia kodi. Unaweza kukusanya kodi ukatengeneza fly over moja na mwingine akakusanya kodi kiwango kile kile angatengeneza tano. Sidhani kama kuna mtu aliwahi kusema serikali iliopo haijafanya kitu tatizo ni bado haitoshi tungeweza kufanya vizuri zaidi
 
Nimekumbuka hivi daraja la kigamboni serikali si nayo inatakiwa kuchangia? Wasije ua penshion fund
 
Ubungo vipi? mbona ubungo ndio pana congestion ya kutisha kuliko Tazara? au tunataka kuonyesha wageni wanaopita hapo toka Airport kwamba nasi tuna FLyover?

umesahau kuwa ile ipo busy na safar za kumpeleka mzee uwanja wa ndege????
Jamaniiiiii
 

Viongozi wetu dhaifu, wameshindwa kukarabati barabara za chini wataweza hizo zinazopita hewani? Nia yao ni kutaka kuwaua wananchi kwa ajali za juu hewani kwani hizi ajali za bara bara za chini hazijawaridhisha!!!
 
Mtoa mada ebu nyosha maelezo fedha zimetengwa for what?
upembuzi yakinifu,ujenzi etc
Na kumbuka kutenga sio kutekeleza?
Ikitokea dhahma katikati apo CCM wanaweza zikwapua mwishowe tutakuja ambaiwa donors hawakutoa ela zote!
 
Hongera sana Waziri Magufuri ni mpango mzuri wa kuondoa foleni kwenye Jiji letu la Dar es Salaam, naona kazi zinafanyika ukipita barabara ya Morogoro unakutana na Strabag Kampuni kutoka Ujerumani wanatengeneza barabara za mabasi yaendayo kasi.

Ritz,

Wenyewe wanasema mabasi yaendayo haraka sio kasi mazee.
 
Hawa nao hawaishi nyimbo na mipango miingiii! Wenzetu Kenya wako very serious na hii issue!
 
Mimi sina tatizo na flyover. Ila naamini foleni nyingi huku mjini tatizo lake ni miundombini ya zamani ambayo haitoshelezi. Wanajamii, mtu huitaji kuwa professor kuelewa kuwa fly over TAZARA au sehemu nyinginge yeyote hapa mjini kwa sasa wakati njia yote kuelekea Ubungo imejaa magari na wakati mwingine hayatembei kwa zaidi ya nusu saa haitasaidia kitu. Na mtu haitaji kuwa mpiga ramli kujua kuwa foleni itahamia kwenye hiyo flyover.

Kwa mawazo yangu, na mifano ya nchi za ulaya ambazo nimewahi kutembelea japo chache, flyover zinakuwa na maana pale kunapokuwa na njia ya kutokea ambayo iko wazi. Ili flyover mahali kama Ubungo iwe na Ufanisi, ni lazima njia ya kuelekea Kibaha iwe inapitika kwa urahisi. Kwa maneno mengine, kuanzia Ubungo kwenda Chalinze angalau kuwe na njia mbili kwenda na kurudi na baada ya hapo ndio tuanze kufikiria mpango wa kupita juu.

Vivyo hivyo kwa upande wa TAZARA, ukianzia pale TAZARA kuelekea airport kuna foleni, watakaokuwa kwenye fly over watatokea wapi?

Nawahakikishieni, flyover yoyote kwa sasa itakuwa sehemu ya watu kwenda kushanga kwa sasa na magari yetu mengi huko barabarani yalivyokuwa mabovu hasa yale ya kubebea taka sijui yatakwamuliwa na nini yatakapozimikiwa huko hewani! Mimi simo, hayo yalikuwa ni mawazo tu.
 
Wana JF naomba mwenye hiyo budget aitupie humu kwani wengine leo hatukuisikia. Asanteni
 
Paukwa! Pakawa!! Nyie hizo story za magufuli hamjazizoea bado? Huyu mtu ni janga la taifa
 
Uongo wa Magufuli unaujua wewe? Kwa taarifa yako hata kwenye huo mradi wa mabasi ya kasi Kimara -Kivukoni hakuna design ya flyover hata moja. Mr dhaifu wakati wa kampeni alidanganya eti kutakuwa na barabara za juu, leo ije kuwa Tazara,kama unabisha nenda ofisi za DART,Starabag au Smec pale Ubungo plaza wanaofanya hiyo project ya Kimara- Kivukoni,check design drawings hakuna barabara za juu kwa maana ya fly over.
 
naoma mwenye kumbukumbu atukumbushe kama hii kitu hata mwaka jana haikutengewa bajeti???
 
Wasiwasi wangu ni kwamba magari yataharibika huko juu na kuleta foleni zaidi ya kawaida

Wabongo hawahawa ama wengine
 

Kwahiyo unataka waanze kujenga kote tu kama matahira? Sio kitu cha haraka haraka kama unavyodhani! Wangeweka hela nyingi bado ungelalamika "yaani wanachezea hela kuiga miundo mbinu ya kizungu tu! Bara bara hizi hazitoshi?". Tujifuze kuelewa.
 
Kwahiyo unataka waanze kujenga kote tu kama matahira? Sio kitu cha haraka haraka kama unavyodhani! Wangeweka hela nyingi bado ungelalamika "yaani wanachezea hela kuiga miundo mbinu ya kizungu tu! Bara bara hizi hazitoshi?". Tujifuze kuelewa.
Acha kutetea udhaifu wa serikali, Miaka yote hamsini ambayo wametawala nchi hii, wangekuwa wameshazikamilisha hizo flyovers za Dar endapo wangekuwa ni visionary. lakini kwasababu ya kutoona mbele, walifikiri magari yataendelea kubaki idadi ileile ya mwaka 1961. Kuwa na serikali isiyoona mbele ni shida tupu. Kwani nchi kama Botwana zilizoendelea kimiundombinu zilifanyaje? Serikali Dhaifu kabisa ya Chama cha mapinduzi. Fedha za maendeleo wanazo kidogo lakini za kuiba na kukimbizia kwenye mabenki ya nje wanazo nyingi. Endelea kuwaunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…