Ni kweli mkuu lakini tutakwa tumepunguza foleni kidogo maana hata Tazara kuna upande wanapita juu bila kusimama na kuna upande lazima wasimameMchoro mzuri sana unafanana na Sinsen Interchange Oslo, Norway.
Ila sasa huwa kuna tatizo la foleni kwenye huo mzunguko hapo kati.. hasa kwa wanaotoka mwenge kwenda magomeni.. kusubiriana na wale wanaotoka tabata kwenda magomeni..
Huu mchoro ungefaa sana Tazara maana traffic kubwa huwa ni airport-mjini na ubungo-kurasini.
Nimekukubali Mkuu. Haijalishi Kama umekopi sehemu au umechora mwenyeweMagari yanayotokea barabara ya Mandela (kutoka Buguruni Tabata na kwingineko ) kuelekea mjini na Ubungo Terminal yatapita kwenye mzunguko (round about) ambapo ukitaka kurudi mandela unaweza
Ni kweli ila hawatabomoa kwa kiasi kikubwa kama ile flyover ya mwanzo hii watabomoa kidogo , na hicho ndoo Serikali yetu haipendi kuwalipa fidia watu.Mkuu, naomba nikuchallenge kidogo...
Ulianza kujua vipimo vya eneo husika ndo ukachora plan au umeanza kuchora kwanza ndo ukaipa jina la mahali?
Na je umefikiria kuhusu ukubwa wa eneo husika?
Kwa haraka inaonekana Songas wahamishe mashine zao zote (200 MW) na upande wa pili Ubungo Main substation ihame....
Bomba la gesi pia linalokatiza hapo?
Gharama ya project?
Vipaumbele?
Mwisho nakupongeza kwa ubunifu mzuri.
Huu ndoo ulikuwa kwenye mchakatoSafi mkuu, kwani mchoro uliopo kwenye project uko vipi.
basi hata songas haponi, maana main conection ya bomba ipo hapo GETI LA KWANZA kutoka mataa, sasa gharama ya kuhamisha ni balaa hapo,lazima fidia itembee tu hakuna kwa kukwepeaHii fly over yako ni hatari kwa jengo la TANESCO, Ubungo...