Flying cars ndiyo suluhisho letu

Flying cars ndiyo suluhisho letu

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,894
Reaction score
7,111
Nashauri tufanye uamuzi kama tuliofanya kwenye huduma za simu, kwamba tuziruke awamu za maendeleo (bypass stages of development) kwa kuruhusu Tanzania iwe sehemu ya majaribio ya teknolojia magari ya kuruka juu (flying cars). Tayari miji kadhaa duniani imekubali kuwa sehemu ya majaribio hayo, ikiwemo Dubai na Los Angeles. Tunaweza hata kuchagua mikoa michache kwa majaribio.

Wengi mnajua jinsi TTCL walivyoshindwa kupeleka huduma za simu za ndani (land lines), hadi kwa bahati nzuri teknolojia ya simu za mikononi ilipokuwa nafuu na tulipoamua kuikubali miaka ya mwishoni kwa 90, mapinduzi makubwa yamekuja.

Kwa kukubali teknolojia ya cellphones, imefika wakati hata baadhi ya huduma, mfano za mobile money zinaanzia/kusambaa huku kwetu kabla hata ya huko walikoendelea.

Ni wazi kwenye barabara bado tupo nyuma saaana. Tukiruhusu hii technolojia, siyo tu tutaelekeza fedha kwenye mambo mengine mfano elimu na afya, lakini upana wa athari zake (multiplier effect) zake ni kubwa kama tulivyoshuhudia kwenye mobile communication, mfano ajira, biashara za mawakala, mawasiliano bora hadi vijijini, nk.

Bado tutaendelea kujenga barabara (kama ambavyo mpaka sasa bado unaweza kuomba na kuunganishiwa land line) lakini tutakuwa tumepunguza shinikizo kwenye bajeti zetu huku tukipata maendeleo ya haraka.
 
Wazo zuri ila maelezo yako hayajitoshelezi, hayajakaa kitaalamu zaidi.
 
Ni hivi....kuna ushindani mkubwa unaendelea sasa hivi duniani katika teknolojia hii. Tunachoweza kufanya ni mamlaka zinazohusika na mambo ya usafiri wa nchi kavu zinaweza ingia ubia na makampuni hayo. Tunawaambia mahitaji yetu (labda badala ya vigali vidogo vya kukaa mtu mmoja kama ambavyo wanafanya sasa, tunawachallenge watutengenezee vya kuchukua watu kama 20 kwa wakati mmoja). Faida kwao itakuwa wana sehemu ya kutest teknolojia zao, sisi tunafaidika na usafiri ulio bora na wa haraka zaidi.

Hizi gari zinaruka na kutua vertically kwa hiyo hauhitaji runway kama ya uwanja wa ndege. Tunaweza tenga sehemu maalumu labda kwa usalama na ufanisi zaidi, kwa ajili ya kutua na kuruka. Nadhani pembezoni kwa vituo vikubwa vilivyopo vya mabasi itafaa zaidi.
 
Wazo zuri ila kwa tanzania yetu bado sana

hivi si nasikia watu wameanza kulalamika kuhusu mabasi ya mwendokasi !!
 
Wazo zuri ila kwa tanzania yetu bado sana

hivi si nasikia watu wameanza kulalamika kuhusu mabasi ya mwendokasi !!

Mwendokasi tatizo kubwa ni mabasi machache kuwekwa barabarani pungufu ya mahitaji. Vilevile kupiga marufuku daladala zinazoshare route na mabasi hayo kwa hiyo wasafiri wanakuwa hawana jinsi.

Flying cars hata kesho zinaweza kuanza kazi Tanzania. Zinatumia GPS system kujua destination zake. Nadhani tupo tayari kwa hili. Kama nilivyosema, tunaweza anzia mikoa michache wakati tunapima usalama na ufanisi wake.
 
Elon Musk, CEO wa Tesla na Space X na chairman wa AI haamini katika flying cars kama ndiyo solution ya foleni ila yeye anaamini solution iko underground ndiyo maana ana project yake ya kusafiri kwenye undeground tube kwa speed ya zaid km 500hr
 
Back
Top Bottom