Flavius na utamaduni wa Kigiriki

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
Flavius,yule Myahudi wa Kigiriki,alikuwa haruhusiwi kuingia Hekaluni,kwa vile alikuwa hajatahiriwa na hajabatizwa;pia kwa vile alikuwa mpenzi mkubwa wa vitu vizuri katika sanaa na uhunzi[sculpture],nyumba yake aliyokuwa anaishi alipokuwa anahiji Jersalem,ilikuwa nyumba nzuri. Nyumba hii ilikuwa imepambwa na tunu za thamani alizozikusanya hapa na pale katika safari zake za dunia.Alipofikiria kwanza kuhusu kumualika Yesu kuja nyumbani kwake,alihofu kwamba Mwalimu atapinga kuja kuviona hivi vitu.Lakini Flavius alifurahi na kushangazwa Yesu alipoingia nyumbani kwake kwamba,badala ya kumgombeza kwa ajili ya haya masanamu yaliyojaa nyumbani kwake,alionyesha kupendezwa na vitu vyote,na aliuliza maswali mengi wakati Flavius alipompeleka chumba baada ya chumba,kumuonyesha zile sanamu alizokuwa anazipenda kuliko zote.

Mwalimu aliona kwamba mwenyeji wake alishangazwa kuona kwamba ana urafiki na sanaa,kwa hiyo alipomaliza kuvikagua vile vitu vyote,Yesu akasema,''Kwa sababu unaupenda uzuri uliopo ndani ya vitu vilivyoumbwa na Baba yangu na kuundwa na mikono ya kisanaa ya binadamu,kwa nini utegemee kugombezwa? Kwa vile Mose alijaribu kupiga vita ushirikina na kuabudu muingu ya uongo ,kwa nini watu wote wachukizwe na uundwaji wa vitu vizuri. Nakuambia,Flavius,watoto wa Mose hawakumuelewa,na sasa hata hili katazo lake la kukataa mifano ya kitu chochote mbinguni au duniani,limekuwa kama ni mungu wa uongo anayeabudiwa. Lakini hata kama Mose aliwafundisha mambo hayo watu katika siku zile za giza,hiyo inahusu vipi siku hizi ambapo Baba wa mbinguni anafunuliwa kama Kiongozi wa Roho juu ya kila kitu? Na,Flavius,nasema kwamba katika ufalme unaokuja hawatafundisha tena,''Usiabudu hiki na usiabudu kile,'' hawatajishughulisha na amri za kuzuia hiki na kujihadhari usifanye kile,ila wote watashughulika na wajibu moja mkubwa. Na huu wajibu unaelezwa katika hesima mbili anazotunukiwa mtu;kumuabudu kwa dhati Muumba wa vyote,Baba wa Paradiso,na kumtumkia kwa upendo binadamu mwenzako. Ukimpenda jirani yako unavyojipenda mwenyewe,unajua kwa hakika kwamba wewe ni mtoto wa Mungu.

''Katika zama ambazo Baba yangu hakueleweka vizuri,Mose alikuwa ana haki katika juhudi zake za kupinga ushirikina[kuabudu sanamu,idolatry],lakini katika siku zijazo Baba atakuwa amefunuliwa katika maisha ya Mwana;na ufunuo huu wa Mungu utafanya iwe milele sio lazima kumchanganya Baba Muumba na sanamu za mawe au sanamu za dhahabu au shaba. Kuanzia hapo,watu wenye akili wanaweza kufurahia sanaa bila kuchanganya kupenda vitu vizuri na kumuabudu na kumtumikia Baba wa Paradiso,Mungu wa vitu vyote na viumbe vyote.''

Flavius aliamini yote ambayo Yesu alimfundisha. Siku iliyofuata alienda Bethany kuvuka Jordan na alibatizwa na wafuasi wa Yohana. Na hii ilikuwa kwa sababu wafuasi wa Yesu walikuwa bado hawajaanza kubatiza waumini.
Flavius aliporudi Jerusalem,alimfanyia Yesu sherehe kubwa na akawaalika rafiki zake sitini. Na wengi wa hawa wageni pia waliamini katika ujumbe wa ufalme unaokuja..

[Wakati tunaambiwa hapa kwamba Yesu,apparently alikuwa rafiki wa sanaa,tukumbuke hizi habari tulizozisikia leo kwamba sanamu ya Yesu kubwa,yenye urefu labda wa mita ishirini,imepigwa radi na kuungua huko Ohio,Marekani. Insurance Companies wamesema kwamba 'it is an act of God.'' Ile Diocese ambapo ile sanamu ilikuwepo,wamesema wataijenga tena hiyo sanamu.]
 
Back
Top Bottom