GE2025 Flatei Massay awekewa pingamizi Ubunge Mbulu

GE2025 Flatei Massay awekewa pingamizi Ubunge Mbulu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Baadhi ya wanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Mbulu-Vijijini, Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara, wamepeleka pingamizi la kumpinga Mgombea wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya chama hicho Flatei Gregory kwenye ofisi ya msimamuzi wa uchaguzi jimbo la Mbulu vijijini kwa madai ya kuwa mgombea huyo hajafuata utaratibu halali wa chama hicho.

1756464510252.png

Wakitoa hoja zao wanachama hao wamesema hawajaridhishwa na utaratibu wa chama chao kumpokea na hatimaye kumpitisha kuwa mgombea wa Jimbo la Mbulu Vijijini bila kufuata utaratibu wa kikatiba.

Msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo hilo Joseph Elia amesema amepokea mapingamizi hayo yaliyofikishwa ofisini hapo na kwamba amewaelekeza mapingamizi hayo yapelekwe ndani ya chama chao.

Ikumbukwe Flatei Gregory alikuwa Mbunge wa Mbulu vijijini kupitia CCM alijizolea umaarufu baada ya kupiga sarakasi bungeni na baada ya jina lake kutorudi akatimkia ACT na kuchukua fomu ya ubunge.
 
Baadhi ya wanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Mbulu-Vijijini, Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara, wamefikisha malalamiko yao katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, wakipinga uteuzi wa mgombea ubunge kupitia chama hicho, Flatei Gregory Massay, wakidai kuwa mchakato huo haukufuata taratibu halali za chama.

Wakitoa malalamiko yao mara baada ya kufika katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wanachama hao wamedai kutoridhishwa na namna jina la mgombea huyo lilivyopitishwa bila kuwashirikisha wanachama wala kufuata utaratibu wa ndani ya chama, huku wakisisitiza demokrasia ya kweli inapaswa kuzingatiwa katika kila hatua ya uchaguzi.

Soma pia

Aidha wananchama hao Wameiomba Tume huru ya Uchaguzi (NEC) na uongozi wa kitaifa wa ACT Wazalendo kuchunguza suala hilo kwa kina na kuhakikisha haki inatendeka ili kuepusha migogoro ya kisiasa ambayo inaweza kudhoofisha chama chao katika uchaguzi mkuu ujao.

Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo Hilo Joseph Elia amesema Ofisi yake Haina mamlaka ya kutolea maamuzi suala hilo licha ya kupokea nakala za madai ya wanachama wa ACT Wazalendo kuwa mgombea hakufata taratibu za uteuzi wa mgombea, nakuwataka wanachama hao kupeleka malalamiko yao Viongozi wa juu wa Chama chao.

Pia, amekiri kupokea pingamizi jingine kutoka CCM dhidi ya ACT-Wazalendo

Chanzo: CloudsTV
 
Baadhi ya wanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Mbulu-Vijijini, Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara, wamepeleka pingamizi la kumpinga Mgombea wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya chama hicho Flatei Gregory kwenye ofisi ya msimamuzi wa uchaguzi jimbo la Mbulu vijijini kwa madai ya kuwa mgombea huyo hajafuata utaratibu halali wa chama hicho.

View attachment 3457348

Wakitoa hoja zao wanachama hao wamesema hawajaridhishwa na utaratibu wa chama chao kumpokea na hatimaye kumpitisha kuwa mgombea wa Jimbo la Mbulu Vijijini bila kufuata utaratibu wa kikatiba.

Msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo hilo Joseph Elia amesema amepokea mapingamizi hayo yaliyofikishwa ofisini hapo na kwamba amewaelekeza mapingamizi hayo yapelekwe ndani ya chama chao.

Ikumbukwe Flatei Gregory alikuwa Mbunge wa Mbulu vijijini kupitia CCM alijizolea umaarufu baada ya kupiga sarakasi bungeni na baada ya jina lake kutorudi akatimkia ACT na kuchukua fomu ya ubunge.
CCM anapita bila kupingwa!

Mkiambiwa mfanye No Reforms No Elections mnakaza shingo!

Pambaneni na hali zenu sasa, sie ngoja tuendelee kusubiri Mwenyekiti wetu siku yake ya unyongwa hadi kufa ifike!
 
Hilo pingamizi la Mbulu hawatashinda. Flatei atapigiwa kura. Sema hatatangazwa maana mwenye kutangaza ni CCM.
 
Back
Top Bottom