Flagship Soundbars

Wakuu, hii Vizio M512a_h6 ni kisanga, inagonga balaa hadi nahisi father house atanifukuza nisije nikatia nyufa nyumba yake🔥🔥🙌🙌
Ndio ile hapo juu ya 1,600,00 aliyoonyesha mdau?
 
Anaposema frequency response ni mfano 100 hz anamaanisha nini?
Sauti inasafiri kwa njia ya mawimbi kama mawimbi ya bahari. Mawimbi hupanda na kushuka kwa hiyo kipimo cha mawimbi Hz inamaanisha ni mara ngapi mawimbi yanajirudia kwa kila sekunde.
Kwa hiyo mawimbi ya 100Hz maana yake ni kwamba yanapanda na kushuka mara 100 kwa kila sekunde.
Spika za sound system zinapimwa uwezo wake kwa frequency response yaani frequency zinazokufikia wewe masikioni ni kiasi gani.
Kadri frequency zinavyopungua ndio sauti inashuka(bass) na frequency zinavyopanda ndio sauti inapanda(treble). Kwa hiyo spika kubwa mfano subwoofer zinatoa sauti yenye mawimbi makubwa machache kwa sekunde na spika ndogo mfano tweeters zinatoa sauti ya mawimbi madogo sana mengi kwa sekunde.
 
Asante kwa ufafanuzi Mkuu
 
Mkuu unawaongeleaje hawa Hometech kwa upande wa sound bar?
CORAL
 
Mkuu unawaongeleaje hawa Hometech kwa upande wa sound bar?
CORAL
Soundbars za Hometech hazina tofauti na subwoofer za Hometech. Ukiangalia hata bei zinaendana. Huwezi kutarajia chochote cha ziada kwenye soundbar ya 250k au 300k. Hizo ni stereo systems za kawaida za kichina. Kama ukinunua utakachopata ni kile tu unachopata kwenye subwoofer za kichina.
 
Wacha nijipige niipate hata hiyo Vizio ya 680k kusupport flat screen ya ukubwa wa 55
 
Wacha nijipige niipate hata hiyo Vizio ya 680k kusupport flat screen ya ukubwa wa 55
ila wabongo mnapenda sifa sn eti kusupport 55 inch tv lengo tujue una tv ya 55 inch wkt unataka kununua sb ya lak 2 iyo ya lak 6 mpk ujipgepge aaahaahaaha.
 
Mi kwangu sjataka mambo mengi nlinunua active subwoofer ya AR-M10 ni 10 inch carpeted boom box, magnet 20 oz, voice coil kvs 1.5 ni 4 layers, frequency 40 to 200hz, 4omhs, sensitivity 90db/m.w. kisha nikanunua used receiver ya sony na twita 4 za mtumba nikafunga kaz ni hatari narudia tn ni hatari hzo sound bar zenu hzo za milion hazsogelei hapa.
 
Kiufupi walio sifia vizio wote ni wauzaji au hawajawahi kusikia sauti ya SONY, kiufupi vizio hana majabu yoyote ukibisha kunya ukalale vizio m elevate, hamna maajabu, frequency 40hz ndo inanzia, hapa nataka nikairudishe hata nibebe tv niwe nangalia porn grapy kuliko kusikia mziki wa kelele usio na maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…