Fixed deposit account vs Hati fungani, ipi ina faida zaidi?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
5,085
2,000
Habari wadau..

Naombeni msaada wa ushauri..

Nimepata mgao wa urithi kama milion 30 hivi.... sitaki kuzitumia now na nipo chuo bado nasoma.

Nafikiria kuziwekeza kwenye non risk investment....

Kwa mnaojua naombeni ushauri je hati fungani faida yake ikoje... na je inaizidi ya fixed deposit.. na faida yake unayopata je inakatwa kodi kwa kiasi gani??

Pia nina wazo ya kununua nyumba zinazopigwaga mnada na mabank na madalali... je changamoto zake zikoje??

Sitaki ushauri kuhusu biashara nyingine yoyote zaidi ya hayo maswali yangu.

Na bank ipi ina faida kubwa zaidi kuwekeza hizo hati fungani au fixed deposit
 
Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
7,619
2,000
Kanunue hisa Voda au Tigo, upige hela kijana. Anyways unahitaji kuwa makini katika hili asee.
 
sawe4u

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
976
1,000
Nunua nyumba utapat faid kuliko yote ulio taja

Viwanja pia ni non risk
 
dSamizi

Senior Member
Jan 2, 2016
106
225
Kanunue hisa voda au tigo, upige hela kijana. Anyways unahitaji kuwa makini katika hili asee.
Humtakii kheri! Hisa bongo? Very risk. Ushauri chukua FDR _Fixed deposit bila shaka Barclays wanarate nzuri au ufuatilie kwa bank zenye uhitaji na deposit acha hii inayopigiwa promo na JPM ina rate ndogo ajabu.
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
5,085
2,000
Thanks ila sitaki ushauri wa hisa ndugu... mi nataka hati fungani au fixed deposit au nyumba za mnada tu... sitoki nje ya hapo

Kanunue hisa voda au tigo, upige hela kijana. Anyways unahitaji kuwa makini katika hili asee.
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
5,085
2,000
Aante viwanja sitaki kwa sasa.. sababu ninacho cja urithi..

Hii hela nataka nije fanyia biashara nikimaliza chuo maana ajira hazieleweki..

So nataka niiwekeze kwa kuitunza na nipate passive income tu.. ndio maana naulizia hati fungani...

Viwanja ni non liquidity... unaweza ukawa na shida ukasema uuze fasta na mteja usimpate au akulalie bei ukala hasara... ndio maana sitaki viwanja...

Na vina drama sana mara umeuziwa eneo la wazi mara migogoro... hayo mawazo ya viwanja siyataki kabisa kwa umri huu nipo chuo.... niko makini sana na hela ya urithi maana wanasemaga inapotea potea tu... sitaki ipoteee hata senti

Nunua nyumba utapat faid kuliko yote ulio taja

Viwanja pia ni non risk
 
mputa

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
1,168
2,000
habari wadau..

naombeni msaada wa ushauri..

nimepata mgao wa urithi kama milion 30 hivi.... sitaki kuzitumia now na nipo chuo bado nasoma.

nafikiria kuziwekeza kwenye non risk investment....

kwa mnaojua naombeni ushauri je hati fungani faida yake ikoje... na je inaizidi ya fixed deposit.. na faida yake unayopata je inakatwa kodi kwa kiasi gani??

pia nina wazo ya kununua nyumba zinazopigwaga mnada na mabank na madalali... je changamoto zake zikoje??

sitaki ushauri kuhusu biashara nyingine yoyote zaidi ya hayo maswali yangu.

na bank ipi ina faida kubwa zaidi kuwekeza hizo hati fungani au fixed deposit

Kijana tumia sehemu ya hiyo fedha kuwekeza kwenye elimu, kama upo first degree unge opt kupata masters, then ukitoka huko unaanza maisha, ajira zipo cha msingi subira
 
GIUSEPPE

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
5,260
2,000
Hebu tafuta baa nzuri, kisha njoo na milioni kama mbili hivi za dharula, kisha tujadili kwa kina kuhusu hii ishu yako.
 
Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
7,619
2,000
Humtakii kheri! Hisa bongo? Very risk. Ushauri chukua FDR _Fixed deposit bila shaka Barclays wanarate nzuri au ufuatilie kwa bank zenye uhitaji na deposit acha hii inayopigiwa promo na JPM ina rate ndogo ajabu.
Asante mkuu kwa kunifumbua macho.
 
Hajto

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
4,054
2,000
habari wadau..

naombeni msaada wa ushauri..

nimepata mgao wa urithi kama milion 30 hivi.... sitaki kuzitumia now na nipo chuo bado nasoma.

nafikiria kuziwekeza kwenye non risk investment....

kwa mnaojua naombeni ushauri je hati fungani faida yake ikoje... na je inaizidi ya fixed deposit.. na faida yake unayopata je inakatwa kodi kwa kiasi gani??

pia nina wazo ya kununua nyumba zinazopigwaga mnada na mabank na madalali... je changamoto zake zikoje??

sitaki ushauri kuhusu biashara nyingine yoyote zaidi ya hayo maswali yangu.

na bank ipi ina faida kubwa zaidi kuwekeza hizo hati fungani au fixed deposit
Uzi wako nimeusoma na kuuelewa,vipi umeamua kuiwekeza kwenye nini iyo hela yako,nami nina kama robo tatu ya pesa yako nataka kuiwekeza
 
Uchira 1

JF-Expert Member
Oct 9, 2017
2,077
2,000
Mkuu bora ungeweka hati fungani maana kule kunafaida faida ni 100 asilimia pia inakuwa na faida zaidi ya fixed a/c maana huko fixed a/c wao wanazitumia katika biashara, ukihitaji hili kwa zaidi waone broker wa hati fungani kama SOLOMON brokers
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
5,085
2,000
mkuu bora ungeweka hati fungani maana kule kunafaida faida ni 100 asilimia pia inakuwa na faida zaidi ya fixed a/c maana huko fixed a/c wao wanazitumia katika biashara, ukihitaji hili kwa zaidi waone broker wa hati fungani kama SOLOMON brokers

Nimeweka fixed na rate sio mbaya. mambo ya hati fungani kuuza ngumu kuziuza ukiwa na dharura ya haraka.. fixed rahisi kuivunja.

Maana mimi target ni kununua nyumba kwenye mnada.. ya location inayopangishika kwa bei nzuri.
 
Uchira 1

JF-Expert Member
Oct 9, 2017
2,077
2,000
nimeweka fixed na rate sio mbaya. mambo ya hati fungani kuuza ngumu kuziuza ukiwa na dharura ya haraka.. fixed rahisi kuivunja

maana mimi target ni kununua nyumba kwenye mnada.. ya location inayopangishika kwa bei nzuri
Poa mkuu ila hiyo rate mbona kubwa sana?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom