Fixed deposit account vs Hati fungani, ipi ina faida zaidi?

nimeweka fixed na rate sio mbaya. mambo ya hati fungani kuuza ngumu kuziuza ukiwa na dharura ya haraka.. fixed rahisi kuivunja

maana mimi target ni kununua nyumba kwenye mnada.. ya location inayopangishika kwa bei nzuri
Na hao Access bank huwa nao naonaga baadhi ya wakopaji wao wakishindwagwa kulipa huuza nyumba za wadeni wao kwaiyo unaweza dili nao unaweza pata nyumba kwa bei rahisi
 
Walikuwa wananipa 13% per annum, mwaka huu wameishusha hadi 9% .. ninaangalia upepo . Kama wataishusha tena hela nazijengea tu.. maana niliziweka tu nikisubiri nipate muda wa kusimamia ujenz nizijengee
Utaratibu wao wa kulipa ukoje au ni after full maturity?..kila mwezi au baada ya miezi kadhaa..
 
i.e unakaa tu bila kulipwa hadi muda wa hiyo fixed deposit uishe(mfano two years/one year) ndo upewe hiyo 13pc?..

One year tu.. na hio 13% nilipewa mwaka wa kwanza tu.. kipindi kile walikuwa wanatafuta deposits kwa nguvu.. siku hizi wameshusha mpaka 9% per annum
 
One year tu.. na hio 13% nilipewa mwaka wa kwanza tu.. kipindi kile walikuwa wanatafuta deposits kwa nguvu.. siku hizi wameshusha mpaka 9% per annum
Swali langu ni kuwa hiyo 13pc ilikuwa inagawanywa na unalipwa kila mwezi au?
 
Swali langu ni kuwa hiyo 13pc ilikuwa inagawanywa na unalipwa kila mwezi au?

Hawalipi kila mwezi.. wanaiweka yote pamoja muda wa maturity ukifika... mfano ukiweka milioni 30 mwezi wa pili mwaka huu.. hulipwi chochote mpaka mwezi wa pili mwakani baada ya maturity unakuta wamekuwekea faida yao milion 3 na nusu.. account inakuwa na milion 33 na laki kazaa wakati wewe uliweka 30 kamili
 
Okay mkuu,nimekusoma
 
mkuu bora ungeweka hati fungani maana kule kunafaida faida ni 100 asilimia pia inakuwa na faida zaidi ya fixed a/c maana huko fixed a/c wao wanazitumia katika biashara, ukihitaji hili kwa zaidi waone broker wa hati fungani kama SOLOMON brokers
Mmmmhhh hatigungani faida asilimia mia? Sijawahi kusikia hii ndugu.
 
Walikuwa wananipa 13% per annum, then 11%, mwaka huu wameishusha hadi 9% .. ninaangalia upepo . Kama wataishusha tena hela nazijengea tu.. maana niliziweka tu nikisubiri nipate muda wa kusimamia ujenz nizijengee
Nimeona Yetu bank wanatoa 13% kwa mwaka, ila sina hakika ni kuanzia kiasi gani cha pesa wanatala uweke in the first place.

Pia niliona TPB bank wana 11% Ila ukiwekeza kwa miaka miwili, na unaanzia kuweka 5M na kuendelea.
 
Back
Top Bottom