Fisadi wa CUF huyu hapa...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fisadi wa CUF huyu hapa...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunango, Mar 6, 2009.

 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  MWENYEKITI wa Kamati ya Kuchunguza Mahesabu ya Fedha na Uchumi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), katika baraza la wawakilishi (PAC), Abass Juma Mhunzi ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa huo.

  Mhunzi, ambaye ni mwakilishi wa Jimbo la Chambani kwa tiketi ya CUF, alisema kuwa amemwandikia kiongozi wa upinzani kumjulisha kuhusu uamuzi wake kutokana na spika wa Baraza la Wawakilishi kutokuwepo kisiwani hapa kwa sasa.

  Mhunzi alirushiwa tuhuma nyingi, zikiwemo za kushindwa kununua magari ya wawakilishi wenzake baada ya kupewa karibu Sh72 milioni, lakini aliiambia Mwananchi jana kuwa magari hayo yamechelewa kufika na kwamba endapo hayatafika, yuko tayari kuuza mali zake kufidia fedha hizo ambazo alipewa na wajumbe wenzake.

  "Kuhusu wajumbe kunipa fedha kwa ajili ya kununulia magari, ni kweli na hayo magari yamechelewa. Yanakuja, lakini nikishindwa nitawalipa hata kwa kuuza mali zangu," alisema Mhunzi kwa njia ya simu alipozungumza na Mwananchi.

  Mhunzi amepata umaarufu mkubwa katika vikao vya baraza la wawakilishi kutokana na misimamo yake ya kutetea matumizi mabaya ya fedha za serikali.

  Katika kipindi chake cha uwakilishi, aliwahi kukumbana na matatizo mengi, likiwemo la kufikishana mahakamani na spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho baada ya kupewa adhabu ya kutohudhuria katika vikao kwa mwaka mzima.

  Adhabu hiyo ilitolewa baada ya Mhunzi kukataa kuomba radhi baraza kutokana na matamshi yake ya kusema bei za mafuta zinapangwa Ikulu.

  Katika kadhia hiyo Spika kificho alimuamuru Mhunzi kutohudhuria vikao kwa mwaka mzima, lakini mwakilishi huyo alipinga mahakamani na kushinda kesi na kulipwa haki yake kwa mwaka mzima.

  Mwaka jana, Mhunzi pia aliwataka wawakilishi wenzake wa kambi ya upinzani kubadili mwelekeo na kuitambua SMZ iliyo chini ya Rais Amani Abeid Karume.

  Mhunzi alisema kwamba anajua kwamba msimamo wake huo unaweza ukawa mwisho wake katika duru za kisiasa na kummaliza, lakini aliwataka wenzake kufahamu ukweli huo na kinachofanyika ni mbwembwe tu za kisiasa huku akisisitiza kuwa Rais Karume ndiye kiongozi wa nchi.

  Kujiuzulu kwa Mhunzi kumekuja siku chache baada ya baraza kuu la uongozi la chama chake cha CUF kumbwaga katika nafasi yake ya mjumbe wa baraza hilo. Uchaguzi huo ulifanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

  Awali jana, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Baraza la Wawakilishi zilizo Maisara mjini hapa, kiongozi wa kambi ya upinzani kwenye baraza la wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari alisema Mhunzi anashutumiwa kutumia fedha kifisadi na anadaiwa kuchota zaidi ya Sh200 millioni ambazo inadaiwa zilitengwa kwa ajili ya kununulia magari wajumbe wenzake.

  Bakari alisema mwakilishi huyo anadaiwa kuchukuwa fedha hizo kwa ajili ya kutafuta magari kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi na fedha za michango ya wajumbe wa baraza hilo wa kambi ya upinzani.

  Kiongozi huyo alisema Mhunzi alipewa kiasi cha Sh72 milioni tangu mwaka 2006 kwa ajili ya kununua magari ya wawakilishi wenzake, lakini hadi sasa ameshindwa kufanya kazi hiyo wala kurejesha fedha alizopewa.

  Alisema pia Mhunzi anadaiwa kushindwa kufikisha hundi 21 kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na nyingine 39 kwenye Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), ambazo ni kwa ajili ya shughuli hiyo.


  Kiongozi huyo amesema fedha hizo zilikuwa ni mchango wa wajumbe wa baraza la wawakilishi ambao walikuwa wakikatwa katika mishaha yao kwa ajili ya kusaidia matatizo mbali mbali yanayoweza kutokea katika kipindi chao chote cha shughuli za baraza hilo.

  Kiongozi huyo wa upinzani amesema kunatokana na kashfa kubwa zinazomkabili za upotevu wa mamilioni ya fedha pamoja na utapeli aliokuwa akiufanya kwa muda mrefu.

  Bakari alisema tayari Mhunzi ameshamuandikia barua Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho pamoja na kiongozi wa kambi ya upinzani kueleza uamuzi huo.

  "Ameniandikia kwa kuwa mimi ni kiongozi wa kambi ya upinzani na katika barua yake ameainisha baadhi ya vitisho, akisema anakusudia kunimaliza kisiasa," alisema Bakari ambaye ni mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni kisiwani Pemba.

  Pia katika barua yake Mwakilishi huyo ilisema anakusudia kufanya jambo kubwa kabisa ambalo litaitetemesha nchi na upinzani kupata pigo la mwaka.

  Source: Mwananchi
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  CUF walishasema kuwa wao ni chama kisafi kisicho na mambo ya ajabu walidiriki hata kukiponda CHADEMA wakasahau kuwa wao ni wapinzani kama CHADEMA. Cha ajabu wao wenyewe wameanza kumalizana wenyewe kwa wenyewe CHADEMA wako kimya.Kabla ya uchaguzi 2010 tutaona mengi.Na kama wameanza kuumbuana mapema wasahau kuongoza ZANZIBAR kamwe, wanawapa raha kina Makamba,Mkuchika,Tambwe na wenginewo wazidi kuongea. Kidumu chama safi na kikuu cha upinzani Bara na mwaka kesho kisiwani CHADEMAAAAAAAAAA.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Chadema wana ubavu wa kushinda huko visiwani?
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka nilieleza wakati alipotowa tamko la kutaka chama chake kiitambuwe SMZ kuwa huyu jamaa huyu alikuwa tayari na bifu na Chama chake na hivyo anatafuta sapoti ya CCM. Sasa imedhihirika na hilo tishio analosema ni kutaka kuhamia CCM lakini kwa historia ya CUF ajue tayari ameshajimaliza hata akibebwa na CCM kwani maadam ni Mpemba hana lake CCM.
  Kitabia huyu bwana sishangai sana kuwa fisadi kwani ni mtu mchafu sana akiwa mitaani. Yeye anajisifu kuwa ni kiboko ya wake za watu na mwenyewe anasema kuwa wamfata mwenyewe kwa vile waume zao ni m a h a n i si. Sasa jeuri hiyo anataka kuwafanyia wajumbe wenzake wa Baraza kwa kuona kuwa asifiwa sana. La kufanya ni kwa yeye kuacha malumbano na chama chake na aendelee kuigida serikali hadi uchaguzi ujao na wala asifanye makosa ya msabaha atabaki kuutangatanga kama anavyofanya Msabaha.
  Vipi ndugu yangu MWIBA mambo yako upenuni kwako unasemaje?
   
 5. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ok, follow the dots.....Kidumu chama safi na tawala bara na visiwani CCM

  Hii nifikra sahihi kabisa kuwa vyama vyote vya upinzani vinatokana na chama tawala CCM. Kwa hiyo basi Population=CCM, Sample=Chadema, CUF nk.

  Siasa za Tanzania = CCM


  CCM bado iko juu sana
   
  Last edited: Mar 7, 2009
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mwiba kaingia kwenye msitu wa karafuu!
   
 7. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwani CUF WALIANZAJE?
   
 8. K

  Kwaminchi Senior Member

  #8
  Mar 7, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Kwa jinsi mnavyoonyeshana vidole, naona pana hatari ya kutoboana macho. Mafisadi ni watu na watu wamo ndani ya CCM., CUF., Chadema na vyama vyote vingine. Mimi nafikiri Chama Cha Mafisadi ni kile ambacho watu wametuhumiwa ufisadi na wengine wamefikishwa mahakamani lakini bado wamekumbatiwa na vyama vyao.

  Kama huyu jamaa wa CUF ni fisadi na analazimika kuachia ngazi na kuhamia kwingine, basi
  CUF kinaendelea kuwa chama safi. Mpaka sasa hivi tuongeavyo, inaonekana CUF bado haijamkingia kifua.
   
 9. M

  Mzenji73 JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
 10. C

  Chuma JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  CUF safi kusafisha safu ya mashambulizi japo mnatakiwa muwahi kuwalipua mapema. Nimesoma barua ya Mh.Khamis very interesting ya vijembe vya kizenj...Najua CUF mmetumia all means and ways ya kumsaidia huyu mwakilishi, lkn naona sasa ni kumfikisha mahakamani...maana hii ya kumfukuzisha chama tu haitoshi....

  Hata kama akiama chama aende zake...Hili la watu kuchukua michango ya watu na kuingiza ktk biashara zao pia lipo ktk Taasisi za DINI, taasis za Umma, Mabenki yetu, viongozi huchukua na kuzizungusha, mambo yakienda mrama utasikia ohh pesa hazijaja....or mfadhili choroko choroko...!!!! Pesa za watu kama unataka uzitumie kwa matumizi yako binafsi yapasa uombe idhini kwa wahusika, wakikubali go ahead, wasipokubali kaa na Njaa zako...
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapana kijana hiyo niliiona tangu alipomtambua Karume na nikahisia kuwa kuna jambo amefanya sasa anasaka pa kujificha akifikiria kuwa CCM watamtetea ,tungoje hilo kubwa alilonalo maana kila anaetoka CUF huwa ana kabrasha la kusema,huyu bado hajaondoka ila amejiuzulu wadhifa flani ndani ya Baraza la Wawakilishi kama akina Lowasa ,ila bado dharuba ya Chama kutoka Chama Chake ,aidha atafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, weka akilini kuwa amewazika wenzake feza ,hapo kuna tofauti kidogo ,na kule kwenye Chama Cha Mfalme Sultani ,aidha amesema magari hayajafika ,siku hizi magari kwa kupeleka Zanzibar yanachukua siku kumi na tano tu na si zaidi ya hapo ,labda jamaa wawe wanapita kwenye mkondo mkubwa kuwakimbia wasomali.
  Alishindwa Mapalala aliekuwa na full back up ya CCM ,ngoja kwanza tuone akirudisha hiyo feza aliyowatapeli wenzake ,CUF wanasema kuwa kila aliemchafu basi hawezi kukaa ndani ya Chama ataibuka tu na kupigwa na chini au kuekwa pembeni ,unajua hawa akina Hiza mpaka sasa huenda wana agenda ya siri ya CUF sishangai ikiwa wanafanya ueFBI.
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana kwa kuwawekea JF hii barua ambayo inaonyesha ni jinsi gani Mwanasheria alivyoweza kuijibu na kumueleza Muwakilishi mkorofi ,moja kwa moja amemwambia ajiuzulu ,sasa huko Kwa Sultani CCM sijui wale matapeli wa miradi ya Serikali kama waliambiwa chochote zaidi ya kukumbatiwa ,huyu bila ya shaka yeyote kama hatajiuzulu atavuliwa uanachama moja kwa moja.

  Mwanasheria amegusia kifungu cha sheria kama kifuatavyo kama si kifungu basi ni maelezo ya kifungu fulani:-

  "Yule mtu anaeona kosa na akaficha au akanyamaza bila ya kutoa taarifa basi naye huwa mkosa sawasawa na yule alietenda kosa” Kikwete ana orodha kibao za kila aina ya mafisadi lakini amebania ,je anajua kubania kwake ni kosa la jinai ?
  Hongera CUF.
   
 13. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,966
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Kaenda kupiga ramli hehehehehehehe!!!!Nyani haoni makalio yake hahahaha!
  Ya leo kali ngoja nikapate soda nimpe mkono kibunango
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unajua SaidSabke ,haijulikani unafurahikia kitu gani ,umelinganisha nini hata ukaibuka na kicheko cha kushangaza.

  Mambo ndani ya CUF yamewekwa wazi ,halafu mambo yaliyotokea hayahusiani na walioko nje kwa maana hayaigusi serikali yanawagusa viongozi na taratibu zao zimeonekana ndani ya barua kuwa jamaa alikuwa akionywa kitu alichokuwa anatafuna zaidi ni vya watu binafsi ,pengine utasema fedha ya Uchaguzi nayo akiitafuna ,vilevile utaona fedha hiyo haiathiri wananchi zaidi ya wao wenyewe sasa kama waliweza kupambana na Sultani CCM bila ya fedha hiyo na kumwacha jamaa wakimvutia siku ili awalipe maana wakienda mahakamani uwezo wa kulipwa utakuwa mdogo jamaa anaweza asilipe kitu na akafungwa jela miaka kumi ,mchezo umekwisha.
  Nashangaa sana maana la kuchekea halipo ,umesikia kumeruka mapanga huko Zanzibar ? Sultani CCM ameanza kurusha ngumi hata uchaguzi mkubwa bado lakini safari hii panga kwa panga ,watu wanakwenda na zana kamili kwenye uchaguzi hakuna kulala.
  Mfuasi wa CCM akitoa panga CUF anatoa Shoka .akitoa bunduki CUF anatoa mzinga ,mfuasi wa Sultani CCM akija kwa helikopta CUF ndio kabisa wanakuja na madege ya kivita. Lazima Sultani CCM safari hii aingie mitini. Maana hata Sultani CCM akija kwa ngalawa jamaa wanakuja na submarine lazima Sultani CCM atoke baru na pampas mkononi.
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mwiba kwa hili utatoa thanks kibao...
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa mmeumbuka mlizani CYF wanamkumbatia mtu ,hapana kile ni Chama cha Wananchi ni si Chama cha masultani ,halafu mwenyewe kaja juu hakulazimishwa hakufanyiwa mizengengwe wala hakuundiwa kamati.

  Na ndivyo inavyotakiwa kwa viongozi ,Mhunzi kama kiongozi nampa heko kwa kujiengua katika uongozi ,akijua kuwa alivyofanya haviendani na sehemu aliyopo na kuendelea kwake ni kukipaka mivi Chama zaidi ameambiwa arudi jimboni na kuomba msamaha ndio maana yake kwani alipewa dhamana na wananchi na kufika alipofika akaburuga na kujiona amekwishafika.

  Sasa huko kwenye wafuasi wa Sultani CCM ,mchukueni jamaa huyo na kumpa kazi ya asasi za propaganda bila ya shaka atazua jipya na nyie wasikilizaje wake mtapata cha kurapu hapa JF.

  Niliwahi kusema kama CCM inameguka mkaleta za kuleta leo safari hiyo imeanza ,sijui nyie wapambe mtaelekea wapi !!!
   
 17. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Maneno mazito hayo...vipi kuhusu Lwakatare, alifanya nini?
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pengine niliposema huyu bwana ni mgoni wa kutupwa mlizani namkandia lakini kutokana na kauli yake iliyonakiliwa na Nipashe anasema kuwa watu wana makosa makubwa yanayohusu UZINZI na hawachukuliwi hatua. Oneni akili yake ilivyochafuliwa na ngono, anahisi makosa yake hayana maana na kuona ngono ni issue.Nafikiri kama ngono ingekuwa issue huko CUF basi huyu bwana angekwishamalizwa tangu kipindi kilichopita cha 2000/2005 kwani alimdandia mwakilishi mwenziwe kama yu mkewe.
   
 19. eddiy

  eddiy Member

  #19
  Mar 8, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 23
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Ndugu yangu Deganche2008 huayajui ni mamgapi yaliyotokea TANZANIA ccm mamefika kuua wewe upo wapi hujui kitu ndugu yangu sio tutizame Muhuzi tu ile ndio CUF MTU NI KUWAJIBIKA sio kulindana ukae ufahamu .
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  ^^ Mtoto akililia wembe mpe...Jamaa zangu walisahau hilo
   
Loading...