Mkuu, pamoja na yote sijaona maana ya BAK kubwatuka namna hiyo, ni vema akatoa sababu za msingi kwa Mbunge huyo kuwa fisadi, na hii iwe mbali na msharahara wake na marupurupu mengine yatokanayo wadhifa wake kama Mbunge.
VETERAN politician Dr Chrisant Mzindakaya yesterday attacked critics of President Jakaya Kikwete's leadership, saying in most cases their accusations and complaints against him were not based on facts.
"It is also not proper to single out Mr Kikwete alone, instead of the entire leadership that collectively runs the country," said Dr Mzindakaya, the Member of Parliament for Kwela constituency (CCM), in Rukwa Region.
He said Mr Kikwete was elected along with MPs, Councillors and other leaders at grass roots level. "The entire leadership is, therefore, collectively responsible
Haijalishi ni kwa namna gani unamfahamu Mhe. huyo, zaidi inanifanya nikuone wewe ni zaidi ya mwehu kwa kuja na tuhuma za kwenye magazeti, ambayo kwa nafasi yao yameaumua kuwa tofauti na Mhe. kwa utashi wao binafsi.Miye ni mmoja wa wale Wehu ambao hawaoni kwamba Kikwete anastahili kugombea tena 2010. Kwa hiyo kama huzijui sababu zilizofanya Mzindakaya awe katika kundi la mafisadi, basi sidhani kama utaweza kuelewa chochote mimi mwehu nikikueleza sababu hizo. Kama unamuona Mzindakaya ni malaika kila la heri tuache sisi wehu tuendelee kumuona Mzindakaya kama ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini na tuna sababu nyingi za kumuona Mzindakaya kama ni fisadi. Miye namfahamu huyu bwana kwa karibu sana tena kwa miaka mingi tu.
Mtizame na huyu! Sijui katokea shamba gani! Hivi kuna fisadi uchwara na fisadi tajiri? Ulofa mwingine unatia shaka!We kibunango pia ni walewale tu, fisadi ingawa ni bado uchwara, sijui mmetumwa nyie, mnanikera na hilo li-chama lenu mafisadi, sasa unamtetea mzindakaya ili iweje. Nyie wote Mafisadi tu.
Sasa kama mheshimiwa raisi naye ana fikra za namna hii, kuna uongozi kweli???????????? What is ths wivu na chuki??? halafu watanzania tutegemee mabadiliko, maendeleo kutoka viongozi wa namna hiiii!!!!!!!!!!!!- Kwanza mbunge anasema kwamba complaints hazina facts! Halafu anakuja chini hapa anasema sio sawa kumshambulia Rais Kikwete peke yake, badala yake iwe ni viongozi wote:-
- Halafu anabadilika tena na kusema Rais alichaguliwa na viongozi wengine pia, ona hapa chini:-
- Sasa unakaa na kujiuliza hivi hili taifa tulimkosea nini Mungu? Sisi wananchi wa Tanzania tumlimchagua Rais kuongoza taifa, yaani sisi wananchi na tukampa nafasi kikatiba kuchagua washauri wake na wasaidizi wa kutimiza lengo letu kwenye taifa, sasa leo tunaposema ameshindwa kazi tuliyompa, Mzindakaya anasema nini tena? eti tuwashambulie viongozi wote, wakati kamati ya bunge imeshasema wazi kwa kuwataja kwa majina wahusika wa Richimonduli na hata ikatoa ushauri wa nini kifanywe kisheria kuwaadhibu majambazi wakubwa kina Lowassa, Rostam, Msabaha, Karamagi, Mwakapugi, mpaka Hosea, sasa tulitegemea our Chief Law-Enforcement Officer, Rais wa jamhuri Kikwete awashughulikie haraka inavyotakiwa, sasa kama ameshindwa ashambuliwe nani madiwani?
- I mean wabunge wamefanya kazi yao, kuanzia kamati ya Mwakyembe, mpaka bunge zima limeipitisha ile ripoti, sasa Mzindakaya anataka tuwalaumu madiwani kwamba kwa nini ripoti haijfanyiwa kazi badala ya kiongozi tuliyemchagua kusimamia sheria za jamhuri yaani Rais wa jamhuri! Sasa kama huyu ni mbunge tena wa toka enzi za Mwalimu, sasa tutegemee nini kutoka kwa Rais? Maana hawa kina Mzindakaya ndio washauri wenyewe wa Rais, na believe me anawawakilisha wengi sana na hizi nonsense!
- Kwanza anasema hakuna facts, halafu anasema asishambuliwe Rais peke yake maana makosa sio yake peke yake na wengine pia, mweeee! Mungu mweeee! hivi tulikukosea nini hili taifa? Wa-Tanzania inabidi tuendelee kushambulia hapo hapo maana inaonekana this time message imefika, tulisema huko nyuma kuwa iko siku the buck itafikishwa inapotakiwa, yaani mezani kwa Rais na sasa imefika!
- I mean Rais wa jamhuri anaulizwa na kina Butiku na Quaresi, kwamba yeye kama Chief Law Enforcer wa Jamhuri hii, kwa nini majambazi wa Richimonduli wapo nje, yeye anajibu kwamba eti ni wivu na chuki, Sophia aliposema ni wivu na chuki kule kwenye kamati ya Mwinyi, tulidhani amepagawa kumbe sasa inaonekana kuwa huenda ndiyo lugha ya huko Ikulu, kwamba kila anayekosoa ana wivu na chuki ya kukosa Urais na u-First Lady, pleeease tulijua tu kuna siku yatawafika shingoni kuhadaa wanachi, kununua media, kuwatumia kina Tido Mhando na polls fake, kuwatumia waalimu wa mlimani, mihela ya Iran, kuwachafua kina Salim, yote haya ya yalikuwa ya nini kama kweli mlikuwa na uwezo wa kuongoza?
- Sasa saa imefika ya kuhesabiwa mnalia wivu na chuki, mkatishia weee kwamba Mtandao msipopewa uongozi basi taifa halitakalika wala halitaongozeka garademiti, sasa uongozi umewashinda mnalilia wivu na chuki, maana Quaresi naye aligombea urais sasa ana chuki za kuukosa na mkewe kukosa u-First Lady pure nonsense!, unajua inafurahisha sana mnavyoumbuka ingawa on the other hand pia inasikitisha sana kwa sababu mnaumbuka kwa ghrama ya migongo ya umasikini wa wanachi walalahoi!
Mungu Aibariki Tanzania!
Respect.
FMEs!
Haijalishi ni kwa namna gani unamfahamu Mhe. huyo, zaidi inanifanya nikuone wewe ni zaidi ya mwehu kwa kuja na tuhuma za kwenye magazeti, ambayo kwa nafasi yao yameaumua kuwa tofauti na Mhe. kwa utashi wao binafsi.
Pengine kutokana na ufahamu wako au ukaribu wako na Mbunge huyo, kumekufanya uwe na chuki binafsi, hata hivyo kwa upande wetu tutasikia kelele zako pasipo majibu. Kwani huyo sio Mnyika ama Slaa ama Zitto kana kwamba ataweza kuja hapa na kukujibu.
Siwezi kukaa kimya na kukuacha ukipandikiza mbegu za chuki, dhihaka na kejeli huku ukijiita mwehu ili kupata huruma za wanaJF. Usipokuwa na ushahidi na tuhuma zako utaelezwa tu, na pengine ni vema kujua kwamba hapa sio genge la kupayuka tu! Hata hao magwiji wa kupayuka na kupaka matope serikali yetu huwa tunawapasha humu humu ndani.
Sio siri kwamba kuna ufisadi ndani ya serikali, ila ni vema kuja na hoja kamilifu juu wa ufisadi husika, zaidi ya madai ya kumjua mtu kibinafsi. Nchi haijengwi kwa majungu!
Nyambala,'Sasa kama mheshimiwa raisi naye ana fikra za namna hii, kuna uongozi kweli???????????? What is ths wivu na chuki??? halafu watanzania tutegemee mabadiliko, maendeleo kutoka viongozi wa namna hiiii!!!!!!!!!!!!
Salim alipenda kusema ni Wavuja jasho... hiyo hapo juu ni ya Mtikila. Hii ni heshima yake kwa wale wanaohangaika katika Taifa hili, na sio kebehi kwao kama Mtikila alivyowatambua. Itachukua muda mrefu kutenganisha wehu katika nchi hii!
on the other hand pia inasikitisha sana kwa sababu mnaumbuka kwa ghrama ya migongo ya umasikini wa wanachi walalahoi!
...Weye mwenye hiyo bendera inayonuka uchafu mwingi bora ufunge domo lako ! Kwani ni uongo huyo mzee mchovu hakupewa mkopo kinyemela, na vipi ule mradi hewa wa kusindika nyama za nzi...?
Si amepora mashamba ya wananchi kule kwao.....!! Na kule Kigoma je ? Acha hizo wewe mshamba usiyejua lolote !! Huyu mzee choka ile mbaya, na sasa anatafuta sababu za kijinga ili aendelee kuganga njaa....maana kila mtu alishamshiti- alihongwa wakati ule akijifanya mzee wa mabomu..!. Muulize hata mwanaye Simon atakupa ukweli jinsi huyu alivyoishiwa, na hata zile dili zake za usangoma hazina nguvu tena ! Kama ni kuruka kwa nyungo, wapo wakali wengine siku hizi.....
hapo umenena,,mzinakaya ni fisadi mkubwa sana mimi namjua fika tunakaa jirani ufipa amepora maelfu ya maekari ya ardhi rukwa na kigoma kawanyanganya wanyonge ardhi zao,pia katika katavi national park ana maeneo ya game reserve analeta wazungu wanajizolea rasilimali zetu mwisho atatumalizia wanyama wetu,katavi kuna maovu makubwa yanafanyika kushinda hata huko loliondo mnapopapigia kelele kila siku,nendeni mpanda mkajionee wasivyofaidika na rasilimali zao,inauma sana.Inashangaza sana akiguswa fisadi la ssm tu utaona jinsi wanassm wa hapa forum wanavyomtetea. Yaani kuna mtu ataniambia kuwa Mzindakaya si fisadi?? Mzindakaya ni fisadi la kutosha na la nguvu kabisa!! Facts zipo!!! Tafuta riport ya PCB enzi hizo na lile deni la kiini macho kule BOT!!!
Kingine ni hovyo si mtendaji, amekuwa katika ubunge kabla hata sijajliwa mtoto, na leo nina wajukuu hakuna kitu cha maana amefanya Bungeni kwake zaidi ya kuwatishia watu wanaotaka kiti chake!!!!! Anawatishia kwa njia gani!!! Jibu kapuni.!!!!
Jamani tuweke itikadi pembeni tuwe wakweli na si kutetea hata uozo. Rafiki mzuri ni yule anayeona ukweli na kuukemea. Hebu nyie wanassm oneni ukweli na mkosoane na mambo yatakuwa shwari. Yaani utaona mtu kama makamba anaropoka mbele ya vyombo vya habari upupu tu eti anatetea chama. Utafikiri speed governor za ubongo zimekatika!!!! Kulaleki.
hapo ndo unaijua CCM vizuri.....yani ukweli kwa CCM ni sumu na wanaweza kukuua ukisimamia ukweli.
Umenena kweli mkuu, hata mabomu aliyokua akifyatua ilikua kwa maslahi binafsi. Watu walikua wakimtumia kudefend madhambi yao au kuwaumbua wenzao kwa kumpa hongo akaropoke kwa sababu upstairs hamnazo....Weye mwenye hiyo bendera inayonuka uchafu mwingi bora ufunge domo lako ! Kwani ni uongo huyo mzee mchovu hakupewa mkopo kinyemela, na vipi ule mradi hewa wa kusindika nyama za nzi...?
Si amepora mashamba ya wananchi kule kwao.....!! Na kule Kigoma je ? Acha hizo wewe mshamba usiyejua lolote !! Huyu mzee choka ile mbaya, na sasa anatafuta sababu za kijinga ili aendelee kuganga njaa....maana kila mtu alishamshiti- alihongwa wakati ule akijifanya mzee wa mabomu..!. Muulize hata mwanaye Simon atakupa ukweli jinsi huyu alivyoishiwa, na hata zile dili zake za usangoma hazina nguvu tena ! Kama ni kuruka kwa nyungo, wapo wakali wengine siku hizi.....