Taratibu hizo ni zipi..? Na kwanini uziite hizo taratibu ni mitego..??
Nitajie hizo sheria za Mungu...Maana stress na anxiety haziletwi na kutotii sheria za Mungu...Kuna external na Intrnal factors....Watu waliotuzunguka na mazingira kwa ujumla...Sasa mimi sijaona hapo hizo sheria za Mungu zina-apply wapi...Nijuze
Let us come to the knowledge of the truth
Miili yetu inahitaji nishati ili kusimamia mood na emotion nzuri. kadri tunavyopata hii nishati ndivyo tunavyokua na mood na emotion nzuri. Kwa hiyo tunakuwa na afya ya kuendesha maisha yetu sawa sawa.
Tunaipataje hii nishati
Hii nishati inapatikana kupitia mambo manne. kwanza kumuabudu Mungu, pili kusoma na kuliamini neno la Mungu, tatu kufanya mambo mema na mwisho kutafakari mambo mema.
mambo gani yanapunguza hii nishati hivyo kusababisha mood na emotion mbaya.
Kuna mambo manne yanayopunguza hii nishati, kwanza kutomuamini Mungu, pili kutoamini neno la Mungu, tatu kutenda mabaya na mwisho kutafakari mambo mabaya.
Kwa hiyo sheria za Mungu kwa ujumla wake ambazo ni chimbuko la nuru ni 1.kumuabudu
Mungu 2. kusoma, kuliamini na kulitii neno lake 3.Kutenda mema na 4. Kutafakari mema.
Kwa kuongezea zaidi Kuhusiana na mema na mabaya ni kwamba chochote kile tunachokifanya au kuwaza kinaweza kuwa kibaya au Kizuri. Kanuni ni kwamba ukifanya au kuwaza mazuri ni chimbuko la nuru na ukifanya au kuwaza mabaya ni chimbuko la giza yaani inapunguza nuru.
Nadhani nimechambua kwa stahili inayoeleweka. Kama ni msomaji wa bibilia, ndicho kitabu ninachokiamini mimi, kuna mambo mengi manabii wamezungumza pamoja na nabii Musa aliandika amri kumi na mkombozi wetu Yesu kristo ametuagiza amri kuu mbili ambazo ni kumuabudu Mungu na Upendo.