Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,593
- 5,583
Bi Simone Gbagbo, mke wa Rais wa zamani wa Ivory Coast amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela. Simone amepatikana na hatia ya kushiriki katika machafuko ya baada ya uchaguzi wa Rais wa Kodivaa baina ya mwezi Novemba 2010 hadi Aprili 2011. Kesi ya Simone Gbagbo na viongozi 82 wa utawala wa zamani wa Ivory Coast ilianza kusikilizwa katika mahakama ya Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika tangu mwezi Januari mwaka huu.
Affi Nguessan, mkuu wa zamani wa chama cha kwanza cha Laurent na Simone Gbagbo naye amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela kwa kosa la kuhusika katika machafuko ya kipindi cha uchaguzi. Affi anatakiwa pia kufika mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ya nchini Uholanzi kwa tuhuma za kutenda jinai dhidi ya binadamu na kuwasaidia wafuasi wa Laurent Gbagbo, dikteta wa zamani wa Kodivaa kufanya mauaji dhidi ya wapinzani kwa nia ya kulinda utawala wao. Machafuko ya kisiasa yalizuka nchini Ivory Coast baada ya Laurent Gbagbo, mgombea wa chama tawala wakati huo kukataa matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi mpinzani wake Alassane Ouattara, Rais wa hivi sasa wa nchi hiyo.
Machafuko hayo yaliendelea kwa muda wa miezi mitano, huku mke wa Gbagbo, akiwa mstari wa mbele kupigania kubakia madarakani kwa njia yoyote ile, chama cha mumewe. Harakati za kisiasa za Simone Gbagbo zilianza wakati alipojiunga na Umoja wa Wafanyakazi wa Kodivaa na baada ya muda si mrefu alifungwa jela kutokana na kuukosoa vikali utawala wa wakati huo wa Félix Houphouët-Boigny. Sababu zilizopelekea kufungwa jela Simone Gbagbo na baadhi ya wapinzani wa Félix Houphouët-Boigny, kiongozi aliyepigania ukombozi wa Ivory Coast na kuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo ni kwamba rais huyo hakuwa tayari kuruhusu mfumo wa vyama vingi nchini humo. Hata hivyo wafuasi wa Simone Gbagbo waliohusika pakubwa katika kuanzisha magenge ya mauaji wakati wa mgogoro wa kisiasa nchini Kodivaa, kulimharibia mwanasiasa huyo na kupelekea hata kubadilishwa lakabu yake kutoka "Bibi Ngangari" na kuwa "Bibi Muuaji." Kipindi hicho cha miezi mitano ya machafuko kiliipelekea Ivory Coast hadi ukingoni mwa shimo la maangamizi ya vita vya pande zote vya wenyewe kwa kwenyewe. Mgogoro huo usingelizuka kama si ukaidi na kupenda madaraka Laurent Gbagbo.
Hatimaye askari wa kimataifa chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wanamgambo waliochukua silaha kulinda matokeo ya uchaguzi, walifanikiwa kuipindua serikali ya Laurent Gbagbo tarehe 11 Aprili 2011 na kumtia mbaroni Laurent Gbagbo na kumkabidhi kwa mahakama ya ICC. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, kufungwa jela Simone Gbagbo na viongozi 82 wa utawala wa zamani wa Kodivaa ni mtihani muhimu kwa mfumo wa mahakama wa nchi hiyo hususan katika wakati huu ambapo wananchi na serikali ya Ivory Coast inapigania kuleta umoja wa kitaifa na kurejesha amani na utulivu nchini humo.