WomanOfSubstance
Platinum Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 972
- Thread starter
-
- #21
WomenofSubstenc,
Bibie hapa kidogo sintakubaliana nawe kwa sababu neno First Lady ni wadhifa (kwa kuelewa kwangu) ..Otherwise tulitakiwa kumwita Mrs. Kikwete.. Hilo neno First Lady lina uzito mkubwa sana na heshima zote anazopata zinatokana na neno hilo na mnategemea vitu fulani kutokana na wadhifa huo. Na wadhifa huu hukoma tu pindi akiondoka Ikulu...Ni sawa na wadhifa wowote ule hata iwe dereva, ataitwa dereva kwa sababu amnaendesha gari, nje ya hapo sii dereva.
Pili, kinachonisumbua mimi na hoja nyingi zinazohusiana na First Lady ni ile copy cat ya First Lady wa Marekani. Kila hoja humu inatazama kazi za First Lady wa Marekani na tunajaribu kulinganisha jambo ambalo sii lazima kabisa. Kuna mataifa mangapi duniani? na ni First Lady wangapi wanayafanya anayoyafanya mke wa Bush au Obama..
Hizo Public Appearence na misafara ni ngapi tumewaona wake wa viongozi hawa wakishiriki..Wachache sana hawaweza kuwa sawa au kulingana na rais wa Marekani. Hivi navyozungumza simfahamu mke wa Gordon hata kwa sura maana sijawahi kumwona popote..Acha huyo naweza sema asilimia 99 ya wake za Marais sina habari zao kikamilifu na umenisaidia sana kusoma baadhi ya maelezo yako ya mwanzo.
Muhimu kwetu ni tufikirie tunataka nini mke wa rais akifanye na anatweza vipi kulisaidia Taifa letu kutunza, kutangaza na kuimarisha asili na mila zetu..
- Mwanamke ndiye mtendaji mkuu (rubani) wa familia zetu!.
Nadhani Mkuu hatutofautiani katika hili na nafikiri hata ukirejea posts zangu za awali utaona tuko pamoja kabisa.Kinachogomba ni vile tunavyotarajia FL wa Tanzania awe sawa na wale wa Marekani na kwingineko wakati mazingira na historia ni tofauti kabisa.
Respect.
WoS
Wakiwekwa ma-first lady hadharani wapeane mkono na watu kila mmoja atakimbilia kwa Mama Maria na kuacha hao wengine wapewe mikono na waliowaajiri kwenye hizo NGO zao.
Paskali.
Nje ya hapo nadhani tumeona kuwa First Lady wote wa Kiafrika wamekuwa mbele ktk siasa za utawala wao kitandani kuingia hadi ktk Utawala wa nchi nzima..Kutokana na Umaskini wetu hata mila na desturi zetu za kiasili zimepotea hivyo tunajaribu kuiga vitu ambavyo hatuna kabisa uwezo navyo kutokana na mazingira yetu kwani Ukitazama kati ya First Lady wote wa nchi za Kiafrika ni asilimia ndogo sana waliomaliza high school acha mbali chuo kikuu
Umeenda mbali. Kwani viongozi wetu hapa nchini ambao waume zao sio mawaziri au viongozi wakuu waume zao umeshawahi kuwaona hadharani? Wanawake ndio zao akishakuwa mkubwa anamwacha nyuma mumewe. Hawi nae bega kwa bega. Hata kwenye sherehe hutawaona. Je, ulimwona mumewe Sophia Simba siku ile anachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake? Mie sikumuona.
Mama Maria Nyerere aliulizwa swali kama mnalolijadili. Alijibu kwamba wao kama wanawake sehemu ya ilikuwa UWT basi. Hakujitutumua na lolote. Ukiuliza shughuli zake sasa hivi tunaambiwa kuwa ni muumini mzuri wa Kanisa lake Katoliki.
Kwa uadilifu wa First Ladies hatajatokea kama huyu. Ujasiri amali aliojaribisha ni wa kufuga kuku tena kwa mtaji aliopata baada ya kupata zawadi ya Rais Nyerere kustaafu.
Leo hii heshima imemjaa tele.
Wakiwekwa ma-first lady hadharani wapeane mkono na watu kila mmoja atakimbilia kwa Mama Maria na kuacha hao wengine wapewe mikono na waliowaajiri kwenye hizo NGO zao.
Paskali.
Good to learn abt the history of FLs of USA.
Tukija huku Tz, wengi wa wale waliokuja kuchukua uongozi, tayari walishajipatia wenzi wao wa maisha ambao si ajabu walijikuta tu wanalazimika kufanya u FL bila hata maandalizi yoyote.Ningetegemea Serikali yetu na hasa Wizara za Mambo ya nje wakishirikiana na Wizara ya Wanawake wangeona umuhimu wa kutengeneza induction programme ya kuwasaidia wamama wa kwanza kwa kila hali - kuanzia kuwapa msasa wa mambo ya kidiplomasia, uendeshaji wa ikulu kama makazi rasmi ya rais, na stadi nyingine ikiwa ni pamoja na public speaking na hata kuongeza elimu.
The question remains -Is it true or false?...I think this is very insulting, generalizing, and biased opinion. Yes, we could argue first ladies perhaps they have not deriver to our expected standards, perhaps they don't have the qualities we dream for. However, building an argument on "utawala wa kitandani, and low education", it is out of boundaries.
Hapa Petu,
The question remains -Is it true or false?...
The FL positions depends on political position of the woman herself, power relations in the marriage, availability of resources, personality, and context of the country.
I believe, first lady could do more even in tanzania, they simply need support to organize their actions.