Fire safety certificate! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fire safety certificate!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kilambi, Oct 23, 2009.

 1. K

  Kilambi Member

  #1
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  samahani wakuu, naomba kumnukuu mdau huyu toka mtaa wa jirani.....

  "Kwako brother Michuzi,Naomba unirushie haya machungu yangu,...............

  Naona serekali kuona vyote hivyo sasa tunatakiwa kuwa na sticker ya Fire, hizo windscreen zipo kwa ajili ya kujaza sticker tu na kilicho kibaya gharama yake ni Tsh 20,000 kwa gari ndogo kama sio ufisadi huu ni nini tena niweke mtungi wa kilo moja gari yenyewe Toyota March kweli hii ni haki??

  Wanachi wenzangu naombeni tusaidiane kwa hili, kama maisha bora kwa kila mtanzania ndio haya, tumekwisha!

  wenzetu waipeleka nchi kubaya kila siku kesi mahakamani halafu zinaishia hewani na sisi tunaojitahidi angalau kidogo kitu tunazidi kubanwa. Basi boresheni usafiri wa jumuia ili tupande mabasi mbaki na magari yenu. Kesho na kesho kutwa tutaambiwa watu wa FIRST AID naona wanataka magari yote yawe na KIT na sticker zipandikwe kwa gharama wanayotaka wao.

  This is too much jamani...........
  tunaelekea wapi?????????
  nisaidieni ndugu zangu

  WENU
  DaimaFuraha"
  • hivi kabla ya kupewa hizi stika si askari anatakiwa kukagua kama unao huo mtungi wa kuzimia moto???
  • si inatakiwa pia kuukagua huo mtungi kama unakidhi mahitaji kulinganisha na gari husika???
  • sasa inakuwaje zinauzwa kama njugu bila kufanyika ukaguzi wowote??
  • haka kamradi kana manufaa yapi na kanamfaidisha nani?
  • iweje basi upewe stika leo October ambayo validity yake ni mwaka mmoja, lakini ziishie mwezi juni mwakani?!
  • kama kuchelewa kuzitoa/kupitisha hiyo sheria sijui muswada kwa nini mimi mwananchi niadhibiwe kulipia huduma ya mwaka mzima then niishie kupata huduma hiyo kwa miezi michache?

   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sheria ya wapi imepitisha kuwekwa sticker za vizimio????
  Huu ni ujinga tu
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hujaona idadi ya magari yanayoungua na kuisha kwa kukosa vizimio?

  Mi naona ni kitu nzuri tu!

  Msinikumbushe 2007 jamaangu mwanafunzi wa CBE, aliyekuwa anasafiri na basi la Mohamed Trans toka Dar to Mza, lililoungua majivu hujo Singida, naye akawa mhanga!
   
 4. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni muhimu gari kuwa na hivi vizimio, lakini kama vinauzwa hovyo hapo ndio tatizo. Wataalamu wakutafuta mradi washagundua dili. Nadhani visimamiwe kwa gharama ambazo zinawezekana kwa watumiaji ili kuboresha usalama. Lakini kama zinatolewa tuu hovyo hovyo hata kwa mtu asiekuwa nacho ndani ya gari ni hatari!
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Unajua hata vizima moto vina namna ya kutumia. Watu wangapi wamefundishwa kuvitumia in case moto unatokea? au ndo kuviweka tu ndani ya gari ili kuwaonyesha trafiki wakiulizia?
   
 6. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  vizimio tununue sticker kulipia 20,000/= ya nini tena?wavivu wa mawazo utawajua tu,upuuzi mtupu!!na mwakani utasikia sticker za uchaguzi kulipia 50,000/-
   
 7. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Sasa hawa jamaa hawaeleweki kabisaaa.
  Saloon car inabeba abiria wangapi na je,gari la abiria linaloanzia na mtu1 linaanzia size gani?

  Kuna hili tangazo limetolewa na hilo jeshi la zimamoto.Nanukulu:

  1.Salooncar-liwe na dry powder f/ext ya kg 1 na stika yake ni Tshs 5000/=

  2.Magari ya abiria kuanzia abiria 1 hadi 20 na magari ya mizigo yenye uzito hadi tani tano,station wagon,liwe na dry powder f/ext kgs5 na stika yake Tshs20000/=.

  3.Magari yote kuanzia tani 7 na kuendelea kizimio chake ni dry powder f/ext kgs2 na stika Tshs 30000/=

  Wote mna karibishwa jengo la ushirika-lumumba st.mnazi mmoja.


  Sasa moja na mbili tofauti ni ipi,katika mchanganuo wao???????
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  pesa za uchaguzi zinatafutwa
   
 9. a

  alex50 JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Stika za fire zinatolewa baada ya kupat huduma gani?

  Stia mtu hupewa baada ya kulipia huduma. stika ni utambulisho kuwa kuna huduma umepewa.

  Ukilipia bima unapewa stika

  Road licence unapewa stika-huduma ni utumiaji wa bara bara

  nenda kwa usalama-gari linakaguliwa

  Fire stika ni kwa huduma gani

  Tumechoka kusumbuliwa na kufanywa mazuzu, watanzania inabidi tuamke, tukatae kuonewa na watawala hawa walafi, mabilioni wanataka kukusanya kwa njia ya panya.

  Serikali hukusanya kodi baada ya bunge kuridhia, Bunge lipi limepitisha sheria ya stika ya fire. Nisipolipa nitapelekwa mahakamani?

  Kwa sheria ipi?

  Naomba ufafanuzi ndugu zangu.[/SIZE][/I][/COLOR]
   
Loading...