Final Decision: Nakimbia ndoa. Naogopa kuua

Final Decision: Nakimbia ndoa. Naogopa kuua

Asanteni sana wadau. Sasa hivi. ...nitamchukua nitaenda nae lunch. ...hotel flani hivi....kupo kimya sana. Nimemuomba nikafanye nae maongezi ili kesho niondoke. Kakubali.........let love lead. To God be the Groly!!!

maaamuzi mazito kama hayo hutakiwi kumpa mwanya adui. ngoja akakulegezee sauti huko akurembulie na macho ulainike mtoto wa kiume.
 
Heee sasa utatuudhi kwa yote alokufanyia bado unampa priority ya kumpeleka lunch muongee?acha hizo kaka...we tambaa zako kama kweli umedhamiria na umekereka na tabia zake..unanegotiate nn sasa?unadhan atakubali uondoke?lazima ataomba msamaha utamsamehe..haujui wanawake tuna nguvu sana ya kushawishi ww..ohooo shauriyakooo
 
How can a normal human being have such patience and humility? Kaka wewe una moyo wa kimalaika aisee hongera sana kwa hilo and umechukua uamuzi sahihi kabisa. Achana na janga hilo!
 
na kweli yawezekana maana kasema ana ugonjwa mkubwa hataki kuutaja naona kama ndo wahusika wenyewe

huyo bnyanya amecoment hapo juu muda sio mrefu nadhan amedelete ndo nikaelewa ndo wenyew lakin kila mmoja anajitetea@The secretary
 
kila la heri ndugu ila kumbuka watoto, huyo mwanamke atawapoteza bure, jitahidi wasidhurike na huo uamuzi wako
 
Ndugu wanajf. Nashukuru kwa michango yenu ya ushauri juu ya swala langu kwenye uzi wa "Nakimbia ndoa-Naogopa kuua". Nawashukuru sana na heshimu sana mawazo yenu.



Kwakua huyu mwanamke amekua sio mstaarabu na katili kiasi hicho nimeamua kufanya yafuatayo lakini kwa uchungu sana kwani ni uamuzi mgumu sana hata zaidi ya waliochukua CDM kwa zito.


Awali ya yote..kama nilivyowafahamisha...licha ya kumsomesha na kumgikisha hapo alipo sasa. Lakin kuna kubwa ambalo sikuliweka wazi ambalo mnaweza kuniona mjinga sana na kunishangaa kwamba mimi ni mwanamme wa namna gani.


Nakumbuka ilikua miaka 5 nyuma..huyu mwanamke nilienda kuchek nae afya(ukimwi). Na majibu yakawa yeye kaathirika. .mimi sijaathirika. Ilikua siku ya huzuni sana na majonzi. Nikamwambia anieleze alikopatia huo ukimwi....na kwann alinificha kwa kipindi chote hicho ili hali anamimba na kajifungua mtoto?..kwann hakua wazi kwangu na kwa mimba yake ili hata mtoto aepushwe na maradhi?


Akaniambia..alikua anaogopa angeniambia ningemuacha na kwamba alikua akinipenda sana. Kuhusu mtoto akasema alifoji vheti vha clinic ili asigunduliwe kua kaathirika. Hajui alikopata ngoma lakini anasema alienda kupima miaka saba kabla haya mimi kukutana nae na akaambiwa kaathirika.


Nilichofanya mimi siku hiyo, nilimwambia ivi:-

"Nimekusamehe...na sitakuacha kwa tatizo ulilonalo;.kwakua tumekua tukisumbuana kwa muda mrefu kupigishana kelele kwa mambo jamii ya umalaya..uzinzi..uongo..unafki. ...Nakuomba usinisumbue tena kuanzia leo. Nahaidi nitakua mfariji wako. Na nitaendelea kufanya mapenzi kama awali na itakua mara dufu. "


Kweli maisha yakaenda...nikawa namhimiza sana mambo ya Mungu. Nikampeleka na chuo kusoma. Huko sasa mambo yakaanza kwenda ovyo taratibutaratibu.....akaanza majibu ya dharau..mara nisikie mastory ya kugongwa na wanamme mara ana marafiki malaya. Nilikua naumia sana...natoka miles nyingi kwenda kunuona pale chuoni. Ilikua ni shida mpaka akamaliza.


Anyways..ni mambo mengi yaliendelea....na nilikua nikizini nae tu na tukaendelea kupata watoto. Cha ajabu kila nikienda kupima...majibu yangu ni negative mpaka leo hii. Sijui ni muujiza wa namna gani huu.


Huu ndio uamuzi wa mwisho ambao nimeamua kuufanya mimi Hasan Abas Abdalah baada ya kuongea na wazazi pande mbili, viongoz wa dini na watu wazima na humu jf.


1: Hassan achana na huyo mwanamke kabisa...ni kafri na muuaji mkubwa...sio mstaarabu hata kidogo.


2. Mwachie kila kitu...kaanze maisha upya. Nenda mbali nae kabisa. Nenda hata Mtwara au Morogoro kaanzishe maisha.

3. Wanawake wapo wengi sana...yupo Mungu aliyekuandalia..ambae atakutii kwa utayokua unamweleza na moyo wako utauona tu koz utakua umetulia wala hutakua na wasiwasi.


4. Ukitaka kuondoka haina haja ya kumuaga na kumtolea maneno makali au ya laana. Mwambie nashukuru...mi naondoka, nitunzie watoto wangu kwa kipindi hiki cha mpito. Na asijue unakokwenda.


5. Kua karibu na Mungu sana...achana na mambo ya wanawake kwasasa Hasan...tafuta hela...Mungu awe rafiki yako mkubwa.



6. Muondoe kabisa katika akili yako...hilo ni joka kubwa ambalo ulikua ukiishi nalo bila kujua.


Nimeongea na kiongoz wa dini mmoja asbh hii.....aisee nimeona akili imefunguka kabisa. Sasa nafua nguo kujiandaa na safari leo hii au kesho au jumatatu.


Mungu nitangulie na nilinde kokote niendako....nakuachia watoto wangu...walinde na waepushe na uchafu wowote. Nakuomba Mungu unajilie huko niendako nipate kibali cha mafanikio ili nije niishi na watoto wangu..wasome katika level yeyote ya elimu na kuwafanikishia kua na maisha bora na familia njema kabisa.


Namsamehe mwanamke huyu kwa yote na mi pia naomba Mungu unisamehe kwa mabaya yote ambayo nimekua nikimtendea. Mlinde pia...muepushe na roho chafu alizonazo....mhurumie. Mpe utashi wa kuelewa anachofanya.


Kwa wanawake wote wanaosoma uzi huu na wanatabia za kunyanyasa wamme zao au kua na majibu machafu ya kuwachanganya wanamme zao...nawasihi waache tabia hizo....sio vizuri kabisa mbele za Mungu.


Asante JF members kwa maoni yenu na ushauri. Mungu awabariki sana.


Nahitaji maombi yenu pia.
Uko sawa lakini hauko sawa..ukisema akutunzie watoto na wewe ni mwanaume hapo mimi kama mwanaume pia sioni kama pako sawa,natambua sana wanawake wenye makelele hukera kupita kiasi na wanakatisha tamaa lakini swala la watoto huwapendi?au ana uwezo wa kuwatunza ndo mana unaona poa tu hata ukiondoka?kwangu mimi watoto ni kila kitu hasa iwapo ninaishi nao nyumbani,ingekua watoto wako huko nje na hauishi na mama mtu ingesema utakua unatuma pesa za matumizi ya hao watoto lakini uko nao ndani uondoke uwaache?? Aaaaah bana
 
Uko sawa lakini hauko sawa..ukisema akutunzie watoto na wewe ni mwanaume hapo mimi kama mwanaume pia sioni kama pako sawa,natambua sana wanawake wenye makelele hukera kupita kiasi na wanakatisha tamaa lakini swala la watoto huwapendi?au ana uwezo wa kuwatunza ndo mana unaona poa tu hata ukiondoka?kwangu mimi watoto ni kila kitu hasa iwapo ninaishi nao nyumbani,ingekua watoto wako huko nje na hauishi na mama mtu ingesema utakua unatuma pesa za matumizi ya hao watoto lakini uko nao ndani uondoke uwaache?? Aaaaah bana
Hii niyamiaka kama kumi kasoro iliyopita. Achana nayo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom