Nakumbuka pale mzumbe sekondari tulikuwa na shujaa mmoja simtaji jina. Alivuma sana na kupendwa na wanafunzi wote.
Ushuja wake ulitokana na kutoroka shule bila ya kukamatwa. Kubishia walimu. Na kuvumilia fimbo siku akikamatwa. Jamaa alikuwa maarufu ilibidi mwalimu mkuu awe anafika mstarini kila asubuhi kuhakikisha huyu jamaa hakulala nje ya shule.
Huyo ndie aliyekuwa shujaa wetu.
Sasa siwashangai wanaomuona Lissu ni shujaa. Ni shujaa kwa sababu anapinga mamlaka iliyopo kama yule shujaa wetu wa Mzumbe.
Uhuru tulishapata siku nyingi. Hayo malalamiko yake angeweza kuyafikisha bila ya matusi na ugomvi katika taratibu zilizowekwa.
Amefikia mpaka kuomba Tanzania inyimwe misaada. Ni watanzania wangapi watakufa njaa, kukosa elimu, kukosa matibabu nk ikiwa jumuia ya kimataifa itaitenga Tanzania?
Lakini bado mtu wa hivyo anaonekana ni shujaa na kushangiliwa na wengi.
CHADEMA ina mwenyekiti na wanasheria wengi wazuri ambao wana uwezo wa kufikiri na kufikisha ujumbe kwa wananchi bila ya kuingia utata na serikali.