Filikunjombe anena mbele ya Mangula

Filikunjombe anena mbele ya Mangula

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803


​


Viongozi wa CCM mkoa Njombe wakishirikiana na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Phili Mangula ( wa pili kulia ) kuwaongoza wanachama wapya wa CCM zaidi ya 600 waliojiunga na CCM jana wakati wa mapokezi ya makamu huyo wa kwanza kulia ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini na spika wa bunge Anne Makinda wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mbunge wa jimbo la Njombe kasikazin na anayefuatia ni katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike




Deo Filikunjombe miongoni mwa wananchi









Msafara wa pikipiki kwenye mapokezi ya Mangula Njombe
​

Picha na Said Ng'amilo wa Mjengwablog



​




Habari na Francis Godwin​


MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe awakuna wapiga kura wa jimbo la Njombe Kaskazini Linaloongozwa na mbunge wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga Kwa kuwalipua watendaji wabovu serikalini ,mbele ya makamu mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Tanzania bara Philip Mangula.


Filikunjombe ambea alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano huo mkubwa wa mapokezi ya Mangula mkoani Njombe alisema kuwa masikitiko ya wananchi juu ya serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya Chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wananchi kukichafua Chama tawala.


" Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe Chama chetu CCM ni Chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete ,Kinana na Mangula ni safu ya uhakika na itakiwezesha Chama chetu kuendelea kuaminiwa zaidi na watanzania ...ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika katika nafasi zao"kauli iliyowakuna wananchi na kushindwa kujizuia kushangilia huku wakiimba wewe ni Jembe .


Hata hivyo Filikunjombe alisema kuwa ili Chama kuendelea kupendwa na akina Mangula na Kinana wanapaswa kusaidiwa na watanzania wote kwa kuombewa zaidi ili kuendelea kuifanya kazi hiyo bila woga ndani ya chama.


Kwa Upande wake Mangula mbali ya kusifu mapokezi makubwa ya kihistoria Katika mji wa Makambako na Njombe mkoani Njombe aliweza kutoa ya Moyoni kuhusu Kati yake na Rais Jakaya Kikwete kwa Madai kuwa yeye alikuwa hajui chochote juu ya uteuzi wake na kuwa alisitaajabu kupokea simu ya Kikwete kuhusu kusudio la uteuzi wake.


" Kweli Mimi nilikwenda Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM Kama mualikwa ila Nikiwa Hotelini nilipokea simu ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete akiomba kuniteua kuwa makamu mwenyekiti na baada ya kwenda Ukumbini wajumbe wote walinipa kura zote za ndio...kweli namshukuru sana mwenyekiti wangu na wanachama wote na sasa ni kazi zaidi na sitawaangusha"


Hata hivyo aliwataka wana CCM kufanya vikao bila kuchota na kuwa wasizingizie kukosa ajenda kwani hata kukosa ajenda ndani ya CCM ni ajenda Kukosa agenda pia ni agenda ndani ya CCM pia yaweza kuwa ajenda.


Aidha amehimiza nidhamu na taratibu ndani ya CCM kuendelea kuzingatiwa ili kukiwezesha Chama kuwa na amani na kuwa iwapo taratibu ndani ya Chama hazitazingatiwa upo uwezekano wa Amani ndani ya nchi kutoweka.


Alisema kuwa haitapendeza kuona Tanzania inafika mahali inaendeshwa bila Chama iwapo tutaruhusu wasiopenda Amani kuendelea kuvuruga Amani yetu iliyopo...​


SOURCE: IRINGA YETU
 
FILIKUNJOMBE angewataja hao VIONGOZi wabovu ndani ya CCM kwa MAJINA... TUMECHOKA kulindana!!!
 
Atawezaje kumtaja mkuu wake? Ila huyu angalau aliwataja mawaziri wabovu kule Bungeni na kwasasa amekuwa adui ndani ya chama chake ilichopelekea hata kunyimwa nafasi ya kugombea NEC yao.
 
Imani ya wana CCM kwa Mangula inanikumbusha imani ya Watanzania kwa JK mwaka 2000, tatizo letu tunatoa sifa mara tu mtu anapochaguliwa wala hatusubiri tuone utendaji wake lah! sisi tunakurupuka na tu kummwagia, sifa akiboronga tunasingizia wasaidizi wake.

Wana CCM wamejenga imani kubwa sana na Mangula as if ameshuka gafla toka mbinguni au hakuwahi kushika madaraka ndani ya chama, kinachonifikirisha ni hapo aliposema alienda Dodoma wala hakujua kama atapata huo wadhifa na alishangaa alipopigiwa simu na JK akiombwa kuwa msaidizi wake, Mangula wala hakufikiria, wala hakujiandaa wala hata hakutaka ushauri kwa watu wake anaowaamini, kwasababu kapigiwa simu ya ulaji wala hakusita kukubali hicho cheo pamoja na unyanyasaji na udhalilishaji waliomfanyia huko nyuma mpaka kuanza kulalamikia rushwa pale aliposhindwa katika chaguzi huko kijijini kwao.
 
Yanani unapigiwa simu uko Bar kuhusu UTEUZI wako na wewe bila kutafakari wala kushauriana na familia yako UNAKUBALI on the Spot.

JK: Nimekupigia simu nataka nikuteuwe Makama mwenyekiti wa CCM Bara
Mangula: Ahsante mzee nimekubali UTEUZI wako. As simple as that!

Kama mambo ndiyo hivi kweli tutaacha kupata majaji VIHIYO!
 
Anaogopa watamuua chezea mafisadi wewe!

Oh Yeah... Nadhani au watamuondoa kwa UBUNGE wa CCM... Wana NGUVU ndani ya CCM Sababu kwa nini Wakati Wanachagua KATIBU MKUU; MELI ILISHA TUA HONG KONG na SHEHENA ya MENO ya TEMBO ya MAMILIONI YA DOLLAR; Na HUYO Katibu MKUU haongelei CHOCHOTE kuhusu SUALA HILO au UFISADI... NAPE NNAUYE PIA MDOMO wake kwenye SUALA HILO AMEUFYATA anamkimbilia Dr. SLAA na KADI ya CCM sijui aliipata kwa UFISADI???
 
Deo njoo CHADEMA tuendeleze mapambano kwani huko mafisadi yatakufanyia kitu mbaya.
 
CCM hamna hata 1. alie msafi kwa hiyo sina Habari nao.
 
mtu akishakuwa ccm ninamuangalia kwa macho ya mashaka.filikunjombe is no exception
 
Ngonjera ,ngonjera, ngonjera, ngonjerax2
 
katika huu ulimwengu wa EPA, KAGODA,RICHMOND bado watu wanajiunga na ccm?? ni ajabu na kweli na wewe mjengwa acha unazi wako waki ccm hao wanachama zaidi ya 600 wako tuonyeshe basi hiyo picha wakiapishwa??
 
" Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe Chama chetu CCM ni Chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete ,Kinana na Mangula ​
​

Yaani safu hiyo ndio nzuri wakati huyo jamaa hapo kwenye red anatumalizia tembo wetu mbugani..?
 
habari yenyewe haijajitosheleza...!au niseme filikunjombe 'hajafunguka' vile wananchi wanataka
 
Kama Njombe kuna tembo waambieni wakimbie wasije wakang'olewa meno
 
Uteuzi wa Mangula ulishaanza kutabiriwa,na Mangula alishaanza kujua kuwa kuna kitu kinakuja!kumbuka Mangula na BWM ni watu wa karibu sana,na wote walitoka kwa pamoja ndani ya chama na wanaongea bado issue nyingi tu,hasa pale awamu ya nne ilipoingia kwa kasi ya ajabu na mtandao wao kujazana ndani chama na serikali!wao walibakia kimya kuona itakuwaje!sasa hao huwa wanaona kuwa chama kinayumba na sababu ni nini!wanajua,JK alipoanza kumshirikisha BWM kwenye issue nyingi za chama na serikali kuomba ushauri,tayari Mangula alishajua (Ubunge wa Jombe Kaskazini) vita ya CCM na CDM(Nyimbo) aliombwa akasidie jahazi ili CCM ishinde na kweli alifanya!baada ya hapo akaombwa kwenda Msumbiji na BWM na wazee wenzake kwenye mkutano mkuu wa Frelimo.alikuwa anajua sana nini kitatokea maana safu aliipanga BWM!alikuwa anasubiri Mwenyekiti amuombe rasmi akiwa Dodoma tayari!kumbuka miaka 4 au 5 iliyopita nadhani hakualikwa au hakutokea kwenye mkutano mkuu wa chama!Tafakari
 
Hayanihusu, acha niende nikapate chai kidogo, then nije nijadiri kuhusu maendeleo.............
 
Uteuzi wa kwako unasubiri ushauriane na mkeo na watoto? Nyie ndiyo wale hata kuongoza nchi unamuliza mkeo kwanza. You must have faster decision.
yanani unapigiwa simu uko bar kuhusu uteuzi wako na wewe bila kutafakari wala kushauriana na familia yako unakubali on the spot.

Jk: Nimekupigia simu nataka nikuteuwe makama mwenyekiti wa ccm bara
mangula: Ahsante mzee nimekubali uteuzi wako. As simple as that!

Kama mambo ndiyo hivi kweli tutaacha kupata majaji vihiyo!
 
Deo ni miongoni mwa mashujaa ambao wako ktk chaka bovu..ndiyo kusema/kukiri udhaifu ni ushujaa, bali uongo ni uoga.
 
sijaona alichowachana, zaidi ya kuwasifu tu wazee wa tembo.
 
Back
Top Bottom