filamu ya " Bohemian Rhapsody".

filamu ya " Bohemian Rhapsody".

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,637
Habari tena waungwana! Kitambo sana sijaongelea kuhusu filamu. Leo nimerudi tena. Jana nilipata kuitazama filamu ya "Bohemian Rhapsody" iliyotoka mwaka wa 2018. Si ajabu imepata kuuzwa sana hadi kupewa tuzo ya Oscar 4 katika kategoria mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwigizaji bora, uchanganyaji bora wa sauti, uhariri bora wa sauti, uhariri bora wa picha au sinema. Huko kwinginek ndiyo usiseme. Kwa ujumla filamu imeshinda tuzo 21 hadi sasa na teuzi 57. Kwa filamu ya wasifu hii imeshinda tuzo nyingi sana. Bahati mbaya tu, sifa zote hakuzipata mwongozaji wa filamu hii bwana Bryan Singer, kwa sababu tu, ati kuna madai ya chokochoko za kinyanyasaji za kingono zilizoibuliwa.

Rami Malek amecheza kama Freddy Mercury na kwa hakika ameuvaa uhusika vilivyo. Naweza kusema kwa maoni yangu ni kwamba, filamu hii imeshobokewa sana na mashoga kwa sababu tu wamedhihirisha hata mashoga wanaweza kuwa na maarifa na kuweza kufika mbali licha ya tofauti zao katika jamii. Ilinichukua muda kuitazama tangu nilivyoipata. Haikuwa rahisi hata kidogo. Hatimaye jana tarehe 4 Aprili nikainza mwanzo mpaka mwisho.

Kwa kusema ukweli tu, sikuwahi kumfuatilia Freddie Mercury hapo awali. Japo nilifahamu kupitai makala mbalimbali wakimtaja kama mfalme wa Rock lakini sikutaka kabisa kuzifuatilia habari zake. Kulingana na filamu, Mercury anaonekana hakuwa mtu wa kuburuzwa wala kutaka kusikia mawazo ya wazee wake. Aliamini katika kile anachokifanya na hajutii nafsi yake kwa kukifanya. Siku moja alimwambia baba yake haitwi tena Farrokh Bulsa, bali Freddie na baadaye akabadili hadi ubini wake na kuwa Mercury kisheria, yaani, Freddie Mercury.

Tofauti na baba yake, mama yake amekuwa mtu wa kumuunga mkono mwanawe kwa kila analolifanya. Haijalishi zuri au baya. Usishangae, malezi ya uzunguni mtoto akifika miaka 18 huna cha kumpangia. Katika filamu tunaona Freddie hachugui nguo za kuvaa, mwendo wa kutembea, wala kupenda anachokipenda. Alianza kuvaa nguo na wigi za kike, polepole akajenga uhusiano na binti mmoja aliyeitwa Mary. Alikutana naye katika ukumbi wa disko.

Ngoja tuanze mwanzo, awali Freddie alikuwa mbeba mizigo wa uwanja wa ndege. Siku moja akiwa katika mihanjo yake, akakutana na bendi inayopiga maarufu kama "Smile" ikitumbuiza. Alipenda sana mtindo wao. Akaulizia wako wapi akaambiwa wapo uwani. Anasogea eneo la uwani kwa lengo la kuwapongeza, Roger anamjibu "ahsante kwa pongezi lakini bendi ishakufa mwimbaji mkuu amesepa hata tena!" Freddie anawaambia anaweza kujaribu kuwa mwimbaji wao, lakini Roger anamsanifu njino zake ati sio kwa njino hizo. Akawajaribia kuimba pale ikatoka sauti ya ajabu. Walibloo mapigo. Wakaungana naye mambo yakawa mambo.

Freddie ana mawazo ya mbali na si kama ya mwimbaji wa zamani. Alitaka bendi ifike mbali na iwe na jina la kipekee sana. Na ndivyo ilivyokuwa. Akabadili jina na kuita Queen. Akajenga uhusiano na Mary, akawa kila siku hakosekani mazoezini. Bendi ikapanda jina hadi kupeleka kupata mameneja. Mercury akawa mkubwa kupita kiasi. Katika bendi kukawa na meneja binafsi wa Mercury na meneja wa bendi. Paul Prenter alikuwa meneja wa Mercury na baadaye akaja kuwa mpenzi wake. Huyu ni Paul Prenter ni mbinafsi na mpotevu kwelikweli. Huenda ikawa huyu ndiye aliyemfanya aingie moja kwa moja katika kupenda wanaume wenzake japo hisia alikuwa nazo tangu zamani lakini uthubutu ulikuwa mdogo.

Meneja wao bwana "John Reid" aliwaingiza katika dili kubwakubwa hadi kuingia mkataba na "EMI Records" na kurekodi kazi chungunzima. Mkataba huu uliwafanya wapate ziara za kufanya tumbuizo katika matamasha makubwa huko nchini Marekani na kwengineko duniani. Kilikuwa kipindi hiki Mercury alipomchumbia Mary Austin. Mwaka wa 1975, wakati wanarekodi albamu ya nne, ya "A Night at the Opera," wanaondoka EMI kwa sababu mkurugenzi wa EMI Ray Foster anakataa kuutoa wimbo wa "Bohemian Rhapsody" kama wimbo kiongozi kutoka katika albamu hiyo kwa kisingizio cha kwamba wimbo ni mrefu sana kwa dakika sita ilhali kipimo sanifu cha wimbo ni dakika tatu.

Freddie anaona uhanithi huo, wanajitoa EMI, Freddie anasogea kwa kwa DJ Kenny Everett na kuutoa wimbo huo redioni. Kwa kusikilizwa kwa mara ya kwanza, wimbo unakuwa maarufu kupita maelezo licha ya kutolewa kasoro nyingi za watahakiki. Katika ziara ya matamasha ya kidunia, Freddie anaanzisha mahusiano ya kimapenzi na Paul Prenter. Anamsogelea Mary, anampa za uso kama yeye ni "biasexual", yaani, mtu asiyejionea tofauti ya kuwa na mahusiano kati ya mwanaume au mwanamke. Freddie zoazoa, anakaza mwanaume, anakaza wanawake. Kifupi alikuwa chenji bin chenji. MSUMENO wakati huku na huku! Au mchicha MWIBA! Kwa haika jumuia ya mashoga wanajivunia kuwa na Mercury!

Mary anamwambia wewe si tu biasexual, wewe ni shoga! Hakuna jina ambalo angelipenda amuite tofauti na hilo. Mary anasepa, anaona hana haja ya kuwa na mahusiano na mtu asiyejua utofauti wa mwanamke wala mwanaume. Walibaki kuwa marafiki tu na si wapenzi tena. Akawa anaishia karibu naye baada ya kununua jumba la kifahari mnamo mwaka wa 1980 karibu na nyumba yao. Kivumbi kinatokea kwa bendi baada ya udanganyifu wa Paul. Katika karamu kubwa iliyoandaliwa na Freddie, anakutana na Jim Hutton aliyekuwa mhudumu wake na kumuahidi amtafute pindi atakapoanza kujifunza kujipenda mwenyewe. Freddie hajipendi, hajithamini, anatumia pesa vibaya, hajui kuchagua, si kike, si kiume, twende! Kila mtu anamwona msenge tu, ndiyo maana hata kumshika tako huyu bwana akampa kubwa!

Kufuatia mafanikio ya onesho la "We Will Rock You", Paul anamtengeneza Reid juu ya wazo la Freddie awe msanii wa kujitegemea na aachane na bendi ya Queen. Linamkera Freddie na kupeleka kumfukuza kazi Reid bila kushauriana na wenzake, hali iliyopelekea tofauti katika bendi. Freddie akazidi kuwa mchelewefu katika mazoezi. Katika mkutano wao na waandishi wa habari wa kuchochea mauzo ya albamu ya Queen ya mwaka 1982 Hot Space, Freddie alipelekeshwa na maswali ya maisha binafsi hali iliyopelekea kutoa majibu ya ovyo kwa waandishi. Aliuliza tupo wanne, lakini anaulizwa yeye tu kuhusu maisha yake binafsi. Waulize maswali ya muziki, wao wanauliza maswali binafsi. Kumbe hata MBELE wambeya wapo!

Uhusiano wa Freddie na bendi ukaanza kwenda kombo baada ya kutoa video ya wimbo wa “I Want to Break Free”, ambao walionekana wamevaia mavazi ya kike ulizuiwa katika MTV. Freddie alikasirika sana na kusema hawapangiwi cha kuvaa. Katika mkutano wao asubuhi iliyofuata Freddie anatangaza dili lake la dola milioni nne alililoingia na CBS Records kwa minajili ya kuwa mwimbaji wa kujitegemea. Hatua hiyo inaua bendi papo hapo. Yakatokea maneno ya karaha baina yao sana, Freddie aliwaambia wenzake kama hana cha kujivunia kama wao, wana wake na watoto. Yeye ana nini? Wakamjibu kama ana milioni nne.

Seti hii filamu inasikitisha sana na ile ya walipopata habari ya kwamba wamekubaliwa kuingia mkataba na EMI, Freddie alipomwambia Mary kama yeye hajachugui wa kulala naye, na tamasha la mwisho kufanya wakiwa na Queen mnamo tarehe 13 Julai 1985. Tuendelee, mwaka wa 1984, Freddie anahamia mjini Munich kufanyakazi juu ya albamu yake ya kujitegemea iliyojulikana kwa jina la Mr. Bad Guy. Akiwa huko, anajikuta katika mazingira ya kupenda kubwia unga, ulevi na mahusiano na mashoga wengiwengi akiwa na Paul-- hali ambayo ilipelekea mwonekano wake kuzidi kuwa mgonjwa. Mary, ambaye sasa ni mjamzito wa mpenzi wake mpya, anaguswa na hali ya Freddie, anamsihi arudi tena katika bendi.

Kwa malumbano makubwa, Freddie anarudi na kuwataka radhi wenzake na hatimaye kurudi tena. Wanapata taarifa ya kushiriki katika tamasha lililoandaliwa na Bob Geldof la kujitolea la Live Aid katika uwanja wa Wembley.
Hali ya kugundua ya kwamba Paul hampi taarifa, Freddie anamchana Paul, na kuachana naye mazima. Amechoshwa na tabia zake za uwongo na udanganyifu, lakini Paul anarudisha kisasi kwa kwenda kutoa siri za maisha yake ya kimapenzi kupitia TV. Anasema Freddie ni buludoza, hachagui pa kukanyaga, wanawake twende, wanaume twende. Katika kurudi kwake Freddie London, nyimbo zitakazotungwa na wanachama wa bendi zitakuwa ni za Queen na si huyu wala huyu. Wakati meneja wao mpya "Jim Beach" akishughulikia suala lao la kutumbuiza katika tamasha la UKIMWI bure la Live Aid. Wanakubaliwa na kupewa kushiriki nafasi ya mwisho. Kwa habari za UKIMWI kuenea duniani, Freddie anagundua kama anao; anatoa siri hii kwa marafiki zake wa karibu katika bendi na kukumbatiana kwa kumpa pole. Freddie anawachimba mkwara hataki pole zao wala maneno ya faraja kwani hayatafanya kazi kwake.

Katika siku ya onesho la Live Aid, Freddie anaungana na Jim, Mary, na familia yake. Anaenda kwa baba na mama yake kuwaaga, anajua kabisa hana siku nyingi za kuishi duniani. Lakini anafahamu kuna urithi kaacha. Onesho la bure anamwambia mama yake juu ya hili. Kwa mara ya kwanza anarejea maneno ya hekima ya baba yake kuhusu matendo mema kwa waja wema. Freddie anamuaga baba na mama yake kisha huyo anaenda zake katika tamasha. Bendi inatumbuiza nyimbo kama "Bohemian Rhapsody", "Radio Ga Ga", "Hammer to Fall" na "We Are the Champions", hali ambayo ilisaidia sana kuongeza michango ya kujitolea ya onesho hili na kupata mafanikio makubwa hakuna mfano. Filamu inaisha na ikionesha jinsi Freddie alivyokufa mnamo Novemba 24, 1991 akiwa na umri wa miaka 45, kifo kilichotokana na enimonia ya UKIMWI, ukaribu uliobaki kati ya Jim na Mary, kuanzishwa kwa taasisi ya Mercury Phoenix Trust iliyoanzishwa kwa ajili ya kupambana na UKIMWI duniani.

MWISHO!

MAONI:
Scene ya mwisho inasikitisha sana. Kwa hakika Rami Malek ana stahili tuzo na pongezi kwa kazi yake. Kama Freddie kuanzia mwonekano hadi kijasho kilichomtoka. Ukiacha yale mambo ambayo yapo nje kimaadili kwa Freddie, bado anabaki mwanamuziki bora wa muda wote. Imenipa hamasa ya kuandika kuhusu Freddie kule Wikipedia ya Kiswahili.
RIP Freddie Mercury!
TAZAMA: Queen - Live AID 1985 Full Concert (Best Version) (HD) = https://www.youtube.com/
watch?v=ktYlzVYQbwY
Nime enjoy baada ya kuiona katika filamu!
 
Ok pia kitu kizur. Zaid mecury alikua ni mzanzibar kazaliwa nakakua zenj na wakaz wa. Zenj wanalifaham ilona nyumba yao inafahamika kwa umaharufu kivutio cha utali
 
vipi hawajaonesha kuwa Freddy ni mzaliwa wa mji mkongwe Zanzibar? yeye na wazazi wake walikimbia kujiokoa baada ya mapinduzi ya Okello.
 
Back
Top Bottom