greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,764
- 3,227
Nili ipenda Sana hii yellow cardWIKI YA PILIWiki hii nakupendekezea za kuchangamsha Ubongo na kukupa tabasamu la kutosha, mana sikukuu nyingi.
1.MAD MAX: FURY ROAD
Waigizaji : Tom Hardy,Charlize Theron na Nicholous Houltz
Muongozaji : George Miller
Mahadhi : Action
Mwaka : 2015
Inahusu : Katika dunia ambayo imeangamia kwa Vita.Max anakamatwa na kupelekwa katika ngoma ya Immortal Joe ,ambaye watu wake wanaamini Joe hafi ,anaishi Milele.
Max anatumika kuchangia vijana wa Joe damu.Akiwa kwenye msafara wa kwenda kubadilishana mafuta na silaha, atashirikiana na mkuu wa msafara (Furiosa) katika kutoroka.
-anza wiki kwa hii movie ,ni action mwanzo mwisho.
-Iliigizwa Botswana
View attachment 2962499
2.ETERNAL SUNSHINE OF SPOTLESS MIND
Waigizaji : Jim Carrey,Kate Winslet,Mark
Muongozaji: Michel Gondry
Mahadhi : Drama + Romance + Science fiction
Mwaka : 2004
Inahusu : Joel Baada ya kuachana na mpenzi wake ,ataenda kwenye kampuni ya Lacuna (inahusika na ufutaji wa kumbukumbu kwenye ubongo) ili afute kumbukumbu za penzi lake na Clementine.
Wakati wa tukio la kufuta kumbukumbu,Joel atapata kumbukumbu ya matukio mazuri katika penzi lao ....
-Pata kumuona Jim Carey nje ya vichekesho
-Itafaa ukiiangalia Alhamis/Ijumaa
View attachment 2962498
3.YELLOW CARD
Waigizaji : Leroy Gopal,Ratidzo mambo,Lazarus Boora
Muongozaji : John Riber
Mahadhi: Romantic+Comedy
Mwaka : 2000
Tiyane kijana mwenye kipaji cha mpira anapata funzo kwa kufanya ngono bila kinga, ambapo atapata misusuko katika kulea mtoto huku akifukuzia ndoto zake.
-utacheka ,utaelimika na kuwa Inspired.
-Kaa na familia Jumamosi ,ufurahi.
View attachment 2962497
Asante kwa taarifa
Vijana wa 2000 wengi wao hawajaiona hiiNili ipenda Sana hii yellow card
Kali SanaVijana wa 2000 wengi wao hawajaiona hii
Hapo nipo kwenye kochi nimefungulia ITV mida ya saa 3,ndiyo nacheki Movie hiyo....Kali Sana
Angalia na hiyo spl 2 ni kisanga na nusu.Hapo nipo kwenye kochi nimefungulia ITV mida ya saa 3,ndiyo nacheki Movie hiyo....
Nitaisaka hiyo,,nina likizo ndefu sana ...Angalia na hiyo spl 2 ni kisanga na nusu.
Steven Spielberg hanaga kazi mbovuzifuatazo ni movie 4 nzuri ambazo unaweza zicheki wiki hii ukiwa umepimzika.
Kwenye orodha zipo 4, ila Angalia angalau 3.
WIKI YA KWANZA
SAVING PRIVATE RYAN
waigizaji: Tom Hanks, Matt Damon, Vin Disel
Muongozaji: Steven Spielberg
Mwaka: 1999
Mahadhi, Drama + Kivita
Inahusu: Baada Wizara ya Vita ya Marekani kupata taarifa kuwa wanajeshi wake wa4 wote familia moja wamefariki, Wizara inamtuma Kapteni Miller na wenzake kwenda kumchukua ndugu wa mwisho wa familia ya Ryan, ili arudi nyumbani....
Siku ya kuangalia: Jumamosi au Jumapili
- Bonge la movie, Kuna actions nzuri.
- Moja ya filam za mwanzo Vin Disel kuigiza
View attachment 2955714
A STAR IS BORN
Waigizaji: Bradley Cooper, Lady Gaga na Sam Elliot
Muongozaji: Bradley Cooper
Mahadhi, Drama + Romance + Musical
Yahusu: Jack muimbaji maarufu wa mahadhi ya country, pia ni urahibu wa madawa ya kulevya na pombe. Siku anatembelea baa moja hivi, wakati yupo hapo mwanadada Ally ataimba na kumshangaza Jack.
Siku: Alhamisi na Ijumaa
- Kuna nyimbo nzuri na Lady gaga ni moto
- Bradley anazidi zihirisha ubora wake katika Uigizaji na uongozaji
View attachment 2955716
CHOZI LA BABA
Waigizaji: Mzee Majuto
Mahadhi: Drama
Mwaka : 1997
Inahusu: Mtoto wa Mzee Majuto ni tajiri mfanyakazi serikalini na amemuoa Bi. Siyawezi.
Mzee Majuto atafunga safari mjini na kwenda kukaa kwa mwanaye, Mateso atakayokumbana nayo mh...
- Kabla ya kuanza vichekesho, majuto alikuwa moto kwenye Drama
- Ngumu kuipata mtaani, ila utafurahia ukiiona.
CATCH ME IF YOU CAN
waigizaji:Tom Hanks ,Leonardo Di Caprio na Christopher Walken
Muongozaji:Steven Spielberg
Mahadhi : Drama + Crime
Inahusu : Baada ya wazazi wake kutarakiana, Frank anatoroka nyumbani na kwenda kuanza Maisha yake. Ili kumudu maisha Frank atakuwa bingwa wa kufoji Cheki za Benki na nyara zinazomuwezesha kuwa Daktari, Rubani hadi wakili.
- Itakjondoa Katika hali ya kukata tama
Siku : Jumatatu hadi Ijumaa
View attachment 2955721
Muwe na wiki njema
Huyo ni mtaalam kweli kweli....anajua namna kukamata hisia za watazamajiSteven Spielberg hanaga kazi mbovu