kkarumekenge
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 1,708
- 1,028
Ligi Kuu Soka Tanzania inafikia ukingoni. Inachezwa pote, baa, magazetini, tv,sokoni, viwanjani nk. Uamuzi wa kamati ya saa 72 umezua jambo na natabiri utamu wote wa ligi hii pamoja na makandokando yake umeishia hapo. Je, ni kweli Simba hawakustahili pointi tatu? Je, ni kweli mchezo wake na Kagera haukuwa na kumbukumbu zozote? Je, Yanga na Africa Ryon kulikuwa na malalamiko, ya timu gani naje, hayakusikilizwa? Je, Mwesigwa (Katibu Mkuu wa Yanga zamani) na Malinzi ambaye pia aliwahi kuwa kiongozi/mfadhili wa Yanga hawatakuwa na mkono katika hili ukizingatia pia kwamba wote wanatoka mkoa wa Kagera nk, nk. Haya, kama malalamiko ya Yanga yatajadiliwa sasa, je, yale ya ndugu zangu Ndanda dhidi ya Simba nayo yapitiwe? TFF ni kimeo na imeharibu ligi. Karibu Mwakyembe.