Malata Junior
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 3,104
- 2,549
CCM ni chama kinachojinasibu kwamba ni chama cha kidemokrasia! Aidha katiba ya chama hicho inaainisha wazi kwamba kila mwanachama ana haki ya kugombea nafasi yoyote ile ikiwemo ya mwenyekiti wa chama Taifa.
Katiba inaeleza pia muda wa viongozi wa chama hicho kukaa madarakani ni miaka mitano kila baada ya uchaguzi.
Leo hii tunaona figisufigisu zimeanza za kutaka kumng'oa madarakani mwenyekiti Kikwete kabla ya muda wake kwisha kinyume na katiba.Tumesikia pia eti kuna mpango wa 'kumkabidhi' madaraka ya mwenyekiti wa Taifa Rais Magufuli.
Tulitarajia kusikia wanachama wakitangaziwa tarehe ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ili atakayeshinda ndiyo akiongoze chama hicho lakini huko kinachotaka kufanyika ni ukiukwaji mkubwa WA demokrasia na katiba ya chama hicho.
Haya yangefanyika kwenye vyama vingine vya siasa tungesikia kelele nyingi kutoka CCM na vyombo vyama vya propaganda ikiwemo ofisi ya msajili WA vyama vya siasa. Tuliona jinsi msajili alivyoingilia uchaguzi wa CHADEMA mpaka kufikia hatua ya kutaka kuwapangia nani agombee na nani asigombee!
Tunamtaka msajili aingilie kati ukiukwaji huu WA demokrasia na katiba ya chama hicho unaofanywa na CCM. Najiuliza kama wanasigina katiba ya chama chao wataweza kuilinda katiba ya nchi?